Kabla hujaamua aina ya gari na lini unataka kumiliki gari ya kwa mala ya kwanza basi muhim ukafaham haya yafuatayo.

1. Tengeneza Bajeti. Baadhi ya watu katika Jamii zetu, wamekua na kawaida ya kununua gari bila kuzingatia bajeti ya vitu kama matengenezo, mafuta, malipo ya maegesho, Vibali, n.k jambo linalopelekea kushindwa kufanya mambo mengine ya msingi iwapo kipato ni cha kati na aina ya gari unalomiliki linahitaji bajeti kubwa....
Kuna gari inaitwa Rush,hii spare zake ni nyingi au ni ghali sana? Nimeona cc zake hazitofautiani na kina Raum,Premio na Ti.
 
hongera kiongozi lakini ningependa kufahamu zaidi kuhusu hizi gari za kuitwa Toyota Opa,,

natanguliza shukurani,,
Opa ni gari nzuri pia ya Toyota ila sijaiweka katoka orodha kwa sababu kadhaa kama kuadimika kwake kwenye soko la huko Japan, na pia ni gari yenye injini ya Cc 1800 na Cc 2000 ambayo sio nzuri sana kwa mtu anayeanza kumiliki gari ukilinganisha na injini za magari mengine za Cc 1500 ambazo pia ni Vvti.

Ikitokea ukaipata Opa kwa sasa ni gari nzuri na ngumu ambayo inafanania na Toyota Wish kwa vitu vitu vingi, tofauti kubwa ni kua Opa ni ya Zamani, Wish ilitengenezwa badae kidogo
 
Kuna gari inaitwa Rush,hii spare zake ni nyingi au ni ghali sana? Nimeona cc zake hazitofautiani na kina Raum,Premio na Ti.
Hii nayo ni gari nzuri ya juu, sijaiweka hapo kwa sababu ya 4WD ambayo wakati mwingine hulazimisha gari kutumia mafuta zaidi touti na Toyota Cami ambayo ina Cc 1300, lakini pia manunuzi kwa kuagiza gari hii ni zaidi ya 14m ambayo inaweza kua changamoto kwa mtu anayemiliki gari kwa mara ya kwanza
 
Nasubiri jibu pia Kwenye hili
Hatukopeshi boss wangu. Ila tuna utaratibu wa mtu kuwekeza kidogo kidogo iwapo yeye mwenyewe anapata ugumu kutimiza hilo lengo lake. Kama amepungukiwa kidogo tunaweza kumuunganisha na taasisi za kutoa mikopo wao wakamsapoti, changamoto ya tasisi hizo ni kua unapewa mda mfupi wa marejesho na pia riba ni juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom