Jamani Corona ipo na wala sio siri.
Leo nimepatwa na huzuni sana. Jana ilikuwa nilipwe deni langu na mtu ninayemdai na yeye alinapa ahadi ya uhakika ya kunilipa jana. Nikachukulia poa usiku nikamtex hakujibu. Leo najua naenda kukunja mshiko wangu nampigia simu inapokelewa na mdogo wake ananiambia mwenye simu amefariki alfajiri hapa natoka kuhifadhi mwili. Corona ipo jamani.
Una huzuni mtu kafariki au una huzuni hutalipwa deni?
 
Jamani Corona ipo na wala sio siri. Leo nimepatwa na huzuni sana. Jana ilikuwa nilipwe deni langu na mtu ninayemdai na yeye alinapa ahadi ya uhakika ya kunilipa jana. Nikachukulia poa usiku nikamtex hakujibu. Leo najua naenda kukunja mshiko wangu nampigia simu inapokelewa na mdogo wake ananiambia mwenye simu amefariki alfajiri hapa natoka kuhifadhi mwili. Corona ipo jamani.
Double blow (home and away). Deni na kupoteza rafiki.
 
Taifa letu limevamiwa na ugonjwa. Hata kama ni ugonjwa mpya lazima tusemezane. Watu wanakufa. Ndugu zetu wanakufa. Kuna kima atakuja na majibu ya kifedhuli kuwa kila siku watu wanakufa. Nini kimelikumba taifa letu Neumonia hii ni toleo gani? Maana kila siku huu ugonjwa upo. Mungu afanye maamuzi ya haraka juu ya watesi wetu. Japokuwa Afya ni jukumu letu lakini magonjwa ya mlipuko ni lazima Kiongozi Mkuu achukue jukumu la kutoa mwelekeo wa taifa. Tunajidanganya juu ya kufunga na kuomba. Acheni mchezo na afya zetu. TANZANIA INA CORONA NYINGI SANA.
 
Kwa wale Wakristu habari za Jumatano ya Majivu, kwa wengine habari za Great Thinkers

Niende kwenye mada yangu. Msingi wa hoja yangu unajikita katika mapambano ya ugonjwa wa covid 19.

1: Hatua za Kijamii

Kwa kweli hapa JF tumejitahidi kuishauri serikali kwa wazi kuwa itamke wazi kuwa Covid 19 imerudi, na hatua za kujikinga zakuvaa barakoa kwenye maofisi, taasisi za umma zitiliwe mkazo km kwanzia, kwenye mwendo kasi watu level sit na hivyo hivyo kwenye daladala, vitakasa mikono pamoja na kunawa mikono.

2: Maziko

Kwenye maziko km mhusika kafa kwa Covid 19 pia kuna hata ya familia yake ameambukiza hivyo kuwe nakutoshikana mikono pia kuwe na umbali katika misiba(social distance)

Nimehudhuria kanisa la Roma leo jtano ya majivu getini huingii km hauna barakoa pia lazima unawe na mnakaa umbali kati ya mtu na mtu binafsi naipongeza kanisa la Roma kuweka utaratibu kitaasisi.

3: Nashauri Serikali kuwa iwalinde Majenerali(Wababe wa vita na mbinu za medani wanazifahamu)

Hii kipengele cha tatu naiweka kwa upekee kabisa maana kwa sasa hivi vifo vya Mabrigedia zimekuwa kwa wingi na nimepenyezewa na watu wa ndani kuwa, taratibu za maziko yaani paredi zao zinaenda kwa rank (Mwili utabebwa na warank yako, sasa km amekufa kwa Covid na familia yake imeathirika ni wazi kuwa hawa wakuu wetu km wafariji wakwanza watachangamana, hivyo ni rahisi kupata maambukizi)...Vita hupiganwa kwanza mezani kabla ya medani sasa tuwalinde hawa majenerali ni lulu jeshini)

Hitimisho
Serikali kupitia waziri wa afya ituongoze kwenye hii vita, tuchukua hatua za kisayansi zaidi tuwape nafasi wataalam wa afya
 
Hii Hakuna takwimu na wanasema wameudhibiti ugonjwa. Lakini wachezaji 3wa Namungo wamekutwa na maambukizi Angola.
Mwl J.K.Nyerere RIP aliwahi kusema . matatizo huwezi yamaliza kwa kuyafumbia macho ukidhani yataondoka.

Ndio tunacho kiishi sasa hivi. kuna viongoz fulan wanafumbia macho hili suala wakidhani litaondoka bila jitihada zozote.
 
Tuko vizuri-.jpg
 
Ni masikitiko kuwa sasa habari za vifo zimeanza kuwaandama viongozi wa Ikulu

Ndani ya saa 24 viongozi wawili wa Ikulu za Tanzania wanaondoka hivi hivi,si hapo tuu watu mashuhuri na wanasiasa ndani ya wiki hii wameondoka hivi hivi bila serikali kuwa wazi nini kinapelekea hii hali kwa sasa

Tunaitaka serikali ijitokeze hadharani iwambie wananchi wake kinachoendelea kwenye hii nchi maana wamekuwa na kauli ya kupinga kuwa nchi hii haina corona

Nb,kama serikali mnaogopa kutangaza kuwa kuna korona nchini kwa kuhofia taharuki,hivyo vifo tu ni taharuki tayari
 
Back
Top Bottom