Hali inazidi kuwa Tete,tunarudi Kwa mwaka Jana

======
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaonesha Petroli imepanda kwa sh. 443 huku Dizeli ikipanda kwa 391 kwa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa sh. 2,736 imepanda hadi 3,199 huku Dezeli iliyokuwa inauzwa sh. 2,544 imepanda hadi 2,935, kwa Dar es Salaam bei ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano, Agosti 02,2023 saa 6:01 usiku.

Aidha EWURA imesema sababu za mabadiliko ya bei hizo kwa mwezi Agosti 2023 ni changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Imesema kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Tanga yatauzwa sh. 3,245 na Mtwara ni sh. 3,271.
Sasa ikifika kule Ngara siitauzwa 4000
 
Hapo kuna watu wanapata mabilioni ndani ya siku 1 maana kama mtu alikuwa na lita milioni 2 tayari faida kapata na hii ilitegemewa maana mafuta yalifichwa mapema mno, maana bei ilishajulikana itapanda
Mwezi unaokuja itapanda tena maana dollar itakuwa imefika 2700 hivyo lita itafika 3500 hadi mwaka uishe mafuta yatakuwa 4000 huko

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Walifungia stock ndio maana hapa katikati mafuta yalikuwa hadimu
 
Huu mlipuko wa bei ya mafuta unaenda kupandisha kila kitu, halafu mishahara ya watumishi imebaki ileile kiduchu.....nchi hii imeharibiwa sana na hawa wanasiasa wachumia tumbo wasiokuwa na vision wala ubunifu wowote, empty set!​
Wao wabunge wanazidi kuongezewa marupurupu ,si wasindikizaji tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom