Wewe unaepinga upo kila mtaa, Kijiji na wilaya?
Watu Kama ninyi, ndiyo mnasababishaga watu kupigwa burn na mods maana unapiga tu shetani nini?
Sijapinga nimeuliza swali dogo tuu!!! Kama kila mmoja wetu anaechangia humu akitoa data kuhusu close family members tutapata picha halisi ya jinsi watu walivyoathirika. Nianze na mimi binafsi thanks God mpaka sasa sijasikia mtu wangu aliyeugua corona/pneumonia au hata homa kali tangu covid ianze.
 
We nunua tangawizi, mchaichai chemsha iive ukiipua mix limao na asali gonga nusu kikombe asubuhi na jioni na familia yako ongeza immunite kwa mbegu za tikiti pia zina zink ya kutosha.

Sometime warm you body by drinking hot water until you sweat.
Mengine iachie serikali itajua cha kufanya.
Immunity, not immunite
 
Covid ipo na uzuri haichagui, hata hao wanaosema haipo inaendelea kuwafyeka tu Jamaa zao na wao hawana kinga wala exception kusema Covid haiwezi kuwafikia.
Ndio Maana wame ji isolate, Mbochi Tocha
Jikinge Mwenyewe usiwangoje wakwambie
Wanaujua ukweli ila kwa kuwa wana ego, wako tayari kuilinda ego yao kuliko kuchukua measures za kulinda wananchi dhidi ya janga hili
 
Mleta mada ahsante sana. Hii kitu ipo aisee...Madaktari wanakuandikia Pneumonia au ARDS/ C19.
Tangu tarehe 26 /12/2020 - 6/01/2021 nilikua Hospital aisee na dada yangu. Ila inawezekana mimi ndiyo nilimuambukiza. MUNGU mwema tulipata huduma na kutoka hospitali ila watu walikua wanadondoka jamani.
Serikali isione aibu katika hili.
 
Itc like Rich people are aware of this. Ila sisi makapuku tunatumiaga tu akili za kuambiwa kama nyumbu. Leo nmepishana na gar ilikuwa ni kama mtu na familia yake. Wote wamevaa barakoa kwenye gari. Na wamejifungia vioo full ac. Nikajiuliza sasa hapa nani ni mpumbavu...sisi tunaosubiri magufuli atuambie tuvae au tusivae barakoa ao hao waliojiamlia kuvaa na kufata taratibu kujilinda na covid.

Swali lingine nimejiuliza.
Hivi inaicost serikal kiasi gani kuwapa awateness wananch juu ya kujikinga na covid 19?
Kwani kuchukua tahadhari unasubiri hadi Magufuli akuambie?
 
Kuna rafiki yangu yupo morogoro amenipigia simu Leo kuniambia kuwa Corona ipo nichukue tahadhari

Mtaani kwao modeko wamezika mtu alikuwa na dalili zote za Corona alipokuwa hai.
Pana watu yafaa washatakiwe kwa kumisslead watu Ili wapotee Hali wao wamejificha majumbani kwao kukimbia corona,nani alikuambia sisi ni kisiwa.
 
Kuna rafiki yangu yupo morogoro amenipigia simu Leo kuniambia kuwa Corona ipo nichukue tahadhari

Mtaani kwao modeko wamezika mtu alikuwa na dalili zote za Corona alipokuwa hai.
Pana watu yafaa washatakiwe kwa kumisslead watu Ili wapotee Hali wao wamejificha majumbani kwao kukimbia corona,nani alikuambia sisi ni kisiwa.
 
Awareness kama tunayo inatosha ss kujikinga wenyewe. Serikali haijakataza raia kujikinga na covid.

Wakati mwingine ni bora kuwe hivi, Kwann tunataka panic irudi tena? Watu waanze kufa tena? Manesi wetu wanajulikana, wakishapanic nani atatoa huduma kwa wenye pumu, kifua kikuu, nimonia, n.k? Yaani serikali ikitangaza corona ipo tegemea matatizo zaidi ya mafanikio.
Kwa hali ilivyokuwa kipindi cha corona mi naona Kila mtu ajikinge, na kusali bila kusubiri tamko la serikali.
Kweli kabisa, yani mtu anang'ang'ania vitu visivyo hata na hoja, hivi kuna mtu asiyejua corona ipo hapa duniani?
Kwangu naiona serikali ipo sahihi kabisa kupiga kimya.
 
Mimi na wewe kwa sababu tuna kielimu kidogo tunaweza kuamini kuwa korona ipo
Ila kuna wale raia ambao uelewa wao wa masuala haya ni mdogo, tangu Magufuli atangaze Korona haipo TZ huwaambii kitu kuhusu korona, wanajua haipo tu!. Na bahati mbaya serikali iliamua makusudi kudiscourage njia za kujikinga na korona kama njia maalum ya kurudisha "ukawaida" (Normalcy), hilo ni kosa kubwa, ilitakiwa ihamasishe jitihada za kujikinga badala ya kuzipiga vijembe
Lakini njia za kujikinga na corona ni zipi hizo? Mbona hizi zinazofahamika duniani bado zinaendelea kuwaumiza watu?
 
Lakini njia za kujikinga na corona ni zipi hizo? Mbona hizi zinazofahamika duniani bado zinaendelea kuwaumiza watu?
Ndugu yangu, hivi kwa sababu wewe una uelewa unadhani wananchi wenzako hawa ambao majuzi tu katika baadhi ya mikoa walikuwa wanafundishwa na taasisi moja ya Taifa kubwa duniani kuosha mikono baada ya kunya nao ni waelewa kama wewe?
 
Back
Top Bottom