Status
Not open for further replies.
Hii nimeipenda!Hakuna nchi iliyoendelea ambayo inatumia lugha isiyoeelweka kwa wengi!Ndio maana hapa TZ ufaulu hushuka kadri mtu anavyopanda juu kwa sababu lugha inaendelea kuwa ngumu zaidi!Tuanze na kiswahili nadhani hata mikataba tutaingia vzr sn
 
Kabla ya kubadili lugha ya ufundishwaji iwe kiswahili lazima atengeneze fursa za ajira ama namna ya kuwa- Enable hao wahitimu watakao maliza chuo kikuu huku hawawezi kuongea Kiingereza kwa usahihi.....

Kwa sasa ajira nyingi zinatolewa na sekta binafsi ambazo wawekezaji ni Wazungu na sifa ya kwanza ili upate ajira ni uwe-fluent kwenye kiingereza huoni hapo soko la ajira tunalikabidhi kwa ndugu zetu Wakenya.....

Hizo nchi ulizozitaja zinajitosheleza karibia kwa kila kitu hazikuitaji sana wewe Mtanzania uende kuwekeza kwao ili wananchi wake wapate ajira...Ila sisi tunawahitaji sana hao...
 
Kabla hujalaumu utendaji Wa rais katika serikali yake, ni vyema ukazingatia haya ili kujua wapi kafanya vizuri tumpongeze, na wapi kapwaya tumshauri aboreshe!
Zifuatazo ni alama za ufaulu katika utendaji wake;
1. Kubana matumizi (B)
2. Nidhamu ya wafanyakazi (A)
3. Huduma za Jamii (D)
4. Miundombinu (C)
5. Mawasiliano (D)
6. Mahusiano ya kimataifa (E)
7. Uthubutu Wa kutoa maamuzi (A)
8. Safari za nje (F)
9. Uhuru Wa Demokrasia (F)
10. Uhuru Wa kujieleza (E)
11. Ajira (F)
12. Kuthibiti Mfumuko Wa bei (E)
13. Ukusanyaji mapato (B)
14. Ubora Wa elimu (C)
15. Kurinda Mali za raia (C)
16. Kuchangia majanga (F)
============================
Je; kuna uwezekano hizo (F) zikaondoka Kwa mda uliobaki?
 
Magufuri (JPM) tunaomba report ya Tume ya pili ''Makinikia''ulipokelee ikulu ndogo KAHAMA au GEITA
upload_2017-6-3_10-36-25.jpeg

Shikamoo.

Salute commende in Chief

Tunashukuru kwa taarifa ya tume ya kwanza ya Prof Mrumma. Asilimia 120% imekidhi aja kwa sisi waathirika wa Migodini na vijiji jirani na nchi kwa ujumla; Tunashukuru kwa kuufumbua umma utajiri uliopo kanda ya ziwa ambao umejenga jiji la mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa.

Ombi letu tunaomba mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya muungano ; Report ya pili ambayo tunategemea utaipokea siku chache au wiki za karibuni tunaomba uje uipokelee mkoa Geita Ikulu ndogo au ikulu ndogo ya kahama. Sisi wachimbaji wadogo na wananchi wa kanda ya ziwa tupo tayari kuupokea ugeni huo mkubwa kwa furaha na shangwe.

Itakuwa ni faraja kwetu na heshima ya pekee kwa sisi wananchi; Kupokea report kwenye kitovu cha Dhahabu.



Tunashukuru iwapo ombi letu litafikiliwa na kujibiwa vema; Ili Dunia ijue na ulimwengu wajue

wao wameenda UK sisi karibu ikulu ndogo kati ya hizi; Geita au Kahama

WABEJA SANA, WABEJA KURUMBA.



Wanakijiji wanaozunguka migodi .

KAKOLA, BULYANKULU , BUZWAGI, MATABE, TULAWAKA, NORTH MARA, BAKRIFU, MGUSU , NYARUGUSU , NYAKANZI,RUNZEWE.

karibu sana karibuni watanzania tupokee Repoti .
upload_2017-6-3_10-38-33.jpeg

 
Mh Rais nianze kwa kukupa pongezi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa Tanzania mpya isiyo na rushwa, uonevu, dhuluma wala ubaguzi. Mungu akubariki, akulinde na kukutinza. Ulinzi wa Malaika na jeshi la mbinguni uwe nguzo yako ulalapo na utembeapo.

Mh Rais najua mtu kama mimi siwezi kukuona ana kwa ana kuzungumza lakini kupitia hapa unaweza kupata ushauri wangu na maoni yangu hasa juu ya faini za barabarani ambazo zinatozwa na askari polisi wetu wa kikosi cha usalama barabarani.

