Kupanda kwa bei za Mafuta, Serikali inadanganya

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.

Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.

Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).

Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta. Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;

Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha

Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.

Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.

Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.

Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.

Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.

Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.

Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.

Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.

Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.

1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.

(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.

(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.

2. Hatua za mahususi za kikodi

(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.

(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje

1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.

2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.

3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.

Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.

Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223
 
Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta
Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.

Kumekuwa na udanganyifu mwingi wa CCM na serikali zake kwa wananchi wake miaka yote tangu Uhuru,na nimekuwa nalisema hili siku zote.Hili swala la mafuta has proved my point.Halafu watu wanakuja eti serikali ya Samia nzuri,kama mazuzu hivii.......!

Lakini swala la serikali kutoa ruzuku kwa wananchi wake si baya.Binafsi ninachojiuliza ni kwa nini iondoe ruzuku hiyo na sasa?Ni adhabu kwa wananchi kwa kuwa wanapinga mkataba kati ya serikali na DP World au serikali haina fedha za kutekeleza zoezi hilo?Whatever the case may be,ni vema serikali ikawa wazi,iwaeleze wananchi kwa nini imeondoa ruzuku.

Kwa maelezo haya serikali kupitia kwa watendaji wake haijatimiza wajibu wake ipasavyo kwa uma,kwa hiyo nashauri wale wote walioshiriki katika kuwaletea wananchi adha hii,wachukuliwe hatua stahiki.

Mwisho,inashangaza kwamba kabla ya malumbano ya serikali na wananchi wake kuhusu mkataba wa DP World kwisha,serikali inaleta tena sintofahamu nyingine.Nini kinaendelea ni vigumu kujua,lakini inaelekea nia ni kuwaletea wananchi hofu ili iwe rahisi kuwa-manipulate na kuwaondoa kwenye mjadala wa DP World.Kama ndio hivyo,it is bad by any standard.Wananchi wanapaswa kujadili matatizo yao kwa kina,ili hatimaye wapate muafaka unaotekelezeka.Huku ni kuwahujumu Wananchi.
 
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.

Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.

Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).

Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta
Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;

Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha

Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.

Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.

Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.

Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.

Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.

Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.

Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.
Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.

Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.

1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.

(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.

(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.

2. Hatua za mahususi za kikodi

(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.

(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje

1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.

2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.

3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.

Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.

Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223
Hata tuseme vipi? Hakuna litakalo fanyika. Maana hata hawa wabunge wa mchongo wakitaka kulizungumzia bi betina atazuiaisizungumziwe kwa sababu mume ndie boss wa ewura.
Bado narudi kwa Mama, amekuwa akidanganywa na kubeba familia hata pale panapo onekana kutakuwa na conflict of interest ..
 
Swali rahisi Tu ..je nchi zote kuna ewura inayo tangaza bei?
Wenzetu kama Kenya na wengine wanafanyaje ?

The best solutions ni kuwa na kampuni moja kubwa ambayo ni public listed...

Sijaelewa hapo kwenye Kuwa na Kampuni moja kubwa Public listed,
Inakuwa na majukumu yapi?
Ya Ewura au Tpdc?
 
Yote kwa yote Serikali yetu ndiyo inayotutesa tangu na hadi leo hii, Nijuavyo mimi na elimu yangu ndogo Serikali kwa sasa inalipa deni lililosababishwa na Mwendazake tena inalipa deni hilo kwa fedha za kigeni ambazo ndizo tulizotegemea kununulia mafuta, deni ili ni lile la wale mabeberu walotushitaki. Si hayo tu, bado wapo wanaochuma chao mapema kwa ajiri ya mchakato wa uchaguzi wa 2025.
Mama naye amewafumbia macho wafanyabiashara wale kwa urefu wa kamba zao! Kuna timu za kina Mwiguru na Makamba!
 
Kumekuwa na udanganyifu mwingi wa CCM na serikali zake kwa wananchi miaka yote tangu uhuru,na nimekuwa nalisema hili siku zote.Hili swala la mafuta has proved my point.

Lakini swala la serikali kutoa ruzuku kwa wananchi wake si baya.Binafsi ninachojiuliza ni kwa nini iondoe ruzuku hiyo na sasa?Ni adhabu kwa wananchi kwa kuwa wanapinga mkataba kati ya serikali na DP World au serikali haina fedha za kuutekeleza zoezi hilo?Whatever the case may be,ni vema serikali ikawa wazi,iwaeleze wananchi kwa nini imeondoa hiyo ruzuku.

Mwisho,kwa maelezo haya serikali kupitia kwa watendaji wake haijatimiza wajibu wake ipasavyo kwa uma,kwa hiyo nashauri wale wote walioshirika katika kuwaletea wananchi adha hii wachukuliwe hatua stahiki.
Utawachukulia hatua JK na Rostam? labda kama hujipendi
 
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.

Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.

Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).

Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta
Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;

Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha

Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.

Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.

Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.

Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.

Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.

Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.

Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.
Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.

Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.

1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.

(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.

(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.

2. Hatua za mahususi za kikodi

(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.

(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje

1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.

2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.

3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.

Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.

Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223
ACT HOJA no 1, ni Bandari🙏🙏
 
Yote kwa yote Serikali yetu ndiyo inayotutesa tangu na hadi leo hii, Nijuavyo mimi na elimu yangu ndogo Serikali kwa sasa inalipa deni lililosababishwa na Mwendazake tena inalipa deni hilo kwa fedha za kigeni ambazo ndizo tulizotegemea kununulia mafuta, deni ili ni lile la wale mabeberu walotushitaki. Si hayo tu, bado wapo wanaochuma chao mapema kwa ajiri ya mchakato wa uchaguzi wa 2025.
Mama naye amewafumbia macho wafanyabiashara wale kwa urefu wa kamba zao! Kuna timu za kina Mwiguru na Makamba!
Maza hajui hata kinachoendelea
 
Kalemani hakuwa na tatizo lolote alikuwa mfuatiliaji mzuri sn bahati mbaya alikuwa adui wa mafisadi
Hata huyo nae mwizi,ana kampuni ndogo ndogo huko kwenye ujenzi wa reli,ile wizara ilimfaa sana profesa muhongo lkn si marope au makamba,kwanza wote wana tamaa ya urithi,kipindi cha jiwe kalemani alikua anajipanga awe mrithi wa jiwe na ndivyo ilivyo kwa feb
 
Kiukweli siwezi soma li post lirefu hivi ila nadhani mfumuko wa Bei ya mafuta haupo Tanzania tu
 
Hata huyo nae mwizi,ana kampuni ndogo ndogo huko kwenye ujenzi wa reli,ile wizara ilimfaa sana profesa muhongo lkn si marope au makamba,kwanza wote wana tamaa ya urithi,kipindi cha jiwe kalemani alikua anajipanga awe mrithi wa jiwe na ndivyo ilivyo kwa feb
Lakini alikuwa na nafuu ila siyo huyu Makamba kazidi asee
 
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.

Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.

Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).

Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta. Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;

Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha

Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.

Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.

Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.

Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.

Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.

Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.

Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.

Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.

Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.

1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.

(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.

(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.

2. Hatua za mahususi za kikodi

(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.

(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje

1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.

2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.

3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.

Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.

Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223
Hii nchi inajimaliza kwa kuendekeza sifa na ufisadi
 
Back
Top Bottom