Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
903
1,000
1616581552047.png
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
 

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
395
1,000
Wakati tuko mbioni kupata Rais mpya wa sita katika awamu ya tano. Tunamsihi sana apate kutekeleza majukumu yake katika Maslahi Mapana ya taifa. Na apate kutambua pia maana ya kauli ya Maslahi Mapana ya taifa. Maana viongozi wengi huamini Maslahi ya taifa Ni katika vitu tu hususa (miundo mbinu, rasili Mali vitu, n.k) na hukomea hapo.

Kiuhalisia si hivyo, Maslahi Mapana ya taifa huanzia kuunganisha taifa lipate kuwa kitu moja bila kujali itkadi za aina yoyote si za kisiasa na si za kiimani na si kikabila wala za kijinsia. Lengo hapa ni taifa lipate kushikamana na kushirikiana bila chuki Wala ubaguzi. Utawala uliopita ndani yake ulikuwa na chuki na ubaguzi wa wazi wazi.

Pili Maslahi Mapana ya taifa ni upande wa kuindaa rasili Mali watu (wananchi), katika fikra na mawazo ya kisasa na kuwaondolea ujinga (kiufupi ni kuwekeza taasisi za elimu katika elimu ya kisasa ya kuendana na Karne ya 21). Elimu ya Sasa iliyipo nchini Ni duni, maana kwa asilimia zaidi ya 80 Ni theory oriented. Wananchi ndio taifa lenyewe, hawa wananchi hutegemea wameandaliwa na elimu ya ubora aina gani.

Kwa uchumi wetu hatuwezi kutoa elimu bure, na tukitoa elimu basi itakuwa Bora na si elimu Bora. Elimu Bora ni gharama.
Sasa Ni Bora tukawa wananchi elfu 20 wenye elimu Bora (quality education, compatible with 21 century environment) na tukawa wananchi million 60 wanaoujua kusoma na kuandika?

Tatu Maslahi Mapana ya taifa ni pamoja na Sera na Sheria wezeshi kwa wananchi wake. Mfano utawala uliopita Sera za Kodi Ni kandamizi, hazimuinui mwananchi. Tukumbuke mwananchi nae anapaswa kuendelea kiuchumi, na serikali inapaswa kuendelea kiuchumi. Sera za Kodi za Sasa so rafiki kwa mwananchi, Bali Ni rafiki kwa serikali. Kwa biashara za watanzania wengi hususa wa mtaji mdogo baada ya makato ya Kodi na Kodi ya pango hujikuta wamepata pesa ya kula, kuvaa, n.k hapati faida ya kumfanya hafungue biashara nyingine, kiufupi apigi hatua nyingine.

4: Maslahi Mapana ya taifa Ni pamoja na utawala Bora na taasisi imara. Tanzania haitaji kiongozi imara inahitaji taasisi imara za kiserikali. Maana taasisi hudumu Karne na Karne, lakini kiongozi ufa au humaliza muda wake. Ndio maana baada Magufuli alivyokufa watu wametandwa na hofu, yote Ni tokana hatuna taasisi imara, serikali ya awamu tano ilisimama si tokana na taasisi imara Bali raisi imara.

Taasisi imara husimikwa na katiba na Sheria za. Nchi, maanake ya Sasa katiba inapaswa kubadilishwa.
 

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,804
2,000
Acha mikwara wewe, mama Samia ndiye amiri jeshi mkuu sasa hivi, na ataongoza nchi kadri kwa style yake sio lazima amuige Magufuli, Magufuli ameshakufa.

Magufuli ali reverse vitu vingi vya Kikwete tu alivyoona havipo sawa, Mwinyi pia ali reverse vingi vya Nyerere ambavyo aliamini havipo sawa, Mkapa hivyo hivyo, Kikwete n.k
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,568
2,000
Mtoa mada wewe endelea tu kuweweseka. Ila muda utakapo wadia, utajikuta unaamini tu ya kwamba, jemedari wako hayupo tena.

