Asante Hayati Magufuli, pongezi Rais Samia

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
ASANTE DKT.JPM ,PONGEZI DKT.SAMIA

Na.Amon Nguma.

Tarehe 17 Machi mwaka huu wa 2024 tumetimiza miaka mitatu tangu kufariki Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati.Dkt.John Pombe Magufuli lakini miaka mitatu ya Uongozi wa aliyepokea kijiti Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita.

Tunamshukuru Mungu na kumshukuru Hayati Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri aliyoianzisha ya kimapinduzi na kimaendeleo lakini pia tunamshukuru Mungu na kumpongeza Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza kazi ya kimapinduzi na kuanzisha kazi mpya ya mapinduzi mengine ya kimaendeleo .

Lile Bwawa la kuzalisha Umeme Julius Nyerere lililokuwa chini ya asilimia 50 ya utekelezaji sasa limekamilika na Mtambo mmoja umeshawashwa na kuingiza umeme Megawati 235 kwenye Gridi ya Taifa na Mtambo wa Pili kuwashwa mwezi April ,Asante Hayati Magufuli na Pongezi Dkt.Samia kuendeleza kazi.

Ile Reli ya Kisasa (SGR) ambayo utekelezaji ulikuwa umeanza kwa vipande viwili sasa chini ya Dkt.Samia vimezinduliwa vipande vingine vinne mpaka Kigoma na sasa kupelekwa kwa nchi jirani na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Kimkakati katika Biashara na Usafirishaji ,kwa hakika ndege wafananao huruka pamoja ,dhamira za viongozi hawa zilikuwa moja .Asante Hayati Magufuli kwa kuanzisha kazi na Pongezi Dkt.Samia kuendeleza kazi.

Dkt.Magufuli akiwa Rais na Dkt.Samia akiwa Makamu walianzisha Elimu bila ada kuanzia shule ya Msingi mpaka kidato cha nne leo miaka mitatu baadae Rais Samia ameendelea na mpango huo na kuongeza mpaka kidato cha sita na si hivyo tu bali kuanzisha Mikopo ya Elimu kwa Vyuo vya kati na kuongeza bajeti ya mikopo vyuo vikuu .Kwa mafanikio haya tunawapongeza na kuwashukuru Viongozi wetu hawa wawili .

2015 Shirika letu la ndege lilikuwa ICU lakini kwa maono ya Dkt.Magufuli na Dkt.Samia kama Rais na Makamu wake walilifufua Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)na kununua ndege 11 ,leo tunapoadhimisha miaka 3 ya Uongozi wa Dkt.Samia tunafurahia kuendelea kwa kazi hii ,ndege nyengine tano zimenunuliwa ikiwemo ya mizigo ,leo shirika linafanya Biashara .Asante Dkt.Magufuli kwa kuanzisha kazi pongezi Dkt.Samia kwa kuendeleza na kuanzisha kazi mpya.

Tunaadhimisha miaka mitatu hii kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa Barabara na Madaraja kuanzia Dar es Salaam mpaka Kigoma na maeneo mengi nchini .

Baada ya mpango wa Elimu bila Ada kuanzishwa wanafunzi wengi wameandikishwa na kupelekea upungufu wa Miundombinu lakini tumeshuhudia Mapinduzi mapya na makubwa chini ya Uongozi wa Dkt.Samia ya ujenzi wa Madarasa zaidi ya 20000 kwa miaka 2 ,hili si jambo dogo ,pongezi nyingi Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Miaka Mitatu ya Uongozi wa Dkt.Samia tumeona mapinduzi mapya aliyoyafanya katika sekta ya Kilimo ,kuongeza bajeti kutoka Bilioni 294 mpaka zaidi ya Bilioni 700 na sasa inakaribia Trilioni hii ni udhihirisho kuwa Rais.Dkt.Samia ameamua kuwainua Watanzania kupitia sekta ya Kilimo ,ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji ,Tafiti,Ruzuku ya Mbolea& Mbegu ,Mradi wa BBT(Jenga Kesho Iliyo Bora).Haya ni mapinduzi mapya na makubwa kwa watanzania ,Asante na pongezi Dkt.Samia kwa hatua hii na kila la kheri kwa hatua zinazofuata.

Mafanikio ni makubwa na mengi katika sekta zote ikiwemo Afya ,Haki ,Michezo, Demokrasia nakadhalika.Haya ni mafanikio ya kazi aliyoianzisha Dkt.Magufuli na kuendelezwa kwa viwango na Dkt.Samia lakini pia kazi mpya za kimapinduzi zilizoanzishwa na Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunaadhimisha miaka mitatu tangu atutoke Hayati. Dkt.Magufuli na wakati huohuo tunatimiza miaka mitatu ya kazi na mafanikio chini ya Uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

kazi Iendelee

Amon Nguma
0620615659
0788613648 .
IMG-20240317-WA0005.jpg
 
Kama kweli vile! Upo kundi gani maana muhusika alikataa hiyo mambo, Alafu uwe unapokea simu ili tukurahisishie kutoboa.
 
0788613648 .View attachment 2936982
🤝🤝
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom