Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3. Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4. Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5. Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7. Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8. Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
Nimecheka sana ushauri huu
 
Wanabodi, kwa trendi hii anayoendanayo Rais Samia Suluhu Hassan katika eneo la demokrasia, natabiri atashinda Tuzo ya Mo Ibrahim aliyoikosa Nzee Nkapa ikaenda kwa Chissano wa Msumbiji.

Mauaji ya Zanzibar yalimharibia sana Nkapa. Hatuyategemei kwa Hangaya. Nawasilisha.

Freeman
 
Habari ,Afya ni mtaji namba Moja wa kila mtu Duniani ukiachana na mitaji kama fedha na Mali .Kwa kusema Hivi namaanisha ili Taifa lolote liweze piga hatua tuna hitaji wananchi wenye Afya njema .

Kama serikali ilivyojipambanua katika nia ya Afya kwa Wote .Mimi kwa upande wangu nimeshashuhudia vifo vingi vya watanzania ambavyo ni matokeo ya kuchelewa au kutofika vituo vya Vya Afya sababu Kubwa ikiwa ni Kukosa Bima au Kukosa Pesa za matibabu ,nimeona ni vyema nitoe mawazo kuhusiana na hili Jambo la Afya kwa wote huenda tunaweza isaidia serikali kulitimiza kwa Urahisi .

NHIF ni bima ya Taifa ambayo imejitahidi kuweza kumfikia kila mtanzania hata kupitia njia iliyokuja nayo ya vifurushi, lakini bado changamoto kubwa imebakia ni Ukosefu wa Fedha na elimu .Binafsi nlijaribu kufikiri hata tukisema tuweke kila mtu achangie elfu 20 kwa Mwaka bado sio Watanzania wote watapata Bima.

Baada ya kujiuliza sana nkapata mawazo mawili 1. kwamba ni lazima kipatikane kitu ambao kitaweza kuingiza fedha Ambayo itatumika katika Matibabu ya watanzania wote 2.Serikali ipange fedha kila mwaka kwenye bajeti kwa ajili ya Matibabu nkagundua itakuwa Ngumu ,nkabaki na Wazo la kwanza .

Katika wazo la kwanza nlipata mawazo nliwaza sana lakini nlikuja kuishia na Wazo la Kutumia TOZO za miamala ya simu na kibenki .Kwa kifupi kwa Siku inafanyanyika miamala mingi na ni chanzo ambacho ni cha uhakika.

Serikali itaweka TOZO ambayo itaonekana inaweza tengeneza kiasi cha kutosha kulingana na Tathimini itayofanywa kwa hospitali zinatoa huduma hapa Tanzania ingawa inaweza kwa Mwanzo ikazidi sana kulingana na watu kumiminika kwa wingi vituo vya Afya hivyo wanaweza anza na watoto/wanafunzi na mama wajawazito iwe binafsi au serikalini ni bure .

Kutokana na Makusanyo ya Mwezi vituo hivyo vya Afya vitalipwa
Pesa kulingana na idadi na Matibabu yaliyo tolewa hii mwa Mwanzo itakuwa Ngumu baadae itazoeleka .
 
Mm kama mdau wa elimu,naomba kumshauri Rais amwondoshe Msonde ktk Baraza la mitihani kwan anafanaya kazi kwa mazoea baada ya kukaa muda mwingi ktk nafasi hiyo,kaanzisha utaratibu wa kiubaguzi na WA kiupuuzi hasa mwaka huu, ktk usimamiz wa mitihani kapeleka majina ya walistafu na walio hama ktk halmashauri nchi nzima!

Lkn pia watu wamejirudia zaid ya mara sita ktk usimizi wa mitihani sasa utaratibu Gani huo.

Huyu anataka kuharibu mfumo wa elimu na kuwakatisha baadhi ya walimu ambao hawafikiriwi ktkt nafasi hizo lkn pia Kuna watu wanaenda marking kwa kujirudia takriban Kila marking hapo Kuna utaratibu Gani huo Rais
 
Huku mtaani sio pazuri

Hakuna maji, Hakuna umeme, wizi na ukabaji umezidi, Jeshi la polisi linatuonea sanna

Raisi anamajukumu mengi ila maji, umeme na usalama wa raia kiwekwe kipaumbele
 
Kwako Mh Rais ikikupendeza 2022 uje na mkeka wa Mawaziri wenye sura ya kutokujipendekeza kwako.

Ipo mifano hai ya manaibu mawaziri wanauwezo kuliko hata mawaziri.

Anza na wizara hizi

1. Fedha
2. Mambo ya ndani
3. Afya
4. Uwekezaji
5. Biashara
6. Nishati,kwa matazamio
7. Mali asili akae Bashe
8. Ujenzi ondoa Mwikwabe
9. Sera/Vijana abaki ndelananga tu,wengine hao badilisha
10. Tamisemi,Silinde mzigo
11. Mambo ya Nje
12. Sheria/Katiba
 
Rais wa nchi lazima uwe self assertive, watu watambue kweli ofisi ya Rais iko na mtu mwenye mamlaka.

Kwa kipindi cha miezi sita ya uongozi wako kumeibuka migogoro ya ajabu. Mara maji hakuna, mara umeme sijui umefanyaje.

Kodi hakuna umekimbilia kutoza watu kwenye miamala. Kutwa kuomba omba kwa wazungu na kujilemaza ati sisi masikini hatujiwezi!

Rais epuka migogoro inayoleta mvutano kati yako na wananchi. Jenga nchi, wape watu matumaini na zungumza lugha inayoonesha unajitambua.

Leo umekuja na habari za maji kuchepushwa. Mara hadithi za sijui tabia ya nchii imefanyaje!!! You speak very recklessly and irresponsibly!

Do the job, acha ubabaishajii. Jenga serikali ya watu ambao ni morally qualified. Achana na magenge ya ajabu ajabu.

Utamaliza miaka mitatu ijayo hakuna ulilolifanya zaidi ya kubomoa vibanda vya mamantilie! Ati unasafisha jiji? ili iweje!!

Makinika. Do the job!
 
Kabla ya kutoa hoja hakikisha kwanza hauna jazba na unayemwongelea, hii itakufanya uitumie akili yako vizuri kwenye kufikiri.

Kuendelea kujiweka kwenye kundi la nchi tajiri ni kujitekenya na kucheka mwenyewe. Sisi ni masikini wa Mali na hata akili na hili limejidhihirisha hata kwa post yako.

Tumpe Mh. Rais nafasi ya kututumikia huku tukimshauri yaliyo mema na kumuunga mkono badala ya kuendeleza chuki na kisirani na dharau dhidi yake na mamlaka.

Huyu ndiye Rais wetu iwe tunakubali au hatukubali.
 
Hali ikiendelea ilivyo, nakushauri usianzishe miradi mipya mikubwa.

Naona kumezuka utamaduni Wa anayeingia kuponda miradi ya mtangulizi wake, nafasi ya wewe kupita 2025 bado iko chini ya 40℅ unaweza kuianzisha mwingine akaja akaibwaga sababu kubwa ninayoiona serikali imeshindwa kuchutama kwa makosa yaliyofanywa na awamu ya Tano, na wanaNchi wanaona kumekuwa na unafiki kwa sababu mlifumbia macho yaliyofanyika kwa makosa na mkabaki kusifia hapa kazi tu.

Unaweza kubaki kimya watu wakapata majibu kwa vitendo vyako pale tu vitendo vitakapo tafsiri kule tuendako.

Yapo mambo ambayo yanapashwa yatolewe elimu ya kutosha kwa watu wako ili wasikutwishe zigo lisilo kuhusu.

Elimu kuhusu uhaba Wa Mbolea na bei juu ya mafuta, athari za kiuchumi za covid19, elimu kuhusu kwa mini sasa! Bandari ya Bwagamoyo na nini viongozi walio wengi walipiga makofi kuunga mkono uongo uliotajwa kwamba kungekuwepo madhira ya kuwa na bandari hiyo ikatajwa kwamba " ni mwendawazimu tu ndiye angekubali masharti ya wawekezaji" he Leo ikoje?

