ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Hali inazidi kuwa Tete,tunarudi Kwa mwaka Jana

======
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaonesha Petroli imepanda kwa sh. 443 huku Dizeli ikipanda kwa 391 kwa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa sh. 2,736 imepanda hadi 3,199 huku Dezeli iliyokuwa inauzwa sh. 2,544 imepanda hadi 2,935, kwa Dar es Salaam bei ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano, Agosti 02,2023 saa 6:01 usiku.

Aidha EWURA imesema sababu za mabadiliko ya bei hizo kwa mwezi Agosti 2023 ni changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Imesema kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Tanga yatauzwa sh. 3,245 na Mtwara ni sh. 3,271.
 

Attachments

  • Cap_Prices_for_Petroleum_Products_wef_2nd_August_2023_Kiswahili (1).pdf
    274.9 KB · Views: 13

Similar Discussions

Back
Top Bottom