Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,494
2,000
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc.

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo.

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc.

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali. Je, Corona ipo Tanzania? Je, serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana! Je, ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata.

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
 

Mwanga Mkali

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
475
1,000
We nunua tangawizi, mchaichai chemsha iive ukiipua mix limao na asali gonga nusu kikombe asubuhi na jioni na familia yako ongeza immunite kwa mbegu za tikiti pia zina zink ya kutosha.

Sometime warm you body by drinking hot water until you sweat.

Mengine iachie serikali itajua cha kufanya.
 

massaiboi

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
1,226
2,000
Watu mitaani wananong'ona kuwa hii kitu inang'ta kimya kimya.

Kuendelea kulikalia kimya hili ni highly irresponsible kwa upande wa serikali
Imeshangata family members au jirani zako wangapi? Labda tuanzie hapo. Nadhani kila mtu aanzie kwa immediate family members na sio hadithi za sijui mtaani wanasema nini, kama mtaani ipo na familia zetu pia zipo huko huko mtaani so hawawezi ugua au kufa bila sisi kujua.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,072
2,000
EYSLdRMWoAYYDUj.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom