Kwa mahitaji ya gari bora ya kutembelea, agiza gari yako na Kimomwe Motors Tanzania Limited

Nissan X- Trail ya 2003
Cc: 1990
Seats: 5
4while drive
Km: 82,000
Bei: 16,000,000 mpaka mkononi
Muda wa kusubiri: Siku 30-35

Gari hii ulaji wake wa mafuta ni wastani, madhubuti kwa barabara zetu za lami na vumbi pia, nzuri kwa safari ndefu, mafundi wake wanapatikana, vipuri vyeke vinapatikana kwa gharama za juu kiasi (ila ukifunga hudumu kwa mda mrefu), pia injini, gia box na body yake huvumilia shida kwa wastani. (Zinahitaji uangalizi kila unapohisi tatizo). Pia huuzika kwa gharama ya chini zaidi pindi utapohitaji kuiuza.

Mawasiliano: 0754 455865

Ofisi zetu zipo Magomeni Mapipa.View attachment 956848
Wewe umekuwa mkweli
 
PhotoGridLite_1565800593160.jpg
Habari ya jioni ndugu wadau?

Pichani ni baadhi ya gari chache tulizopokea kwa ajili ya wateja wetu.

Kwa msaada na maelezo zaidi kuhusu huduma zetu, usisite kutembelea ofisi zetu zilizopo Magomeni Mapipa mkabala na kituo cha mwendo kasi au piga sim namba 0746267740
 
Kabla hujaamua aina ya gari na lini unataka kumiliki gari ya kwa mala ya kwanza basi muhim ukafaham haya yafuatayo.

1. Tengeneza Bajeti. Baadhi ya watu katika Jamii zetu, wamekua na kawaida ya kununua gari bila kuzingatia bajeti ya vitu kama matengenezo, mafuta, malipo ya maegesho, Vibali, n.k jambo linalopelekea kushindwa kufanya mambo mengine ya msingi iwapo kipato ni cha kati na aina ya gari unalomiliki linahitaji bajeti kubwa.

2. Amua utatumia utaratibu gani wa malipo. Kuna njia za kulipia gari yako kama vile kulipia kwa awamu, kupewa mkopo na taasisi za fedha, au kuhifadhi we mwenyewe na kilipia yote kwa mara moja. Ni muhim kuangalia hili ili kujiepusha na hali ya kujiumiza kiuchumi pindi unapoamua kumiliki gari kwa mara ya kwanza. Iwapo kipato ni cha kati unaweza kuzungumza na muuzaji husika ukalipia kidogo kidogo na mwishowe ukamalizia na kupewa gari yako, hii itakuepusha kumaliza mpaka akiba ambayo ingeweza kukusaidia wakati wa dharula.

3. Angalia unataka nini kwenye gari yako. Usinunue gari kwa sababu umemuona jilani yako ana gari. Ni vizuri sana uangalie mambo mbali mbali kabla hujaamua kuchukua aina flani ya gari, vitu vya msingi kijiuliza ni kama vile (unataka gari yenyewe 4WD, 2WD, ya juu juu au chini, yenye sun roof, yenye camera ya nyima, inayotumua upepo kwenye shock up au za kawaida, itakua inapita njia mbovu zaidi au ya lami, iwe ya aina gani ya mafuta, iwe imetembea kilomita ngapi, aina ya injini na ukubwa wake n.k ukiacha kununua gari kwa ushabiki utakua kwenye nafasi nzuri ya kukipenda chombo chako na kupatq kilicho sahihi ambacho hakitakupa tabu moyoni.

4. Chunguza bei za kuimiliki hiyo gari ya ndoto yako. Hapa usifike kwa muuzaji au muagizaji mmoja ukamalizana nae halafu baada ya siku 2 unakutana na gari kama hiyo inauzwa kwa bei chini zaidi na ambayo ina ubora kuliko hiyo uliyouziwa bila kutafiti bei kwanza. Hii itakusaidia kuokoa kiasi cha pesa na pia kupata kilicho bora zaidi.

5. Chagua aina tofauti zinazofanana ili kuzilinganisha. Unapopenda aina flani ya gari na kuamua kuchukua hiyo hiyo wakati mwingine hua inaleta maumivu pale unapogundua aina flani ya gari ni bora zaidi kuliko hiyo na uzuri zote zinalingana bei na mwonekano hazitofautiani sana. Hapa nazungumzia gari kama Toyota Allion Vs Premio, Toyota Allex Vs Run X, Alteza Vs Lexus IS 200, n.k

6. Chunguzq gari husika itakua ikigharim kiasi gani kwa mwezi na kwa mwaka. Kununua gari hua ni jambo jepesi, lakini wakati mwingine kuihudumia gari hua ni jambo gumu kidogo haswa kama huitumii vizuri gari hiyo kukuingizia pesa zitakazokua zikiwesha uihudumie na pia uweze kutekeleza majuk yako mengine. Hapa angalia gharama za Bima, Mkopo, Vibali, Usajili, Ushuru, Mafuta, Matengenezo, Dharula n.k

Zifuatazo ni baadhi ya aina za magari ambazo zinawafaa sana vijana au watu wa kipato cha kati.

Gari hizo ni Vitz, Raum, IST, Passo, Platz, Ractis, Fun Cargo, Porte, Bb, Sienta, Duet, Nissan Note, Nissan March, Honda Fit, Spacio, Carina T.I, Cami, Allex/ Run X, Allion, Premio n.k

Gari hizo hapo juu hutumia mafuta kidogo, matengenezo yake ni rahisi na vifaa vyake ni vingi hapa Tanzania.

Wasalaam

Kimomwe Motors Tanzania Limited- Waagizaji wa Magari toka Japan

0746267740
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom