Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
Kwa huu upeo wako wa kufikiri, hukutakiwa kabisa kuchangia chochote kwenye huu mjadala. Ulitakiwa usome tu na kwenda zako kujitafutia huo mkate wako wa kila siku!

Ila kwa bahati mbaya umeamua kujidhalilisha.
 
Yaani nyie chadema mnajidanganya kuwa hicho mnachokitaka nyinyi ni hitaji la kila mtu mko wachache sana mnaolazimisha hiyo katiba yaani kama vile hamjui kama kuitengeneza inatumika hela acheni upiumbavu wenu mpeni muda atengeneze uchumi hayo ya tamaa zenu za madaraka yatafuata baadae hata mkipewa hiyo katiba mpya mnayoitaka hamuwezi kushinda hata siku moja hamna sera nzuri
 
Habari wakuu? Ni mambo ya ajabu sana kusikia kila siku, kujenga nchi, kutengeneza ajira, mm najiuliza, Mpaka lini? Hivyi kweli ni kwa sababu Watanzania ni wapole ndo maana tunaambiwa mambo yaleyale, toka wakati wa jpm ni maneno hayohayo, jamani itafika wakati watanzania uvumilivu utawashinda, nchi hii uchumi umeyumba na hata ajira kwa sababu ya katiba hii, sasa kama hamna katiba mpya huo uchumi utapandaje? Tunahitaji katiba mpya
 
Utakuza vipi uchumi bila demokrasia?Wawekezaji na Demokrasia ni sawa na mtoto na mbeleko! Ikikatika mbeleko, mtoto huanguka!

Ukiminya Demokrasia, wawekezaji hukimbia! Huwezi kumnyima pumzi mama mjamzito ukategemea kuwa mtoto aliye tumboni ataendelea kuishi! Miujiza ya aina hiyo bado haijatendeka katika uso wa dunia.Demokrasia ndiyo pumzi ya wawekezaji.Hakuna demokrasia ni hakuna uwekezaji na ni hakuna ukuaji wa uchumi pia.

Mama ni inept leader anaelinda maslahi yake ya kujinufaisha kisiasa na kadhalika kwa kuitawala Tanzania kidikteta kama alivyofanya Magufuli ndiyo maana hajali yote haya.
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Watu mnakuwa wagumu kuelewa sijui mnawazaje, ipo hivii katiba iliyopo ni mbovu mkuu

Labda nikupe mfano kidogo tu, kipindi cha JPM wakulima walikata tamaa kabisa
Kulima ulilima wewe ila Rais kwa kulinda maslahi yake kisiasa anaamua kuzuia mazao yasiende nje ilihali anajua kabisa soko la ndani halitoshi matokeo mazao yakawa mengi bei ikashuka

Yapo mengi mifumo ya elimu, afya, nishati, biashara nk. maisha yetu ya kila siku ni siasa, siasa ndo inaamua uishije au wewe unawazaje ukiitenga siasa umejitenga na maisha ya kawaida

Wawekezaji wakimataifa wanaojielewa lkn, huwa hawaendi kuwekeza kwenye taifa lolote bila kuchunguza mfumo wao wa kiutawala (siasa inaingia hapa) wanaiangalia sana siasa japo huwa hawaendi kufanya siasa

Katiba mpya na bora ni mhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu
 
Yaani nyie chadema mnajidanganya kuwa hicho mnachokitaka nyinyi ni hitaji la kila mtu mko wachache sana mnaolazimisha hiyo katiba yaani kama vile hamjui kama kuitengeneza inatumika hela acheni upiumbavu wenu mpeni muda atengeneze uchumi hayo ya tamaa zenu za madaraka yatafuata baadae hata mkipewa hiyo katiba mpya mnayoitaka hamuwezi kushinda hata siku moja hamna sera nzuri
Sio chadema wanataka katiba mpya hata mm mwanccm nataka katiba mpya,
 
Hapa Uko Sahihi 100%, Mfano ni Uongozi wa Awamu ya Tano, nchi iliendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja. Alilokuwa wanalisema ndio ilikuwa sheria na kila mtu alikubaliona nao apende asipende...Katiba mpya ndio jibu la mambo ya namna ile...
Kwani shida kubwa ni katiba mpya au viongozi kufuata katiba? Kwa sababu hata hii katiba tunayoilalamikia ina mambo mengi mazuri tu lakini viongozi wetu mengine hawayafuati.

Kwa hiyo hata kama tungekuwa na katiba nzuri kiasi gani lakini ikiwa haifuatwi ni kazi bure pia tujue kuwa hata hiyo mpya tunayoitaka leo baada ya muda mchache tutaiona ina mapungufu
 
Habari wakuu?? Ni mambo ya ajabu sana kusikia kila siku, kujenga nchi, kutengeneza ajira, mm najiuliza, Mpaka lini???? Hivyi kweli ni kwa sababu watanzania ni wapole ndo maana tunaambiwa mambo yaleyale, toka wakati wa jpm ni maneno hayohayo , jamani itafika wakati watanzania uvumilivu utawashinda, nchi hii uchumi umeyumba na hata ajira kwa sababu ya katiba hii, sasa kama hamna katiba mpya huo uchumi utapandaje???? Tunahitaji katiba mpya
Nani alikwambia katiba mpya ndio inapandisha uchumi?
 