Na sasa Nchi iko mikononi mwa mtu mwingine! Tena ni mama! Na sidhani kama anawajibika kutenda kila alichokitenda huyo mtangulizi wake.
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,097
2,000
Wakati tuko mbioni kupata raisi mpya wa sita katika awamu ya tano. Tunamsihi sana apate kutekeleza majukumu yake katika Maslahi Mapana ya taifa. Na apate kutambua pia maana ya kauli ya Maslahi Mapana ya taifa. Maana viongozi wengi huamini Maslahi ya taifa Ni katika vitu tu hususa (miundo mbinu, rasili Mali vitu, n.k) na hukomea hapo.
Labda amchague mtu kama Dr. Slaa awe makamu wa Rais, hao wengine wote tutarudi kuleeeeeeee, Ruksa
 

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,124
2,000
Habari za wakti huu;

Kwanza kabisa nimpe Pole mama yangu ,Samia Hassan Suluhu kwa kuondokewa na Boss wake,Lakini zaidi nimpe hongera kwa kupata fursa ya kuwa RAIS wa Jamhuri katika kipindi ambacho Jemadari mwendazake JPM alikuwa ameweka moja kati ya malengo makubwa sana(Most ambitious goals of the Modern Tanzania) ya kutaka kufanya Tanzania iwe nchi ya kisasa.Lakini Pia niseme tu kwamba Mwendazake JPM amemuachia TAIFA ambalo kwanza ni divided yet united.Lakini pia anayo kazi ya Pembeni ya kufanya Damage control and healing

Sasa nirudi kwenye mada kuhusu nzi.Kuna nzi wengi sana ambao wamezagaa na najua mpaka wakati huu wengi tayari wameshaanza kujisogeza karibu.Kuna nzi wa aina mbili ambao wanajisogeza kwa kasi sana karibu na RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hasan

Nzi wa Aina ya kwanza ni wale ambao walinufaika na Mfumo uliokuwepo zama za Magufuli ambao wanatafuta kila namna kuhakikisha kwamba Maslahi na fursa walizokuwa nazo kisiasa,kijamii na kiuchumi zinaendelea kuwepo na kuna wale Nzi ambao hawakupendezwa na mfumo ule na wengine hata kama waliufaidi lakini hawakuupenda na wengine ambao waliumia na hawakunufaika nao na ambao nao wanasogea kwa kasi kabisa ili waweze kubadili uelekeo wa Upepo.Hawa nzi wote ni nzi hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.

Najua wachache wa nzi hawa unawajua ila pia najua kuna ambao huwajua au hujaweza kuwatambua ila jihadhari nao.Mheshimiwa RAIS ninapoandika waraka huu ninawaona jinsi wanavyoweka mikakati, wengine wanafuatilia historia yako kujua kama kuna kitu wanaweza kukitumia ili kukufikia kwa urahisi uweze kusikia ushauri wao. Mimi nakusisitizia waepuke hawa nzi.Kazi uliyo nayo ni kubwa sana.

Mheshimiwa RAIS, Wewe ni mrithi wa Magufuli na jamii haitakuelewa kama utaachia kusimamia yale mema ambayo Mwendazake Magufuli aliyasimamia.Usije kushawishika kudharau kukamilisha baadhi ya miradi ambayo ina tija ambayo iko katika hatua za utekelezaji kwani utajishushi heshima yako wewe na utakuwa umeitukana kumbukumbu ya mtangulizi wako JPM ambaye kifo chake kimekupa nafasi ya kuwa rais wa nchi.

Hata hivyo usiogope kuonesha tofauti hasa katika maeneo ambayo kwa hakika Mtangulizi wako hakuwa sahihi.Ndio hakuwa mkamilifu.Kuna baadhi ya mambo mengi sana yanahitaji kurekebishwa na usiogope kuwa tofauti kwani wewe unayo haki ya kuweka tone ya uongozi wako.

Naendelea kukusisitiza kwamba kwa sasa litazame Baraza la Mawaziri, kuna watu hawatakiwa kabisa kuwa humo,watakuvuruga.Kumbuka moja kati ya heshima kubwa uliyo nayo ni kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mpya.Nafasi hio inakupa jukumu moja kubwa nalo ni kuukamilisha mchakato ule na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikiwa.

Mama Samia, Wewe ni Mzanzibari, tena Mzanzibari kweli kweli Usisahau hilo.Fanya Jambo kuhusu Zanzibar

Sitaki kusema zaidi ila kama nikajaliwa nitaongeza mengine ila kwa sasa nikutakie kila la heri katika kazi yako ya kuendesha nchi yetu

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Mh. Samia H. Suluhu

Rais wa JMT
 

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
1,904
2,000
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3. Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4. Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5. Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7. Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8. Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,329
2,000
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:
1.Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2.Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa...
Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye!

Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu!

Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom