Maoni: Dira ya Taifa ya maendeleo itakayo fungamanishwa na falsafa za 4R za Rais Samia na katiba mpya, ni matokeo makubwa kesho

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
"The best is yet to come"(Obama ,2012) ni maneno yaliyotolewa na Rais Obama katika hotuba yake siku aliyotangazwa mshindi kuongoza Taifa hilo kubwa kabisa duniani kijeshi na kiuchumi kwa kipindi Cha pili mwaka 2012. Ilikuwa ni hotuba ya matumaini makubwa kwa Marekani na Wamarekani. Kwa tafsiri isiyo rasmi maneno hayo tunaweza kuyatafsiri " mazuri bado yanakuja".

Katika kipindi cha Rais Kikwete kulikuwa na sera ya BRN ( Big Results Now) ambayo kwa tafsiri ni Matokeo Makubwa Kesho. Mafanikio ya mpango wa BRN kwa kifupi yalikuwa:
i. Usambazaji wa maji salama vijijini.
ii. Ulinzi wa Chakula
iii. Kuimarisha usafirishaji wa Bandari, Reli na Barabara
iv. Kuziwezesha kifedha miradi
v. Uboreshaji wa elimu ya msingi na sekondari.

BRN ilikuwa ni sehemu na nyenzo muhimu katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025 ambayo ilikuwa na lengo la kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 kulingana na mikakati na mipango iliyokuwa nayo. Mwaka 2020, tukafanikiwa kuingia uchumi wa kati wa chini lakini licha ya yote mkakati wa matokeo makubwa Sasa ilikosa meno, waziri mkuu mstaafu Lowassa alitanabaisha hayo alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa 2014/2015, novemba, 2013.

Sasa Taifa linakwenda kuandaa dira mpya mpya ya maendeleo ya 2050. Na hapa ninaona mikakati ya maandalizi na utekelezaji ya dira mpya itakavyoleta mwanga wa matumaini katika MATOKEO MAKUBWA KESHO (BEST RESULTS TOMORROW, BRT)

Kwanza, katika mchango wake Lowassa alisema kitengo Cha Utekelezaji, ufuatiliaji na Tathmini ya miradi (PDB) kilichokuwa chini ya Ofisi ya Rais kilikosa meno ya kufanikisha mipango ya BRN. Changamoto hii imetatuliwa na Rais Samia ambaye atakuwa na jukumu la kuandaa dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050 (2025-2050). Kwanza Ameunda wizara ya mipango na uwekezaji na kuunda tume ya Taifa ya mipango ambacho kitakuwa ni chombo rasmi na chenye meno katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.

Pili, Rais Samia amekuja na falsafa zake katika uongozi ambazo ni Reconciliation (maridhiano), Resilience ( Uvumilivu), Reforms ( maboresho) na Rebuilding ( Kujenga upya) kwa kifupi ni 4R au RRRR. Falsafa hizi ni nyenzo muhimu katika uandaaji na utekelezaji wa dira ya Taifa ya maendeleo. Kwa mfano, kupitia falsafa ya Maboresho( Reforms) hapo tunaona maboresho haya yatakuwa na msaada mkubwa kwenye dira hiyo.

Tatu, nia na dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia kutupatia katiba mpya. katiba ni nyenzo katika uandaaji wa dira ya maendeleo Kwa sababu katiba itaendelea kuwepo hata baada ya dira kutekelezwa. Kupitia nyenzo hii itasaidia wapanga mikakati kuja na dira itakayofungamanishwa na katiba na matakwa ya katiba tarajiwa.

Ushauri wangu:
Kabla ya kuanza mpango wa kuandaa dira ya Taifa ya maendeleo tuangalie kwanza upatikanaji wa katiba ili dira hiyo iandaliwe katika mazingira ya katiba mpya.

Hitimisho :
Kwa kuwa dira ya Taifa ya maendeleo itakuwa imebebwa na nyenzo muhimu, ni ishara kuwa itakuwa ni dira bora zaidi kuwahi kutengenezwa katika Taifa hili. Tutumie nyenzo ya falsafa za Rais Samia za 4R na katiba mpya kupata dira mpya ya maendeleo na huu ndio mchango wangu.

Bado naamini mazuri mengi yanakuja chini ya uongozi wa Rais Samia, tukae tuyasikilizie kama Wamarekani walivyoyasikilizia mazuri kutoka Kwa Rais Obama.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom