Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira – Arusha leo tarehe 21 Agosti, 2023.


6552f6d9-9b22-4c33-b12c-c829c8674543.jpg

153f5a00-c5eb-4500-83a7-30613f209567.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Maaskofu na Viongozi mbalimbali wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wakati alipowasili katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo tarehe 21 Agosti, 2023.

DKT. FREDRICK SHOO - ASKOFU MKUU WA KKKT

- Hatupingi uwekezaji
Viongozi wa Dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona (Rais Samia) mwanzoni mwa jambo hili, kwa ungwana ukatupokea na tukakukabidhi maoni yetu na ukaahidi utayawasilisha kwa wataalam kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

lipo hili la DP World Mheshimiwa…kwanza naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe

Ninatambua kuwa ulipokea kijiti katika mazingira magumu sana, lakini pia pamoja na mazingira yale wewe ukaanza historia mpya ya nchi yetu ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais, kuna wengi hawakuamini, hawakutaki na mpaka leo wamebaki na jinamizi la namna hii, huu ulikuwa ni mpango wa Mungu

- Hatutaacha kushauri, kukemea
Kama tukiona kuna sehemu hakupo sawa hatutaacha kuwaona, kuwashauri, kukemea na ikifika hatua hiyo tusiambiwe kuwa tunachanganya Dini na Siasa

- Mungu amekujalia Hekima

Najua katika jambo hilo linaelekea mahali tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi, nashukuru Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi, umekaa kimya

- Tusiwagawe watu kwa utofauti wa Dini
Mimi nilikerwa juzi niliposikia baada ya mtu mmoja ..akisema kwanini Serikali inatumia pesa zake kusaidia au kuendesha taasisi za wakristo, ...watu wamesahau historia, kwenye miaka ile ya 90 kuelekea 2000 ..Kanisa la Kilutheri Tanzania kwa kushirikiana na marafiki zake wa nje na ndani ya nchi, tuliongoza kampeni kubwa ya Tanzania kufutiwa madeni na nchi za G7...na Tanzania ikafutiwa madeni...Tuheshimu jambo hilo. Kwahiyo naomba sana mtu asibeze au kudhihaki ushirikiano huu kwa sababu yoyote ile.

Umoja wa Taifa letu la Tanzania, mshikamano ni muhimu kuliko Mtu au kundi lolote, niwaombe Viongozi wenzangu wa Dini zote, niwaombe Wanasiasa, kuacha kabisa kujaribu kuwagawa Watu kwa misingi ya Dini au kwa misingi ya itikadi iwayo yoyote ya kisiasa na kwa misingi ya maslahi binafsi

Niombe Serikali yako kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kutugawa kwa utofauti wa Dini zetu, hata pale Mtu anaposema jambo la kuipendeza Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi wa kutugawa kidini au kwasababu nyingine yoyote huyo akemewe, tumkatae hana nia njema

871d486b-64a2-4fd3-86c5-b10226c3d0ec.jpg

dc1de800-92d1-4cf8-be49-76ada8376cd5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali za Kanisa alipotembelea Maonesho Maalum kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

- Uharibifu wa mazingira

Katika nchi kama yetu ambayo asilimia kubwa tunategemea kilimo, madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa zaidi, binafsi nafarijika kuona viongozi wa dini wanalipigia kelele jambo hili, ningetamani kuona kila taasisi ya dini inajiwekea mkakati mahususi wa kupambana na uharibifu wa mazingira.

- Hakuna mwenye msuli wa kuharibu amani yetu
Ndugu zangu, na hususani Baba Askofu Shoo, Kaka yangu Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa Taifa letu, niliamua kunyazama kimya na naendelea kunyama kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza Taifa hili

Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa hili, hayo itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu, asanteni sana

c1e5952d-7bd0-4260-98f6-654f1c30e807.jpg

ec7b6652-e80a-4ad2-a011-c3b60feb575c.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki kuimba kwaya na Watoto wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
🤣🤣🤣kaenda na kiti chake kanisani
Afu wanasema tutenganishe kanisa na siasa🤣🤣🤣
Waraka wa amani🤣🤣🤣
 
…hawa ndio Wakristo pekee Tanzania 🇹🇿! Hao wengine ni genge la wahuni waliosababisha vita na migogoro yote Duniani!

👉🏾 Vita kuu ya kwanza na ya pili ya Dunia, chanzo ni wao!

👉🏾 Mauaji ya kimbari Rwanda, Namibia, chanzo ni wao!

👉🏾 Vita inayoendelea Congo, CAR, na sehemu nyengine Duniani, chanzo ni hao hao wanaojiita «Waroma» wakati hawana uraia wa Italy! 😁🚮🚮🚮

👉
 
…hawa ndio Wakristo pekee Tanzania 🇹🇿! Hao wengine ni genge la wahuni waliosababisha vita na migogoro yote Duniani!

👉🏾 Vita kuu ya kwanza na ya pili ya Dunia, chanzo ni wao!

👉🏾 Mauaji ya kimbari Rwanda, Namibia, chanzo ni wao!

👉🏾 Vita inayoendelea Congo, CAR, na sehemu nyengine Duniani, chanzo ni hao hao wanaojiita «Waroma» wakati hawana uraia wa Italy! 😁🚮🚮🚮

👉

Kuna nduguyo mwingine hapa, umesahau kumsifia:

 
…hawa ndio Wakristo pekee Tanzania 🇹🇿! Hao wengine ni genge la wahuni waliosababisha vita na migogoro yote Duniani!

👉🏾 Vita kuu ya kwanza na ya pili ya Dunia, chanzo ni wao!

👉🏾 Mauaji ya kimbari Rwanda, Namibia, chanzo ni wao!

👉🏾 Vita inayoendelea Congo, CAR, na sehemu nyengine Duniani, chanzo ni hao hao wanaojiita «Waroma» wakati hawana uraia wa Italy! 😁🚮🚮🚮

👉
 

Attachments

  • FB_IMG_1692612034018.jpg
    FB_IMG_1692612034018.jpg
    46 KB · Views: 1
Back
Top Bottom