Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
999
2,000
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za Siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Lissu: Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom