Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,526
- 121,366
Wanabodi
Msingi Mkuu wa kazi ya uandishi wa habari ni ukweli, kuwa mkweli kuusema ukweli na kuandika ukweli!.
Sisi waandishi wa habari wa zamani tulifundishwa na waalimu wazungu, mimi mpaka leo mpaka kesho nakumbuka kauli ya Mwalimu wangu mzungu pale TSJ, a Canadian, Patrick Walsh akitufundisha kuwa kazi uandishi wa habari, "journalism is to tell nothing but the truth"
Hivyo mimi kama mwandishi wa habari, I have been telling the truth, writing the truth, until nilipogundua ukiwa mkweli mno , haswa kwa kuusema ukweli mchungu ambao watu hawapendi kusikia, utachukiwa and sometimes ni hatari hata kwako na kwa maisha yako.
Tumeyashuhudia kwa waandishi wakweli kama kuna Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Erick Kabendera, and the like!. Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
Uandishi wa habari ni sawa na kazi ya siasa, siasa za ukweli wa kuleta maendeleo ya kweli ni siasa za kweli na wanasiasa wanaosema ukweli ndio wanasiasa wa ukweli wa kuleta maendeleo ya kweli. JPM alikuwa ni mmoja wao, Tundu Lissu pia yumo!.
Kuna wengi wanadhani kazi ya siasa na wanasiasa ni kazi ya kupiga bla bla, kuwadanganya wananchi kwa ahadi hewa kam kem zisizotekelezeka!.
Hivyo ndivyo walivyo wengi wa wanasiasa wetu wakiwemo baadhi ya viongozi wetu hadi wakuu, sio wakweli daima, ni watu wa blah blah nyingi!.
Ukimuondoa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ni mkweli daima, Rais Mwnyi yeye alikuwa ni mkimya sio mtu wa blah blah. Mkapa pia alikuwa mkweli, JK naomba nisimzungumzie ila JPM alikuwa ni mtu mkweli mwenye ukweli sometimes kupitiliza hivyo kumfanya achukiwe!.
Ni ukweli wa JPM ndio uliomfanya aweze kuyatenda yale aliyoyatenda. Kuna wakweli wa type fulani ambao wao ni "hapa kazi tuu", wakitaka jambo lao liwe na lifanyike kwa haraka, kama katiba, sheria, taratibu na kanuni, ni vikwazo, then wataziweka pembeni na kulifanya jambo lao, na ndio maana JPM alikanyaga katiba ili mambo yaende na kiukweli yalikwenda!. Watu tulinyooka!, nchi ilinyooka, mafisadi, wazembe, walarushwa walinyooka na vyama vilikaza kweli kweli!. Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli Wake, Hata Kama Uko Kinyume cha Katiba, Sera na Ilani?.
Mimi nimesoma sekondari Ilboru na Tundu Lissu, huyu jamaa Tundu Lissu ni mkweli na yuko bold tangu shuleni!. Kuna vitu vitatu Tundu Lissu anafanana sana na Magufuli, kimoja ni kwenye kuusema ukweli, Tundu Lissu ni mkweli kama JPM!, kwenye kuusema ukweli Lissu atausema no matter what!. Kitu cha pili ambacho Tundu Lissu ni kama Magufuli, naomba nisikitaje hapa kwasababu niliisha kitaja hapa, tena hicho cha pili Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, hivyo hata ile 2020, mimi ni miongoni mwa tuliomchagiza Tundu Lissu agombee na Magufuli kwasababu Lissu ni zaidi ya Magufuli Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! ila kama mgombea wa CCM 2025, ni Mwanamke, simshauri Lissu kugombea!, maana kwa mwanamume jitu la miraba 4 kushindwa vibaya na mwanamke... itakuwa aibu!.
Kitu cha tatu ambacho Tundu Lissu ni kama Magufuli, ni udikiteta!. Matukio yote ya udikteta Chadema TAL is behind! Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA ni TAL alisimamia torture ya Kagenzi kwenye torture chamber pale Ufipa!.
Jana nimetazama mahojiano ya Tundu Lissu kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV na kumsikiliza kwa makini Tundu Lissu, nikafarijika sana kwa jinsi Tundu Lissu alivyokuwa mkweli.
Mimi kama mwandishi mkweli kazi yangu ni kuuliza, hivyo hili ni bandiko la kuuliza, kumbe Tundu Lissu yuko kama JPM, kwa mambo matatu, JPM ni mtu mkweli. Na Tundu Lissu ni mtu mkweli. Jana meusema ukweli wa jinsi kipengele cha ukomo wa uongozi kilivyoyeyuka toka ndani ya katiba ya Chadema!. Kumbe kipengele hicho haikuyeyuka, kiliyeyushwa kwa kunyofolewa, kimya kimya na ku vanish into thin air!.
Kipengele hicho, nimekuwa nakiulizia sana kwa muda mrefu toka kwa viongozi wa Chadema, kuhusu kipengele hicho cha ukomo wa uongozi ndani ya katiba ya Chadema, kilitowekaje?, kiliondolewa au kiliyeyuka tuu chenyewe?
Hoja ya kunyofolewa kwa kipengele hicho, niliibua hapa Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Angalia nilichojibiwa na Dr. Slaa
Jibu la Dr. Slaa linaonyesha, licha ya huyu kuwa ni mtendaji mkuu wa Chadema, alipaswa kuijua katiba ya Chadema kinyume nyume!, lakini Dr. Slaa kumbe haijui katiba ya Chadema wala hajui uwepo wa kipengele hicho hivyo yeye akasema hakijawahi kuwepo!.
