Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,910
114,692
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa.

Hoja yangu ya leo ni hii ,"kuna watu wana macho lakini hawaoni!, na wana masikio lakini hawasikii!". Swali ni je Chadema wana macho na yanaona?. Je wana masikio na yanasikia?

Kwenye hili la Wabunge 19, je Chadema wawasamehe wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke hata kama ni kulaaniwa?

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, kwa inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile.

Balile ameandika bandiko hili akiwa safarini jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile.

CHADEMA wasamehe wenye dhambi muuone ufalme wa Mbingu

Na Deodatus Balile, New Delhi, India

Leo nipo hapa Jijini Delhi, India. Kuwa hapa hakuniondolei utaratibu wangu wa kufatilia kinachoendelea hapo nyumbani nchini Tanzania ninachodhani ni muhimu kuliko yaliyoko huku. Katika nchi za watu huku walikwishajenga misingi imara ya miundombinu, demokrasia, maisha ya kijamii (imani za kidini) na mpangilio wa maisha ya kila familia.

Sitanii, nimesikia hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Miaka ya 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania. Nimemwelewa mno juu ya changamoto ya wanafunzi kushinda mitihani kwa alama za juu (AAA), lakini utendaji wao ni sifuri (ZZZ). Anaumia kichwa nini kinatokea. Anajiuliza kwa nini watoto wa siku hizi hawawezi kuandika barua ikawakilisha mawazo yao wakaeleweka?

Niwe mkweli, kwa sisi ambao tuna umri zaidi ya miaka 50 matokeo ya miaka ya sasa yanatushangaza. Sisi somo la mwanafunzi kupata alama A, ilikuwa tunaulizana. Kwenye kata nzima tunamfahamu kuwa fulani kapata A. Lakini pia ukweli mchungu, alama za ufauli wakati wetu aliyepata D (yaani maksi 21), bado alikuwa na uwezo mkubwa. Tunao makandarasi, walimu na kada nyingi waliopata alama hizi, lakini wanao uelewa wa hali ya juu.

Mwaka wetu tuliohitimu wote darasa la saba, hata ambao hawakuendelea na elimu ya sekondari, leo tukikutana tunazungumza Kiingereza kwa kiwango ambacho bado baadhi ya wanafunzi wa sasa wenye shahada ya kwanza hawawezi. Tulifundishwa kazi za mikono, Sanaa, Sayansi Kimu, Kilimo… hadi leo nafahamu kutengeneza wanga kwa kutumia viazi na mihogo. Haya nilifundishwa shule ya msingi mwaka 1982.

Tulikuwa na mwalimu wa Kiingereza anaitwa Marcel Rweyemamu, ukikosea anakundikia “See Me”. Hadi leo darasa letu kama yupo anayekosea, ni kwa utashi wake. Niishie hapo. Chuoni tulikuwa na Fr. Theodore W. Walters (Fr. Ted Walters), ilikuwa ukikosea anakuandikia “Re Do”. Tulikuwa na Mwalimu Harry Kalokora, yeye alikuwa na elimu ya cheti, ila ana uzoefu wa miaka 45. Alihamishia ujuzi wake wote kwetu.

Sitanii, kichwa cha Makala hii, kinasema: “CHADEMA wasamehe wenye dhambi muuone ufalme wa Mbingu”. Nafahamu wengi wamekwishandika juu ya wabunge 19 wa Viti Maalum wa CHADEMA walioapishwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa BAWACHA, Halima Mdee. Nimeisoma hukumu iliyotolewa na Jaji Cyprian Mkeha. Nafahamu Watanzania mmeijadili kwa kiasi kikubwa hukumu hii.

