Hercule Poirot
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 1,717
- 1,472
Hisani, haki na wajibu.Hakuna kitu kama chuki dhidi ya Rais SSH eti kwa kuwa Mbowe kakamatwa. Kama ujinga wanaofanya CHADEMA ungeachwa uendelee ningesema Taasisi ya Rais ni dhaifu. Mama ana siku takriban 120 tangu amehukua uongizi wa nchi.
Nchi imepita kwenye kipindi kigumu sana cha miaka 5 chini ya Mwendazake. Ila tumeyaona ambayo Rais SSH ametenda wala sina haja ya kuyaorodhesha hapa. Lakini Mbowe na Lissu wa CHADEMA wanataka vipaumbele vyao ndivyo mama afuate na siyo vipaumbele vya Serikali yake ya CCM.
Rais kasema Katiba isubiri nipange uchumi kwanza, CHADEMA hawwtaki. Pumbavu zao!!
Sasa akiwasikiliza wao ni nani atakuwa ndiye Rais wa Tanzania?
Hawa CHADEMA mtangulizi wa SSH alikuwa amewaacha wanahangaika na makesi Mahakamani, huyu amesema haki itendeke. Na kweli tunaona akina Mdude wanatoka na na RUFAA ya akina Mbowe inakubalika. Yote haya hamridhiki??
Mbowe anaweza akawa anawatumia wanachama wake ili arudishe nguvu zake kiuchumi kwa kumuonyesha Rais SSH kuwa Chama chake ndiyo kina nguvu sana za upinzani, hivyo Rais awe anamuogopa. Kumbuka alipoteza Bilicanas na Shamba la maua. Vijana wa CHADEMA tafuteni fedha kwenye ujasiriamali achaneni na Mbowe