Samia anacheza vizuri huu mziki, leo anapiga rungu inakua zogo, kesho anatupoza na lingine tunashangilia, kesho kutwa rungu tunaanza yalaaaaaa next anatupoza tena tunashangilia...
Hiyo ya kupoza hapa na pale ni jambo zuri lakini ni short term. Kwa mfano akishamaliza kuondoa Mabaya ya Magufuli then yeye ana nini cha kuoffer?. Ni lazima asimame sasa ajipambanue kwa ujasiri kuonyesha anajua Taifa linahitaji nini. Asiangalie utswala wake wa miaka mitano au Tisa anayoweza kukaa nadarakani. Aangalie miaka 50 au 100 ijayo.

Kujenga uchumi ni process endelevu, hakuna siku ktk dunia hii nchi yoyote ikasema eti imemaliza kazi ya kujenga uchumi. Kwa hiyo hoja ya Samia ni kujaribu kupotezea suala la katiba mpya, lakini hii haitokwenda vizuri kwake kiuongozi na kwa imani ya wananchi kwake.

Samia ajue tu kuwa ni mchakato wa katiba mpya uliomuibua akajulikana na ni mchakato huohuo utakaomuangusha asiposoma alama za nyakati
 
Kwa hiyo Nchi hii aina demokrasia Mama anaongoza kidikteta?
Unaelewa kuwa mikutano ya kisiasa siyo tu kwamba ni haki yetu ya kikatiba bali ni universal declaration of human rights?
109_20210628_200150.jpg
 
Unaelewa kuwa mikutano ya kisiasa siyo tu kwamba ni haki yetu ya kikatiba bali ni universal declaration of human rights?View attachment 1834320
Ndio maana hapo juu nilisema tatizo kubwa ni viongozi kufuata yaliyomo kwenye katiba unaweza kuwa na katiba nzuuuri ila kama haifuatwi ni kazi bure

Ila pia tukumbuke hakuna uhuru usio kuwa na mipaka tumeshuhudi kipindi cha nyuma wanasiasa wetu walipokuwa huru kidogo matusi,kejeli,maandamano yasio na kichwa wala miguu kila uchwao ila kwa sasa Nchi imetulia kidogo

Mikutano haijakatazwa ila kila mtu afanye kwenye jimbo lake shida ni kwa wale wasio na majimbo inabidi wafanye mikutano ya ndani hiyo imeruhusiwa
 
Ndio maana hapo juu nilisema tatizo kubwa ni viongozi kufuata yaliyomo kwenye katiba unaweza kuwa na katiba nzuuuri ila kama haifuatwi ni kazi bure
Kuwa na katiba bora hata kama haifuatwi kwa wakati huo ni one step ahead kwa sababu ukishakuwa na katiba bora kinachofuata ni mikakati ya kupigania katiba hiyo ifuatwe.Vita ya kupigania demokrasia siyo vita ya siku moja bali ni vita ya kudumu na kija jambo litakuwa archieved kwa muda wake.
Ila pia tukumbuke hakuna uhuru usio kuwa na mipaka tumeshuhudi kipindi cha nyuma wanasiasa wetu walipokuwa huru kidogo matusi,kejeli,maandamano yasio na kichwa wala miguu kila uchwao ila kwa sasa Nchi imetulia kidogo
Kwani nani amekuwa na uhuru ambao upo kinyume na katiba?Hata kama kuna mtu amekuwa na uhuru ambao upo kinyume na katiba mahakama si zipo!Si apelekwe mahakamani?Rais au wewe mnapotaka kututafsiria maana ya uhuru na mipaka yake ni mmekuwa mahakama?Kama kuna mtu ana practise uhuru ambao hauna mipaka si apelekwe mahakamani?
Mikutano haijakatazwa ila kila mtu afanye kwenye jimbo lake shida ni kwa wale wasio na majimbo inabidi wafanye mikutano ya ndani hiyo imeruhusiwa
Mikutano ya kisiasa ifanyike ya ndani kwa mujibu wa sheria ipi?Katiba tuliyonayo inaruhusu mikutano ya nje,sasa wewe na Rais mnataka ifanyike mikutano ya ndani kwa mujibu wa katiba ipi?Yaani mnalazimisha tuvunje katiba?
 
Chadema/Upinzani bora mfanye mchakato wa katiba mpya 2025/2030 kwas sasa hilo bunge la CCM litasimamia huo mchakato na katiba tutakayoipata itakuwa ni kiccm CCM tu mtapigwa tena, subirini mrudi bungeni kwanza.
 
Back
Top Bottom