Umeongea kimbea mbea mno, wahuni wanao mhujumu ni wale wahuni wa pwani na wababa wakambo sio sukuma gang wala team magufuli, Kali* we.
 
Mama Samia,
1. Unajua kuwa una maadui wa ile timu aliyoiacha "mwenzio"?
2. Unajua hao ndugu wa mwezio hawajaridhika Bado wewe kuwepo hapo?
3. Unajua kuwa kuna hujuma dhidi yako? Unahujumiwa nawe umejisahau.

Sasa mama umepigwa hujuma nzito, huku mtaani haunogi, wasikupambe hao wanaokubebea miavuli, wanakudanganya kulinda ugali wao. Watu wana chuki na wewe.

Fanya hivi.

(a) Mtoe FREEMAN MBOWE gerezani kupitia DPP, hapo umehujumiwa na hujashtuka(umepigwa kanyanga na wazandiki, mmoja huyo mvaa gwanda la policcm).

Ukitaka uupige mwingi, Mtoe mwenyekiti wa chama Chao hao CHADEMA na weka maridhiano nao, naapa utakuwa umeupiga mwingi.

(b) Kuna wajinga wanakuhujumu kwenye upandaji wa bidhaa, kaa chini, utafakari, una vyanzo vingi vya kupata taarifa, ila kwa hapa umepigwa.

Kidumu chama chenu Cha Mapinduzi!!!!!!!!
Hii imekaa kama blackmailing ya aina fulani. Huyo mrithi wake Rais Samia alimfunga bosi wa TRA kuanzia anaingia ikulu mpaka mwaka 2020 ndio akawaachia. Hivyo suala la Mbowe lisitumike kama njia ya kujengea hoja, sheria ifuate mkondo wake.

Kwamba wanaomchukia ni wengi ni siasa nyingine dhaifu tu. Kuna wanaompenda na wanaongezeka kadri anavyowagusa na mahitaji yao ya kila siku.

Yeye kuwepo hapo ni kwa matakwa ya hayati JPM mwenyewe, hivyo hao wanaoumia mioyo yao watatulia tu wakielewa ukubwa wa mamlaka yake na ukubwa wa kiapo kinachotokana na mamlaka hayo.
 
Kesi iko mahakamani Kama nyinginezo.......

Rais hayuko mahakamani......

Huku mitaani mzunguko wa pesa umeanza kuonekana na mh.Samia ananoga haswa......


#Siempre JMT
Acha hizo, kesi za masheikh wa uamsho zilikuwa mahakamani mbona mlishangilia na kusema mama Samia kawatoa, ana huruma. Iweje kesi ya mbowe ndio mseme eti tuiachie mahakama
 
Acha hizo, kesi za masheikh wa uamsho zilikuwa mahakamani mbona mlishangilia na kusema mama Samia kawatoa, ana huruma. Iweje kesi ya mbowe ndio mseme eti tuiachie mahakama
Kwani anavyowaacha huru wafungwa katika sikukuu kwa kitaifa huwa ni lazima afanye hivyo?!!

Mahakama ndiyo itakayoona Mbowe ana hatia ama laa.....
 
Enzi za utawala wa Magufuli umeme haukua changamoto kabisa,na hata siku ambayo kulikua na marekebisho ya miundombinu ya umeme basi TANESCO walikua wanatoa taarifa siku mbili kabla ya nini kitatokea na masaa ambayo huduma ya umeme haitopatikana.

Sasa tokea mheshimiwa SSH aingie madarakani mambo yamekuwa vice versa,umeme unakatika hovyo tu na tena hata bila taarifa kwa wateja, mfano siku ya leo sehemu kubwa ya Dar haikua na umeme na hakuna hata kiongozi yeyote wa serikali anayejali hilo suala.

My point is, Mama Samia usipokua makini na hawa Tanesco watakujengea chuki kubwa sana kwa wananchi. Nakuomba uwe mkali mama na ikiwezekana tumbua kuanzia waziri wa wizara husika na menejiment ya Tanesco, tuwekee watu wanaojua kuchapa kazi, sio hao uliowaweka kwani ni kama wanakuhujumu tu.
 
Yaani waafrika hua tunapenda kuabudiwa Sana, sijui kwanini wakipata madaraka wanageuka miunguwatu Hawa viumbe inasikitisha Sana

Kwahiyo nchi haiendeshwi Kwa sheria na taratibu ila Kwa matamko ya wanasiasa
Mweeeee mbombo ngafu mwaisa!
 
Wewe umejua wapi pa kuelekeza dukuduku lako nashangaa sana kuona wanaomshambulia Zitto kwa kutoa maoni yake. Wakushambuliwa ni hao wenye mamlaka
 
Back
Top Bottom