Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KAZI NZURI YA RAIS DKT SAMIA INAHITAJI KATIBA MPYA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kumekuwa na mjadala wa Katiba mpya ambao umekuwa ukiibuka na kufifia. Mjadala umekuwa unaibuka na kufifia kwa kuwa una sura mbili. Sura ya kwanza wanahitaji katiba mpya na sura ya pili hawahitaji katiba mpya.

Nilishawahi kuandika sababu nyingi ambazo katiba mpya inahitajika kabla Mama wa Taifa hajakamilisha kipindi Cha Uongozi wake mwaka 2030 kama Mungu atampa nafasi na uhai.

Wapo wanaCCM wenzangu ambao ukisema tunahitaji katiba mpya wanakuona kama msaliti. Hawa Mimi wakati mwingine ninawapuuza kwa kuwa wanadhani CCM tutatawala miaka yote. Lakini wale wanaCCM ambao wanafanana na Mimi kuwaza wanajuwa kwa katiba hii Siku CCM tukiwa Wapinzani itatunyanyasa sana hasa Chama kitakachoshika Serikali kikiamua kuifuata katiba hii walau kwa 60% tu. Tutaona ni kama ni Serikali ya Kidikteta. Ma Rais waliotokana na CCM wamejitahidi kuwa waungwana na kutumia zaidi hekima kuongoza kuliko katiba.

Kwa nini ninasema kazi nzuri ya Mama wa Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahitaji katiba mpya?

Tunahitaji katiba mpya ambayo itatafsiri namna ya kulinda na kuendeleza kazi za Mtangulizi wako. Tunahitaji katiba ambayo maendeleo ya nchi yatakuwa jumuishi siyo maono ya mtu mmoja ambaye ni Rais. Tunahitaji katiba itakayozalisha great Thinkers siyo Wanafiki wa kusifia mchana na usiku kutukana.

Leo Rais Samia amefanya kazi kubwa ambazo kwa takwimu tu hakuna aliyewahi kufanya. Sasa tunajiuliza atakayekuja 2030 ataendeleza haya au ataanza na ya kwake?

Katiba hii tuliyonayo ndiyo iliweka Taifa lockup ya siasa kwa miaka zaidi ya mitano na ni katiba hii hii ambayo imetuondoa Kwenye lock up. Hapa hayati JPM alitumia utashi wake na maono yake kutuweka lock up na Mhe DKt. Samia ametumia utashi na maono yake kutuondoa lockup. Ili kuondokana na utashi na maono tupate katiba ambayo ndiyo italeta mwongozo badala ya utashi na maono.

Mwaka 2030 tunahitaji kupata Rais ambaye atakanyagia Kwenye gia namba tano ambayo Mama amekanyaga, hatuhitaji tena Rais atakayetuanzishia gia number Moja kuturusha nyuma.

Ili tupate Rais wa kulinda haya, zawadi pekee na kubwa ambayo Mama wa Taifa hatasahaulika ni kutupatia mrithi ambaye ataenda na gia yake. Ili mrithi apatikane wa kwenda na gia yake lazima Mama atuachie katiba ambayo Rais atakayekuja itamlazimu kwenda na Yale atakayoyakuta.

Leo tungempa Rais ambaye hayupo kama Mama Samia angeweza kuachana na miradi yote aliyoianzisha Hayati John Pombe Magufuli akamua kuanza na yake, lakini kwa kuwa Mama Uongozi upo moyoni aliamua kubeba maono ya Mtangulizi wake akaongeza na mengine ya kwake. Ni watu na ni Viongozi wachache aina ya DKt . Samia na hawa hupatikanika mara chache.

Ninamuomba Mama dhamira yake ya kuanzisha mchakato wa Katiba mpya aendelee nayo ili atakapokuwa anahitimisha Uongozi wake 2030 ahitimishe kwa kutuachia zawadi hii.

Tunahitaji katiba ambayo hata ikitokea huko mbele CCM tukawa Wapinzani tukawe na amani, hatutaki katiba ambayo itatufanya kuishi kama tupo ugenini.

Rais amefungua milango ya Demokrasia Kwenye mawanda mapana sana. Wakati Wanasiasa hasa Viongozi wakitumia njia zao za Uongozi kushawishi mchakato uendelee kama Mama alivyosema, huku wengine wakisema Mama aachane na Zoezi hili, na sisi ambao hatuna nafasi za kusema majukwani tunatumia maarifa aliyotupa Mungu kuongea na Rais kwa njia hii ya kuandika.

Katiba ni mhimu. Tunahitaji katiba ambayo itasaidia kuziongezea ulinzi tunu za Taifa. Katiba ambayo haitarusu Siku tupate Rais ambaye ataamua kuibomoa misingi yote waliiyoiacha waasisi wa Taifa hili.
 
Back
Top Bottom