Pamoja na kwamba mimi ni Mwanasheria kwa taaluma, hapa sitajadili vifungu vya kisheria, bali najaribu kuwaza kimantiki. Niliwahi kumwambia mke wangu, kuwa binasi sipendi mchezo wa ndondi (ngumi). Ninao marafiki zangu, Masyaga Matinyi na Manyerere Jackton, hawa ni wapenzi kindakindaki wa masumbwi. Sishangai maana wanatokea “Kanda Maalum a.k.a Musoma line.”

Kwa hakika ninachokifahamu, katika mchezo wa ngumi, wote anayeshinda na anayeshindwa baada ya mchezo kila mtu kwa nafasi yake anakuwa na maumivu. Bingwa wa masumbwi wa kihistoria duniani, Muhammad Ali, aliyezaliwa Januari 17, 1942 na kufaridi dunia Juni 3, 2016 alishinda mapambano mengi, ila mwisho wa siku alifariki kwa ugonjwa wa kutetemeka kutokana na ngumi zilizopata kichwa chake.

Mchezo unaondelea kati ya CHADEMA na wabunge 19, nikiungalia hauna tofauti sana na mchezo wa ngumi. Baadhi ya viongozi wasipofikiri sawa sawa wakadhani wanawakomoa akina Mdee na wenzake, watajikuta wanayeyusha imani ya jamii kwa chama chao. Wakumbuke kilichovimaliza vyama vya NCCR – Mageuzi - Ugomvi wa Agustino Mrema na Mabere Marando.

Chama cha TLP sijui kama kimeishatolewa mipira ya Oxygen ICU, ilikuwa ni Ugomvi wa Agustino Mrema na Leo Lwekamwa. CUF iliyobaki kama jeshi la mtu mmoja ni ugomvi wa Prof. Ibrahim Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad. Kwamba CHADEMA walinusurika wimbi la Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Richard Mwigamba na wengine, si la kuwapofusha kudhani tayari wamevuka mto.

Sitanii, sote tunafahamu kilichotokea mwaka 2019 na 2020. Hata kundi lililodaiwa kuwa limeunga mkono juhudi, kuna maelezo kuwa liliunga mkono “M-Pesa na Vitisho vya Kesi za Uhujumu Uchumi”, hivyo likajisalimisha. Leo Rais Samia amerejesha uhuru wa kisiasa hasa baada ya kuunda Kikosi Kazi cha Hali ya Siasa nchini, ambacho kimezaa hizo sheria tatu zilizofikishwa bungeni.

Nimesema leo sitajadili nani anashinda kisheria, nani ana haki na nani mkosefu. Katika hili kama CHADEMA, mlivyokaa na kuzungumza na Rais Samia wa CCM, nadhani kukaa mkazungumza na Halima Mdee na wenzake wa CHADEMA, hili si gumu. Lindeni imani ya Watanzania kwa chama chenu. Mkiendeleza ugomvi huu, mtafika 2025 mkipambana na kesi baada ya nyingine, hawa wabunge 19 watamaliza muda wao wa ubunge watakwenda vyama vingine na kwenye kampeni watakuwa mwiba kwenu.

Ndiyo maana nimesema, kwa fikira za kuona mbali na kwa ukweli kuwa Rais Samia amebadili mazingira ya kufanya siasa, wakati umefika ninyi “CHADEMA wasamehe wenye dhambi muuone ufalme wa Mbingu”. Taasisi nyingi hufungua miradi na kuifunga isipofanya vizuri. Inawezekana mradi wa Uchaguzi wa 2020 ulipata hitilafu na sote tunajua kilichotokea sitaki kumtaja aliyetufikisha hapo kusikojulikana. CHADEMA kaeni, fungueni ukurasa mpya. Kuna maisha baada ya ugomvi. Hiki mnachofanya hakina tofauti na mchezo wa gumi. Mungu ibariki Tanzania.
Mwisho wa kunukuu

Chief @⁨Balile⁩ , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kuhusu kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaepushia Chadema karma ya mambo
mabaya waliowatenda hawa wadada 19 ambao mimi nawaita ni mashujaa, hivyo huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema wenye maslahi kwa Chadema na maslahi kwa taifa only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, nilipandisha makala mfufulizo za Kilio cha Haki, nikiangazia haki jinai.
Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo tulimpongeza rais Samia kwa kauli hii baada ya Freeman Mbowe kuombewa msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Baada tuu ya bandiko hili, haukupita muda hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!,

Sisi wa kupongeza tukapongeza
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Sasa kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.

Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent
Na nikashauri Chadema

CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Na nikawashauri tena Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
Wakati wa safari ya kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020 nilishauri For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

Na baada ya matokeo ya uchaguzi, nikashauri tena Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Tukatoa maombi Ombi Maalum kwa Rais Magufuli: Mteue Zitto Kabwe kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, ndiye mpinzani pekee mzalendo, Capable kuongoza PAC!

Chadema walipogomea kutambua matokeo na kususia kuteua viti maalum, tulitoa ushauri Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Pia tukaishauri Chadema Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Hatukuishia kuishauri pia tukaipo onyo la the consequences Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Kufuatia hali hiyo, kina Mdee na makamanda hao 19 walipoibukia Bungeni na kuapishiwa pale gereji ya Bungeni, niliwapongeza "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Na nikashauri Chadema CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Na nikawashauri tena Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kilichofuata ni sarakasi na sarakasi za kutimuana kwa mtindo wa kangaroo court Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?

Nikaja A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?

Nikaja Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?

Nikaja Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

Nikaja Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi

Nikaja Kutotambua Matokeo ni Kutomtambua Rais, Serikali na Bunge. Rais Akiishaapishwa ni Rais! Tutaendelea kuruhusu hali hii Mpaka Lini?

Nikaja Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Japo kwa jicho la juu juu, hao 19, wanaonekana kama wameshinda kesi yao mahakamani but in reality ni wameshindwa na hili nililisema The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! kwasababu katiba ya Chadema ina kipengele kilicho kinyume cha katiba, mwanachama wa Chadema akifungua shauri lolote mahakani, akishindwa kesi ni amejifukuzisha, hivyo Mahakama tayari imeishabariki kufukuzwa kwao, salama yao ni kusamehewa tuu!.

Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.

It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.

Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.

Merry Christmas

Paskali.
Update swali very objective
Unaposema kuwatimua kwa haki una maana gani?
Mkuu Bulesi , there you are.
Katiba ya Chadema imeweka utaratibu wa kuwatimua wanachama wake, nimekuwekea katiba ya Chadema ya 2006, hapo chini , kwanini CC ya Chadema imewatimua kinyume cha utaratibu wa kwenye katiba yao?.

Kuwatimua kwa haki ni kuwatimua kwa mujibu wa katiba ya Chadema.

Hata mtu anayehukumiwa kunyonywa, adhabu hiyo inatekelezwa kwa utaratibu.
 1. Baada ya hukumu ya kunyongwa, mtuhumiwa atahamishiwa gereza la kunyongea kwa Tanzania ni Gereza la Isanga.
 2. Huko gerezani, huwekwa chumba cha peke yake, na hafanyi kazi yoyote zaidi ya kula na kulala.
 3. Mfungwa huyo hupatiwa huduma za ushauri nasaha kumuandaa kwa kifo.
 4. Pia hupatiwa huduma za kiroho kwa mujibu wa imani ya dini yake ili kumuandaa kwenda kukutana na muumba wake.
 5. Nakala ya hukumu hupelekwa Ikulu kutayarishiwa Death Warrant ambayo lazima Rais wa nchi aisaini ndipo adhabu hiyo hutekelezwa.
 6. Rais akiisha saini death warrant, itaonyesha mfungwa huyo atanyongwa lini, wapi na saa ngapi.
 7. Ndugu wa mfungwa huarifiwa, kuwapa fursa ya kuja kumuaga kabla ya kunyongwa.
 8. Ndugu wa aliyemua hujulishwa kama watapenda kushuhudia.
 9. Siku ya kunyongwa hufanyiwa usafi, shaving, new dress, heavy breakfast.
 10. Kabla ya kunyongwa daktari humpima kujiridhisha yuko fit kiafya, akikutwa na ugonjwa wowote, hata homa tuu, au mafua, adhabu haitekelezwi, anapaswa kutibiwa kwanza apone ndipo anyongwe.
 11. Akikutwa fit, hupewa fursa ya kuaga ndugu zake na kutoa neno lolote la mwisho.
 12. Viongozi wa dini yake humsalia sala ya mwisho, kama ni Mkristo Mkatoliki hupakwa mafuta ya krisma.
 13. Ndipo hunyongwa na kama ni Muislamu hunyongwa kwa kutizamishwa kibla.
 14. Baada ya kunyongwa, daktari hiitwa kuthibitisha amekufa.
 15. Familia hukabidhiwa mwili kwenda kuuzika.
Huo ni utaratibu.
Kumfutia mwanachama uanachama wake ndio capital punishment kwenye chama lazima ufunyike kwa uangalifu na umakini kwa mujibu wa katiba ya Chadema. Kwanini haukufanyika?.
Kwa faida ya wasio na uwezo wa kuisoma katiba, nimewawekea hivyo vifungu hapa

Kwa Vile Kamati Kuu ya Chadema Imewaita Kina Halima Mdee ili Iwahoji, na Wamegomea Mwito, Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.

6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza: (haya ni masherti ya vikao vya nidhamu)
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu ya maandishi katika muda usiopungua wiki mbili. (Mashitaka ni kwa maandishi na Majibu ni kwa maandishi na sio kuitana kienyeji enyeji)

(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
(d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa ( kwenye issue ya kina Halima Mdee, kulikuwa na uharaka huu?.) isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.

Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
 • Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
 • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
 • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
 • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, kugomea wito huo wa kienyeji wa kufika mbele ya Kangaroo court iitwayo CC ya Chadema ambapo CC hiyo inapokaa kama a Kangaroo court, kazi yake huwa ni moja tuu, kuchinja bila kueleleza Kibla!. Ukichinja bila kuelekeza Kibla, kunahesabika ni kunyonga. Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!.

Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Paskali
 
Attachments

 • KATIBA CHADEMA 2016.pdf
  21.2 MB · Views: 3
Andiko nzuri my Adv.Mayala, ila HAKUNA mgogoro ndani ya CHADEMA, huo mgogoro unaouna wewe kama mwandishi, issue hii CHADEMA walishatoa uamuzi wake na uamuzi ule ulikua kuwafukuza uanachama wale watuhumiwa, kwa shinikizo la chama dola wakaenda mahakamani na hukumu imetoka, case hii imefungwa, na tuelewe kuwa kujiunga na chama cha kisiasa ni hiari ila ni muhimu katiba ya chama hicho kuiheshimu.Tanzania yangu inahitaji kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
 
Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii Kuna Watu Wana Macho lakini Hawaoni!, Wana Masikio lakini Hawasikii!. Je Chadema wana macho na yanaona?, au wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, Jee Chadema Wawasamehe Wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke ?.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, nimepata inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile

Balile ameandika bandiko hili akiwa safari jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile

Mwisho wa kunukuu

Chief @⁨Balile⁩ , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaupushia Chadema karma ya waliwatendea walichowatendea hao 19!. Kiukweli kabisa huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.

Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea".

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, kwanza tulieleza humu Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Kuna watu tulimuombea msamaha
Kwa jambo lenyewe anzia hapa, Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Kisha nenda hapa Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Kisha hapa, Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?

Kisha hapa Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!, kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.

Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent

Na nikashauri Chadema CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Na nikawashauri tena Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kilichofuata ni sarakasi na sarakasi za kutimuana kwa mtindo wa kangaroo court

Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.

It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.

Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.

Merry Christmas

Paskali.

Paskali naomba uwe mkweli. Siku hizi kuna wakati huleti mada elimishi bali unaleta mada za kuwapumbaza watu.

Wewe leta tu mada, lakini usiseme kuwa ni elimishi. Watu wataamua wenyewe kama ni mada elimishi au mada pumbazishi.
 
Mayalla nina wasiwasi hao wabunge 19 utakuwa unakuta nao / au na mwakilishi wao mafichoni, au kwa maslahi mapana ya chama chako.

- Sijui kwanini mnataka hao wanawake wasamehewe bila kwanza wao kuomba radhi, au ndio mnataka kufanya ionekane Chadema walikosea kuwaadhibu?

Wanatakiwa kuomba radhi kwanza, ndio chama chao kiamue kuwasamehe au vinginevyo. Mdee alivyo na jeuri siku hizi...

NB. Unatakiwa ujue kutofautisha vichwa vya habari kwa makala zako, makala gani iwe kwa maslahi ya taifa, na makala ipi iwe kwa maslahi ya CCM.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Haishangazi sana,Baba yako alikua afisa usalama,Mama yako pia afisa usalama!!

Ikiwa leo tunaona vitoto vya kina Mwigulu na CCM wengine wapo makada,wewe kuendelea kua afisa usalama wa spinning and clearance ya CCM ni sehemu ya maisha!!

Uligombea kura za maoni Kawe,huwezi ukakaa ukaishauri kheri CHADEMA,ni mwandishi wa kimkakati,haitashangaza siku ya mazishi yako ukibebwa na "askari" na ukapigiwa risasi kadhaa hewani ila Jimbo la Kawe CCM mtauana,Manara yupo,Gwajuma yupo,Mdee yupo,mtoto wa Warioba etc etc
 
Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii Kuna Watu Wana Macho lakini Hawaoni!, Wana Masikio lakini Hawasikii!. Je Chadema wana macho na yanaona?, au wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, Jee Chadema Wawasamehe Wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke ?.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, nimepata inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile

Balile ameandika bandiko hili akiwa safari jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile

Mwisho wa kunukuu

Chief @⁨Balile⁩ , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaupushia Chadema karma ya waliwatendea walichowatendea hao 19!. Kiukweli kabisa huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.

Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea".

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, kwanza tulieleza humu Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Kuna watu tulimuombea msamaha
Kwa jambo lenyewe anzia hapa, Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Kisha nenda hapa Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Kisha hapa, Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?

Kisha hapa Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!, kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.

Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent

Na nikashauri Chadema CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Na nikawashauri tena Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kilichofuata ni sarakasi na sarakasi za kutimuana kwa mtindo wa kangaroo court

Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.

It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.

Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.

Merry Christmas

Paskali.
1. Kusamehe maana yake ni nini? Ni mtu mwenyewe anayehusika kuona alilolifanya ni kosa au baya na anajuta kwa nini alilifanya na anaomba asamehewe huku akisema hatarudia tena. Hii ndiyo maana halisi ya kusamehe.
2. Kama mhusika (alyefanya kosa/baya) haoni kosa/baya alilolifanya na kwa sababu hiyo haoni haja ya kuomba msamaha, hastahili kusamehewa. Kwa maneno mengine, kumsamehe mtu wa namna hii ni kazi bure!
3. Suala la wabunge 19 kuna issues 2: 1) Je, waligushi barua na saini na kwenda kuapishwa bila ridhaa ya Chadema au 2) waliteuliwa na Chadema na kuandikiwa barua ya kuwaidhinisha waapishwe? Kwa maneno, mengine wanaosema ukweli katika jambo hili ni Chadema au ni hao wabunge 19? Kama wanaosema ukweli ni hao 19 na katika yote wanaomba warudi (kwa vile wanaona hawana cha kutubu na hawana sababu ya kutubu), hapa ni kweli wasamehewe kwa sababu Chadema wamewakosea. Kama wanaosema ukweli ni Chadema na hao 19 pamoja na kuona kwamba walifanya kosa na wanakomaa kutosema kwamba walifanya kosa isipokuwa wanataka kusamehewa bila kuona kosa lao, hapa hawastahili kusamehewa. Acha Chadema ife, lakini siyo kusamehe watu ambao wao wenyewe hawataki kukiri kosa lao (labda tu kwa maana kwamba kwa sasa issue ya hao 19 kwa Chadema si issue tena ya kuwapotezea muda na fedha).
4. Hivyo, kwa upande wangu kama ni kusamehe lazima kuwe na justification (and the justification is for them to come forward and say they did ABC and now they are sorry and ask for forgiveness), but if there is no justification I cannot see why they should be forgiven.
 
