Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,602
Bila kujali uhalisia wa taarifa yoyote, ila ningependa kumuombea siha njema Rais Magufuli, aje aendelee na kazi zake.
Japo kuna baadhi ya sera zake sikubaliani nae, ila niseme tu kuna mambo mimi Magufuli namuunga mkono kabisa na ninaona yupo sahihi.
Lakini pia ningependa, pindi ataporejea kazini, afanyie kazi changamoto ambazo watu wamekuwa wakimlalamikia.
1) Kuna suala la kodi kwa wafanya biashara.
2) Kuna issue sa upendeleo wa kikabila, kikanda, na kidini ambavyo watu wanalalamika sana kipindi hiki kwamba vimeshamiri.
3) Kuna masuala ya utawala wa haki na sheria ambao umedorora kipindi hiki.
4) Kuna suala la katiba mpya, hiki bado ni kilio kikubwa kwa watanzania.
5. Diplomasia njema na majirani
Endapo Magufuli akiondoka madarakani bila kutatua hizo changamoto hapo juu, yale yote mazuri aliyoyafanya yatasahaulika mapema sana.
Isitoshe pia, kama asipotekeleza hivi vilio vya wengi, sioni kama mfumo wa Chama Cha Mapinduzi utaweza kufanya mabadiliko yoyote.
Bado system ya CCM itabaki kuwa tatizo. With or without Magufuli, bado kutakuwa na changamoto kubwa sana.