Uongo uliotajwa kuhusiana na uanzishwaji Wa shirika ndege kwamba ilikuwa ni hasara kubwa, Leo mnaendelea kuongeza ndege nyingine.

Kampeni mbaya inayozunguka midomoni mwa watu kwamba Mstaafu awamu ya NNE ana mkono katika yote uyafanyayo.

Mimi siamini hivyo lakini inaweza kuharibu taswila ya awamu yako.

Tumeweka msukumo mkubwa kwa elimu (labda ndiyo matakwa ya watoa misaada na mikopo )lakini soon tutaagiza chakula Nje kwa sababu watu wanaelekea kususia kulima na hifadhi ya chakula haijaangaliwa sana.

Mwisho niseme huwezi kuwapendeza wote , nakuombea Mungu akuongoze kufanya maamuzi sahihi kwa watu wako suala la msingi si wewe kuwa Rais Ila yale utakayoyaacha nyuma yako. Una mifano mingi iliyokutangulia.

Nyimbo zetu na bwembwe zetu wanachama wako zinaweza kukufanya udhani mambo yako poa, maana tumezoea unafiki hatusemi ukweli ili tupendwe na viongozi lakini kupata anayeweza kukwambia ukweli kama huu ni nadra sana wengi wako kwa ajili ya mkate wao basi.

Mungu akulinde
Mungu akufanikishe
Mungu akuhekimishe
Mungu aondoe madhira na majanga katika awamu zako ili amani itawale.
KAZI NJEMA ZIENDELEE.
 
Wana JF

Unaweza ukaishi na nyoka ukamkumbatia na kumpiga mabusu wakati ukizingatia umri wa meno yake, nyoka kibogoyo mwenye sumu kali hana madhara mpaka meno yake yawe na utayari kudhuru mtu.

Haya yametokea kwa idara ya mikopo Tanzania, ule ukritimba bado haujapata tiba, waliofanikiwa kupata mikopo ni wale waliopenyeza shiringi mambo waende, wale kapuku wote wamemwagwa kwenye mabwawa.

Pengine mama kutokana na shughuli ufatilii, na wazili wako yuko bize na ukame, kuwaletea wana daresalaam maji wapunguze kunuka vikwapa, mama vijana wako wamepitiwa na utapia mulo kwa kukosa boom.

Wengi wao pamoja na wazazi wao walikuona mkombozi sana baada ya mwendambinguni kuondoa fursa ya kuwasomesha wasaka tonge eti kwa kuwa wamepitia shule za watakavitu (sts) bila kujua kuwa walikosa nafasi serikalini wazazi wakajinyima wakapambana.

Nakuomba mama tuma watu wako pale kwenye mkwamo uwaokoe vijana wala mihogo.
 
Binafsi nimekua mfuatiliaji mkubwa wa utendaji kazi wa serikali hii y awamu ya sita kwenye sekta na miradi mbalimbali mtambuka hakika ni vema na haki kusema kwamba kasi ya Mh. Samia kwenye maendeleo inatisha. Kama kutakua na kata ambayo tangu Rais Samia ashike hatamu ya uongozi haijapata mradi mpya basi ni chahche mno lakini kwa ujumla wake miradi mbalimbali ya maendeleo Bara na visiwani inaendelea.

Rais huyu anawavusha watanzania katika kipndi hiki ambacho serikali nyingi zimeathiriwa na janga la corona lakini amejitahidi kuinawirisha nchi yetu huko vijijini na mijini neeema tupu zimemwagika. Ni muda sahihi wa watanzania wote kwenda nae pamoja ili kuifikia nchi ya ahadi. Ni Rais wa kazi na matokeo ya haraka sana , huyu ni lulu ya taifa tuitunze na kuilinda.

Hakika miradi ya MAMA ni suluhu ya changamoto za Watanzania .
 
Back
Top Bottom