Mh Rais, vijana wako hawa wanafanya kazi nzuri ya kuthibiti makosa ya barabarani. Kilichonifanya niamue kuandika ushauri wangu kwako ni taarifa ya makusanyo ya Mwezi Januari hadi Mei mwaka huu ambayo inafikiw takribani 12 na ushee Bilioni tena kwa mkoa mmoja tu wa Dar es salaam.

Mh Rais, jeshi letu la polisi linakabiliwa na changamoto nyingi sana. Mimi kama raia ninaweza nisizijue zote lakini kwa uchache ni nyumba za kuishi zenye hadhi ya kiaskari. Askari wetu hawa wanaofanya kazi kubwa barabarani na wale wanaolinda raia na mali zao wanaishi nyumba za ajabu ajabu sana ambazo hazina hadhi kabisa.

Mh Rais, ushauri wangu kwako kama Rais wetu, Amiri Jeshi, baba na mlezi naomba mimi niliye mdogo nishauri angalau hizi pesa ambazo vijana wetu wanakusanya kwa makosa ya barabarani kwa sehemu zisaidie kuondoa kero ya nyumba za askari. Mh mathalani kati ya hizo bilioni 12 na ushee walizokusanya wakitengewa hata bilioni 1 kwa mwezi zikaelekezwa kujenga makazi ya Askari tatizo hili lingemalizika ndani ya kipindi kifupi.

Mh Rais, nikushukuru kwa kazi nzuri naomba kuwasilisha ushauri wangu. Najua unasoma au vijana wako wanasoma. Naomba uusikilize ushauri wangu na ukiona unafaa basi ufanyiwe kazi ili tujenge Jeshi letu imara lakini lenye afya kuanzia nyumbani hadi Kazini.

Mh naomba kuwasilisha.
 
Tuache hizi longolongo za uzalendo sasa,zimepitwa na wakati.Mara wapiga dili sijui mafisadi na wala rushwa mambo ya kizamani hayo. Mhenga mkuu aliyezifanya mbingu na nchi alishasema ni halali kwa mlawi kula vya madhabahuni.
Unategemea nini kuniweka juu ya hazina yako wakati nina kiu na njaa balaa!naanzaje mimi kutunza hiyo hazina bila kuitiatia mkono?
Njaa siyo mchezo,Mfalme Daudi alikula mikate ya wonyesho akijua si halali kwake, Hivi vijichenji mnavyo walipa watumishi wenu havikidhi njaa zao mjue.Lipeni mishahara ya maana muone watu wanavyopiga kazi.Kazi na njaa ni kama mbingu na ardhi bana.
Hebu jaribuni hilo mjionee maajabu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Tuache hizi longolongo za uzalendo sasa,zimepitwa na wakati.Mara wapiga dili sijui mafisadi na wala rushwa mambo ya kizamani hayo. Mhenga mkuu aliyezifanya mbingu na nchi alishasema ni halali kwa mlawi kula vya madhabahuni.
Unategemea nini kuniweka juu ya hazina yako wakati nina kiu na njaa balaa!naanzaje mimi kutunza hiyo hazina bila kuitiatia mkono?
Njaa siyo mchezo,Mfalme Daudi alikula mikate ya wonyesho akijua si halali kwake, Hivi vijichenji mnavyo walipa watumishi wenu havikidhi njaa zao mjue.Lipeni mishahara ya maana muone watu wanavyopiga kazi.Kazi na njaa ni kama mbingu na ardhi bana.
Hebu jaribuni hilo mjionee maajabu.

Post sent using JamiiForums mobile app


Ni kama Yai na Kuku kipi kilianza, sasa hela za kuwalipa Wafanyakazi vizuri zitatoka wapi kama hawafanyi kazi kwa bidii?
 
Ni kama Yai na Kuku kipi kilianza, sasa hela za kuwalipa Wafanyakazi vizuri zitatoka wapi kama hawafanyi kazi kwa bidii?
Kwani hizo wanazojilipa wao zinatoka wapi?tugawane hizo hizo sawa bin sawia,sote tule na tunywe.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kenya inaongoza kwa ufisadi...ila maendeleo yako juu yetu... Tatizo la serikali yetu ni wanasiasa kuingilia mambo ya kitaalamu... Na juzi nilimsikia kenyatta akijipongeza kwa hili...
 
Kwani hizo wanazojilipa wao zinatoka wapi?tugawane hizo hizo sawa bin sawia,sote tule na tunywe.

Post sent using JamiiForums mobile app


Hilo haliwezekani, hata wakiacha kujilipa hata shilingi na kufanya kazi ya kujitolea hizo fedha bado hazitatosha kulipa kila Mtanzania vizuri, maadamu hkn uzalishaji hakuwezi kuwa na fedha ya maisha mazuri!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom