Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Mkuu hoja yangu Ni kuwa kwa kuwa sisi Ni corona free tofauti na wenzetu, bado tunahitaji tahadhari kuruhusu mwingiliano, toka kwa nchi ziliathirika,

Ni hatari kushangilia utalii alafu ukakarbisha. Maradhi nchini mwako, kisa unataka kuwaaminisha watu uongo ili wakupe kura, baadaye ita
Mkuu wewe na mimi tuanaujua ukweli kuhusu corona, tuachie hapo mkuu.
Kwa hivyo kama ndiyo vile basi maisha lazima yaendelee kwenye sekta za kiuchumi.
 
Kumbe Nini?
Petty issue_Maendeleo is increased productivity ya watu, universal and improved health systems,Quality and inclusive education system and not petty issue like taa za barabarani au kununua ndege kwa keshi
 
Lisu kawashauri muwe mnakaa kwa distance na mvae barakoa msifanya ujinga kama ule wa kwenye mkutano mkuu na ile siku ya kumpokea!

Pia yeye mwenyewe mwambieni aache upumabvu! Asiwe anatangaza kuna corona wakati anapuyanga kwenye makundi ya watu bila barakoa
Kwahiyo wewe unakaa unafuata anayokueleza Magufuli kuhusu Corona? Utakuwa mwenda wazimu kuamini hivyo!
 
Yaani kweli media za ndani zimeamua kusaliti upinzani kweli kabisa kweli haya bwana siku hazigandi.
Hata mim ningekua nna milik kituo..marufuku kushabikia chama ambacho sio tawala

Yaan watoto wangu na mkewangu walale njaa kisa wananchi...am soo fucki.n selfish
 
Ni mpumbavu pekee anaweza kusema USA wameendelea wana taa hadi barabarani ila ziliwa tz siyo maendeleo.
Kama wewe si mwanaccm, huwezi ukasema U.S. wameendelea kwa kuwa wanataa za barabarani au wana fly overs.Hizi ni petty issues kwenye Ile kitu inaitwa maendeleo
 
Sasa Kama haipo tunajihadhari nayo kwa kipi? Hata hivyo issue yangu haikuwa corona bali mtu anajejifanya kwamba bila yeye hakuna Tanzania
Baadhi ya watu waliobahatika/wanao bahatika kuwa nyuma ya mikamera wanadhani wanaakili kuliko watanania wote mimi huwa napigwa na butwaa tu!
 
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)

Lisu dishi limeyumba
Yeye barakoa havai, social distance haweki
Juzi na Jana ameshiriki vikao na mikutano, mbona hajafanta hayo?
Au anaongelea Corona ya Ubelgiji siyo Tanzania!
Kuna ndugu yake hata mmoja amekufa kwa Corona?
Kweli bado nawashangaa wanaomshabikia huyu mzimu
 
Lisu dishi limeyumba
Yeye barakoa havai, social distance haweki
Juzi na Jana ameshiriki vikao na mikutano, mbona hajafanta hayo?
Au anaongelea Corona ya Ubelgiji siyo Tanzania!
Kuna ndugu yake hata mmoja amekufa kwa Corona?
Kweli bado nawashangaa wanaomshabikia huyu mzimu
Hivi ni wakati gani mtu anapaswa kuvaa barakoa? Naona watu mnakaririshwa tu ujinga na ninyi mnaubeba Kama ulivyo
 
Unafiki gani huu bana wa kuzungumzia Corona huko? Yeye amefuata social distancing tangu afike?

Mimi siupendi utawala huu lakini the approach on Coronavirus was spot on.
 
Hahaaa kumbe na yeye anasikia??
Tundu lissu nenda Amana,nenda temeke,nenda mloganzila ukikuta wagonjwa wa corona huko hata Mimi nitakupa kura,wewe Ni mwanasheria hakuna Mambo ya kusikia mahakamani
Lissu akizingatia social distance
image-200.jpeg
images%20(9).jpeg
images%20(8).jpeg
images%20(7).jpeg
 
Lissu akiendekeza siasa za corona hatapata kura za wabongo,hasa huku uswahilini...huku raia wanavyomkubali jiwe hasa katika maamuzi yake juu ya corona ...

Halafu mi wanachoniuzi wapinzani ni kushobokea sana wakenya,wakenya kudadeki zao wametufanyia unyambilisi toka zamani sana,wanatubeza kudadeki zao..lissu angalia mienendo yako utakosa kura...
 
Hoja za Lissu ni kuhakikisha Wapiga dili wanakwamisha Mipango yetu ambayo mpaka saizi wamekwama.

Mfano Mtu unajikweza kwa Wakenya waliorubuni ndege za EAC ambazo ni za Watz na wana EAC si lazima unatambulika kwamba upapeti wako ni wa namna vipi 😀😀😀😀😀😀

Kama vyombo vya hapa nchini kila akiongea wanatoa sauti unategemea aache kutumia plan b?
 
Huyu jamaa shoga kweli, asa kama kuna corona na inaua mbona toka aje hajaonekana kavaa barakoa wala kufanya self isolation!
 
Back
Top Bottom