CDM inawahitaji inaowaita COVID 19. Hii batch mpya bado sana kufikia hao waliopo bungeni. Perfomance kwenye nafasi za uongozi ndani ya chama haiko vizuri, mimi sikumbuki hata lini nimewasikia BAWACHA. Yaani Ruge halinganishiki na Mdee, Matiko halinganishiki na sijui nani. Bulaya tumemlea CCM yule ni chotara simsifii.
Wawasamehe,wawaache waendelee kujenga chama chao na kuandaa wajao. Mimi binafsi siwataki hao wanawake waje CCM maana sitakuwa na jipya la kujifunza huko. Nilitembea majimbo ambayo hao wanawake walioko bungeni waligombea,nilijifunza mengi sana. Napokea matusi
 
Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii Kuna Watu Wana Macho lakini Hawaoni!, Wana Masikio lakini Hawasikii!. Je Chadema wana macho na yanaona?, au wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, Jee Chadema Wawasamehe Wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke ?.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, nimepata inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile

Balile ameandika bandiko hili akiwa safari jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile

Mwisho wa kunukuu

Chief @⁨Balile⁩ , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaupushia Chadema karma ya waliwatendea walichowatendea hao 19!. Kiukweli kabisa huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.

Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea".

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, kwanza tulieleza humu Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Kuna watu tulimuombea msamaha
Kwa jambo lenyewe anzia hapa, Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Kisha nenda hapa Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Kisha hapa, Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?

Kisha hapa Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!, kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.

Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent

Na nikashauri Chadema CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Na nikawashauri tena Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kilichofuata ni sarakasi na sarakasi za kutimuana kwa mtindo wa kangaroo court

Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.

It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.

Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.

Merry Christmas

Paskali.
Hivi mzee Bado Kuna watu wanakuchukulia serous? Nitashangaa sana kama Bado wapo.
 
Wewe mkuu una tatizo kubwa sana. Kimsingi, lengo la mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kuwapa nguvu wananchi kuchagua viongozi wao na kuamua mustakabali wa nchi yao. Hata CHADEMA ikifa leo hii haitakuwa mwisho wa upinzani. Mapambano ya wananchi yataendelea kwa namna zozote zile.

Ni ajabu kwamba wewe unatumia nguvu nyingi sana kuandika mabandiko kadhaa yanayoishutumu (unadai unaishauri) CHADEMA kama vile ndiyo inayoharibu mustakabali wa nchi hii. Unataka CHADEMA ipokee na kukubali kila adha inayoletewa na serikali ya CCM. Eti ikubali kila “nusu shari” ili i-survive; isife kimoja! Ingekuwa wewe ni kada au mfuasi makini wa CHADEMA ingefikirisha. Ingekuwa ni ushauri wa mara moja tungesema well, huenda ni jambo la kawaida. Lakini hii toka kwa mtu mwenye mitazamo ya kijanja janja ni zaidi OBSESSION kabisa!

You’re not honest my friend. Anyone can clearly see that you’re on a one track mission to bring CHADEMA down on its knees before the might of the state. For exactly what gratification OR how many “pieces of silver”? That remains to be seen.
 
Back
Top Bottom