Mtu wa pili kulijibia hili ni J.J Mnyika, yeye alijibu
Sasa jana ndio Tundu Lissu amefichua ukweli, kumbe kuna watu wakikijadili kipengele hicho kimya kimya bila Dr.Slaa na Mnyika kujua na kuamua kukinyofoa kimya kimya bila kuwasilishwa wala kujadiliwa!.
Kipengele chenyewe ni hiki
Kwa mujibu wa Tundu Lissu, sababu za kukiondoa ni changamoto ya kupata viongozi bora, kuwa kipindi cha miaka 10, hakitoshi kupika viongozi hivyo inapofika kipindi cha uchaguzi wa ndani, Chadema imekuwa ikipata changamoto ya kupata watu wa kujaza nafasi za viongozi waliotimiza umri wa miaka 10, hivyo wakaamua kukifuta kipengele hicho!.
Kiukweli kabisa kama chama hakina succession plan na hakuna grooming yoyote ya future leaders, na kipindi cha miaka 10 kinaonekana hakitoshi!, hii ni dalili ya incompetence ya aina fulani kwenye succession plan yao, na unaweza kukuta mpaka sasa ndani ya Chadema hakuna maandalizi yoyote ya succession plan ya Mwenyekiti wala hakuna grooming yoyote ya mtu yoyote wa kumpokea Mbowe uenyekiti!.
Lissu alipoulizwa kuhusu yeye kugombea urais 2025 alijibu kwanza katiba, alipobanwa sana akasema ndio atagombea!. That was a mistake!. Kwa vile Chadema bado hawajafanya kikao chochote cha kumteua mgombea wake wa urais wa 2025, hakuna ubaya wowote kwa mwana Chadema yeyote kuwa a wishful thinker kugombea urais 2025 lakini kutamka kwenye TV kuwa yes nitagombea wakati hakuna kikao chochote kilichomteua ni very dangerous!.
He who pays the piper, may call the tune!, whoever is paying the Chadema piper ndio may call the tune, nani agombee Chadema ili usimsumbue yule Malkia wetu, ikitokea sio Lissu, na huku Lissu ameisha tangaza kugombea, huko ndani kutakalika?.
Viongozi wasema ukweli wa type ya Lissu, ndio wanaolifaa taifa letu, na kwavile nilisema Lissu anafanana na Magufuli kwa mambo matatu, moja ni hili la ukweli, na hayo mawili yaliyobakia Lissu ni zaidi ya Magufuli, kama ikitokea Tundu Lissu akagombea tena urais na akachaguliwa kuwa rais wa JMT, then maendeleo ya Tanzania yatapaa maana Lissu ni zaidi ya Magufuli kwa hayo mengine mawili.
Hongera sana Tundu Lissu, jana umeongea vizuri kwenye ITV, hukutaja taja tena majina ya waliokushambulia.
Pia umesema dereva wao yuko Ubelgiji akihitajika kuhojiwa serikali inawaandikia serikali ya Belgium anarudishwa nchini kuhojiwa, kumbe Lissu hajui kuwa Tanzania hatuna mkataba wa extradition act na Belgium!.
Nimefurahi Lissu ameongea huku ametulia bila Jazba bila kutukana na au lugha ya maudhi.
Kilicho nifurahisha zaidi ni Tundu Lissu kuwa mkweli daima, keep on telling the truth and the truth will set you free!. Lissu akiendelea hivi, soon atakuwa like a real politician tena presidential material na sio mwanaharakati kama alivyo sasa!. Big up sana Bwana mdogo wangu wa Ilboru.
Paskali

WanaJF,
Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.
2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.
3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.
Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.
Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
Jibu la Dr. Slaa linaonyesha, licha ya huyu kuwa ni mtendaji mkuu wa Chadema, alipaswa kuijua katiba ya Chadema kinyume nyume!, lakini Dr. Slaa kumbe haijui katiba ya Chadema wala hajui uwepo wa kipengele hicho hivyo yeye akasema hakijawahi kuwepo!.
Mtu wa pili kulijibia hili ni J.J Mnyika, yeye alijibu
Jibu hili la Mnyika linaonyesha kipengele hicho hakikujadiliwa popote, hivyo kiliachwa kwa kuwa redundant.Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Kabla ya kusoma mjadala huu, niliitikia mwito wa Mtoi kwenye Jukwaa la Wanamabadiliko na nikaandika kwa kirefu kuhusu suala hili ambalo mimi nilishiriki kwa karibu sana nikiwa sehemu ya timu zote tatu zilizohusika na mchakato wa kukusanya maoni ya wanachama kwa ajili ya kuandika katiba, kanuni, itifaki na maadili ya chama pamoja na miongozo ya mabaraza ya chama. Naomba Mods muuweke waraka huo ambao nitawatumia kwa barua pepe au mnaweza kuuchukua kutoka huko. Nimekubaliana na katibu mkuu kuna marekebisho kwenye majibu yake ya awali, katiba ya mwaka 2004 iliondolewe katika orodha ya katiba alizozitaja. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu hayo. Baada ya majibu hayo kusomwa, kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi wa kichama kuhusu suala hili la katiba na mengine au maoni yangu binafsi nitafanya hivyo leo kati ya saa 9 mpaka 10 Jioni. Niko kwenye kikao, baada ya hapo nitakuwa kwenye mkutano. Nikihitajika baadae nitarejea tena. Mjadala mwema. JJ