Katiba Mpya ndio legacy pekee ya Rais Samia, Watangulizi wako walishindwa

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,033
Wadau nawasalimu.

Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri hayati Samweli Sitta alikuwa mwenyekiti wa bunge la katiba na Rais Samia alikuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la Katiba.

Binafsi baada ya Rais Samia kuwa Rais ninaamini Rais Samia kwa kuwa anaujua vizuri sana mchakato ule wa bunge la katiba ulipoishia hivyo ingekuwa rahisi sana kwake kuukamilisha mchakato ule na kuwapatia Watanzania Katiba mpya wanayoihitaji Watanzania mil. 62 kwani dosari zilizosababisha mkwamo wa ule mchakato Rais Samia anaujua na ni rahisi kwake kuzirekebisha dosari zote.

Nimesikitika sana kuona Rais Samia ameamua kuurudisha nyuma zaidi ule mchakato badala ya kuuharakisha kwani katiba iliyopo imekuwa ya miaka mingi na mabadiliko mengi yametokea yanayohitaji katiba ibadilishwe kulingana na hali ya maisha kiuchumi kijamii ilivyo. Rais Samia nakuomba ukumbuke mabilioni ya fedha za kodi zilizotumika wakati wa bunge la katiba na katiba haikupatikana.

Kwa kuwa Rais Samia unatakiwa kutuachia legacy yako kitu pekee kitakachokufanya watanzania wakukumbuke milele sio kujenga zahanati vyumba vya madarasa bali ni katiba mpya kwani watangulizi wako tukianzia Rais Kikwete aliyeuanzisha mchakato alishindwa kuukamilisha.

Hayati Rais Magufuli yeye hakutaka kabisa kuushughulikia kwa vigezo viwili;

1. Hana bajeti

2. Sio kipaumbele cha serikali yake.

Mh. Rais samia hebu wapatie katiba mpya wa tanzania.
 
Back
Top Bottom