Kwanini wapo watu wanamuomba Rais Samia Suluhu kuendelea kuwa Rais wa Tanzania?

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
Na Mwl Udadis, DSM-CBD

Kwa sisi waumini wa makanisa ya Orthodox tunaamini sana katika kweli isiyochanganywa na busara za waja japo tunaheshimu sana imani za watu wengine. Natumia falsafa ya kweli hiyo ninayoiishi kukupa ujumbe ambao unaoweza kukupa picha ya yajayo katika uga wa siasa za Tanzania.

Mpaka sasa, zimebaki takribani siku 295 kuingia katika mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Rais aliyepo madarakani tayari ameonyesha ushawishi mkubwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya wanasiasa kuchagua kwenda kugombea Ubunge na kufuta kabisa wazo la kuufikiria Urais. Baadhi ya sababu za ushawishi huu ni hizi:

1. Rais Samia ameirejesha heshima ya Tanzania katika mawanda ya diplomasia za kimataifa, tija ya jambo hili ni mtambuka lakini ndio msingi wa utekelezaji wa sera ya diplomasia ya uchumi.

2. Rais Samia amefanikiwa kukuza utalii kwa kasi kubwa licha ya athari za Janga la UVIKO-19 lililoharibu kabisa sekta hii na kufanya watu wengi wapoteze ajira. Mfano, kuanzia mwezi August 2023 hadi Feb 2024 tayari watalii wamevuka lengo la mwaka kwa kufikia watalii 1.45M kabla hata mwaka kuisha. Hii ni si ngekewa ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

3. Rais Samia amevunja rekodi Afrika kwa kuweka mazingira wezeshi na ya kuvutia wawekezaji ambapo hivi sasa Tanzania ni kati ya nchi bora 10 Afrika kwa mazingira ya kuvutia wawekezaji. Jambo hili linatokana na sera rafiki kama vile "Blueprint" iliyoasisiwa na Mhe. Rais ikilenga kuondoa vikwazo kwa wawekezaj na wafanyabiashara.

4. Rais Samia anatekeleza sera imara zilizoiwezesha Tanzania kuweza kuhimili mtikisiko ya kimataifa hususani katika bei ya mafuta na vyakula, kwa msingi huo mfumuko wa bei umeendelea kuwa wa chini zaidi ndani ya Afrika mashariki na kati. Hili ji jambo kubwa mno.

5. Rais Samia kupitia mpango wa BOOST na SEQUIP ametekeleza ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kasi ya ajabu, mfano ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara na katika baadhi ya maeneo shule mpya. Mkoa kama Singida zaidi ya madarasa 800 yamejengwa bila mwananchi kubughudhiwa michango.

6. Rais Samia amewezesha kila Wilaya, Mkoa, na Kanda kuwa na Hospitali zinazoenda na hadhi ya ngazi husika. Hakuona haja ya kuwekeza katika majengo tu bali ameenda hatua 100 mbele katika vifaa tiba jambo ambalo limewezesha hata utalii tiba katika baadhi ya mikoa iliyo mipakani na nchi jirani na pia ametoa fedha kusomesha Madaktari Bingwa.

7. Rais Samia katika kilimo amefanya mambo makubwa ajabu, hakuishia tu katika ruzuku ya pembejeo ameamua kutambua thamani ya umwagiliaji kama njia inayoweza kumhakikishia mkulima mavuno ya uhakika ili kutekeleza dhana ya kilimo biashara. Hivi sasa mabonde yote nchini yanayohitaji miundombinu ya umwagiliaji yako katika hatua za kupewa miundombinu. Wazungu hii wanaita "Game changer"

8. Rais Samia hajawaacha wanafunzi elimu ya juu, kwa mara ya kwanza maombi ya kuongezwa kwa posho ya kujikimu kwa wanafunzi elimu ya juu yamefanyiwa kazi, mikopo ya wanafuika inatoka kwa wakati(mambo ya migomo ni historia), Makato ya VRF (6%) yameondolewa kabisa na Ufadhili maalum wa "Samia Scholarships" umeanzishwa. Nini hapo kimebaki?

9. Rais Samia hajaiacha miradi ya kimkakati licha ya gharama kubwa kuhitajika. Hivi sasa watanzania tunatumia umeme wa JNHPP ndoto sasa imekuwa uhalisia (Mradi unaobeba zaidi ya Trilioni 6). Upande wa SGR majaribio yameanza na reli mpya zinajengwa. Daraja la Kigongo Busisi liko mwishoni hivi karibuni litaanza kutumika.

10. Rais Samia hajaacha kaya maskini, fedha zinaendelea kutolewa kwa walengwa wote(TASAF), zaidi wanufaika wanazidi kuongezeka na kuwezeshwa zaidi.

11. Rais Samia hajaacha ajira serikalini, ametoa vibali kwa kila Taasisi yenye uhitaji wa watumishi kutoa ajira haraka na pia, madai ya fedha na malimbikizo ya watumishi yote yamelipwa bila kusahau kupandisha madaraja watumishi wote wenye sifa. Huyu ndiye Rais Samia Suluhu Hassan ambae anakwenda tena kugombea maana asipogombea wananchi tutaandamana kumtaka agombee.

12. Rais Samia hajaacha kuwainua vijana wanaojiajiri, tayari ameweka msamaha wa kodi "grace period", sheria za manunuzi tayari zinatoa upendeleo wa tenda kwa vijana, mradi wa BBT kilimo na mifugo tayari umetoa fursa kwa vijana na hata katika uvuvi boti na zana za uvuvi zinaendelea kutolewa.

Sababu ni nyingi kwanini karibu kila mtanzania anaonyesha nia ya kutamani Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa Rais mpaka 2030 (Mungu akitujalia uzima) kwa ufupi unaweza kusema ni nia yake ya dhati, uzalendo wake, uchapakazi wake, umakini wake na zaidi moyo wake wa upendo na maono sahihi kwa nchi yetu.
 
IMG-20240312-WA0055.jpg
 
Ndani ya miaka miwili hii nimetembelea karibu mikoa 15 ya Tanzania ki ukweli nimeiona mabadiliko makubwa mno mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa sasa Nchi inapiga maendeleo kwa kasi sana
 
Na Mwl Udadis, DSM-CBD

Kwa sisi waumini wa makanisa ya Orthodox tunaamini sana katika kweli isiyochanganywa na busara za waja japo tunaheshimu sana imani za watu wengine...
Hao ni wa "NAFIKI" wanaocheza na akili.za viongozi, hao ni wale wale walisema Magufuli nichaguo la Mungu hivyo aongezewe muda, na ni wale wale walisema Magufuli alipora watu fedha zao.... Na ni wale wale watakuja sema Samia aliharibu Nchi!!!
 
Na Mwl Udadis, DSM-CBD

Kwa sisi waumini wa makanisa ya Orthodox tunaamini sana katika kweli isiyochanganywa na busara za waja japo tunaheshimu sana imani za watu wengine...
Alafu bado anaogopa uchaguzi,

Na anatumia hela nyingi kuwalipa machawa wa kumsifia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom