Status
Not open for further replies.
Kama ni kweli Serikali imetumia usalama kugushi makaratasi ya uchaguzi, kupanga matokeo ya uchaguzi Tanzania nzima na kufilisi wapinzani wafanyabiashara na hata kuwajeruhi au kushiriki kwa namna yeyote kwenye mauaji ya wapinzani ni tishio kubwa sio tu kwasasa lakini kwa miaka mingi sana ijayo.

Tatizo kubwa kuna watu wanafikiri hili ni jambo la mpito tu lakini ukweli ni kwamba usalama wa taifa umejipa kazi isiyo ya kwao. Hiki kitengo hakitakuwa cha awamu moja maana ukisha onjesha madaraka makubwa hivi kwa idara moja haina tofauti sana na nchi kutawaliwa kijeshi.

Je hii ina maana gani? Hii ina maana kwamba usalama unakuwa na nguvu kuliko wananchi hivyo hakutakuwa na sababu ya wagombea wa nafasi tofauti kuwafuata wananchi badala yake wanaweza kuwafuata viongozi wa chama na usalama pekee kwani ndiyo wachaguaji wa ukweli sio wananchi. Lakini la pili kwenye hili ni kwamba usalama utakuwa na nguvu ya kutishia bunge zima hadi mawaziri.

Kwa wale washabiki hasa wenye elimu inaelekea wanashabikia kitu ambacho hawajui au wamejidanganya kwasababu tu wanampenda Magufuli na mambo anayofanya. Hili sio sawa maana bila mfumo mzuri wa kidemokrasia tunaweza kuwa na Raisi mbaya na hatutaweza kumtoa kwa namna yeyote. Lakini vilevile unaweza ukawa na viongozi wabaya usalama wenye malengo binafsi na wakamtisha mpaka raisi wa nchi maana serikali imewapa vitu na uwezo ambao hawatakiwi kuwa nao. Hatuwezi kukaa na kusali tu nkwamba kila siku tutapata watu bora kwenye hizi idara au hata Uraisi hivyo mnaoshangilia sana mjue mabadiliko haya makubwa inawezekana kabisa akapewa kiongozi ambaye si mzalendo na nchi yetu inaweza kurudi nyuma kwa miaka mingi bila na kuwa na sheria yeyote ya kumtoa.

Umri wa kati wa Watanzania ni miaka 17-18 tu hivyo Tanzania ina watoto wengi ambao hawawezi kugoma, kuandamana wala kuelewa mambo mengi kwa upana na wale wachache wanaoelewa wamekuwa vipofu kwa manufaa binafsi au kwa mapenzi yao. Binadamu ni kama maua yenye harufu nzuri mwisho wake yanaharibika hata yawe mazuri vipi. Hii ndiyo sababu pekee pamoja na mapenzi yangu binafsi kwa Magufuli jinsi alivyobadilisha siasa hasa kwa upinzani na CCM ilivyoshinda kwa kutumia usalama imeweka pengo kubwa ambalo itakuwa ngumu kuziba.

Quote Reply
Select for moderation Report Edit


Remove formattingBoldItalicFont sizeText colorMore options…
ListAlignment
  • Align left
  • Align center
  • Align right
  • Justify text
Paragraph format
Insert linkInsert imageSmiliesMediaQuoteInsert tableMore options…
UndoRedoToggle BB codeDrafts
Preview

Font familyStrike-throughUnderlineInline codeInline spoiler
Insert horizontal lineInsert videoSpoilerCodeSubscriptSuperscript

Write your reply...
Post reply

Attach files Insert quotes…
Similar Discussions

Who Read This Thread (Total Members: 4)​

Share:
FacebookTwitterRedditWhatsAppEmailLink


KEdit

Kamundu

JF-Expert Member
Messages3,799Reaction score3,605Trophy points2,000


WHO WE ARE​

JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.
You are always welcome!
Read more...

WHERE ARE WE?​

We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.
For anything related to this site please Contact us.
Contact us now...

DISCLAIMER​

JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..
Read more...

FORUM RULES​

JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.
You MUST read them and comply accordingly.
Read more...

PRIVACY POLICY​

We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.
Read our Privacy Policy.
Proceed here...

Connect with us​

Facebook Twitter Instagram Telegram Contact us RSS


TopBottom
 
Uchaguzi umeisha Serikali imeanza kuundwa na hivi karibuni Baraza litaundwa. Kwa maoni yako ni mambo gani ungeshauri Serikali ya Dkt. Magufuli ifanye kiuchumi, kisiasa na kijamii?
 
Apandishe madaraja kwa watumishi, atengeneze mazingira rafiki kwa wawekezaji, ushirikiano wa kimataifa na Haki na utu uwepo miongoni mwa wananchi ili kuleta umoja wa kitaifa, nafikiri itasaidia kuleta maendeleo ya pamoja
 
Kwani walishauriwa na nani kuiba kura na kumwaga damu? Nendeni kwenye mabaraza ya ccm mkachukue ushauri. Mngekuwa mmeingia kwa ridhaa ya wananchi walio wengi, hapo mngekuwa na uhalali wa kuomba maoni.
 
1. Ahuishe na kuipa nguvu sekta binafsi maana ndo imeshikilia uchumi wa nchi.

2. Afumue na kuunda upya mifumo ya ukusanyaji Kodi wa TRA....hii iliyopo Sasa ni ya hovyo sana.

Mambo ya kufutiana leseni za biashara kisa kuchelewa kulipa Kodi ni uonevu mkubwa.

3. Aache kuongoza nchi kivyake vyake tu kwa kuamini kuwa yeye pekee ndio anaweza Kusimamia Mambo yote na yakaenda (perfection syndrome) Bali afuate katiba na sheria za uongozi .

4. Awamu hii apunguze au aache kabisa kutumbua tumbua watu aliowateua yeye mwenyewe maana kuendelea kufanya hivyo kunadhihirisha kwamba huwa hayupo makini kufanya"vetting" hivyo teuzi zake nyingi ni za kukurupuka.

5. Aajiri kada zote na sio kupendelea tu waalimu na madaktari.

6. Apandishe watumishi madaraja na kuwapa nyongeza stahiki za mishahara Kama sheria ya utumishi wa umma inavyosema.

7.Bunge lirushwe live Kama zamani ili wanachi wapate fursa ya kuona jitihada za wawakilishi wao.

8. Atafute mbinu mpya za kurudisha mahusiano mazuri na nchi zingine....maana hivisasa TANZANIA ni Kama mtoto wa kambo.

9. Asianzishe miradi mingine mipya isiyo na ulazima sana Bali ajikite katika kumalizia miradi aliyokwisha ianzisha na kuboresha miradi iliyo kuepo kabla.

Don't take it too personal....
 
Uchaguzi umeisha serikali imeanza kuundwa na hivi karibuni Baraza litaundwa’Kwa Maori yako ni mambo gani ungeshauri serikali ya Dr magufuli ifanye KIUCHUMI kisiasa na kijamii
Atofautishe kusifiwa kinafiki na kutiwa moyo, kwa taarifa tu anasemwa vibaya sana kuliko kawaida, wanamuombea amalize muda wake haraka aondoke hivyo ajitafakari sana sana, kiuchumi ajiangalie nchi itaporomoka ajiandae kisaikolojia.
 
Sekta binafsi.

Sheria za TRA zifumuliwe ili ziendane na azma ya kuinua sekta binafsi na uchumi.

Miradi ya umeme,viwanja vya ndege,SGR iishie makutupora na Mza Isaka basi mwingine ataendeleza,ndege ya mizigo muhimu,madaraja ya vielelezo i.e Busisi.

Mishahara kwa watumishi
 
Atoe ajira za ualimu kwa wingi ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wanafunzi mashuleni!
Kwa bahati mbaya hii ni ndoto,,, magufuli awezi kufanya ujinga huu. Wanafunzi wa sasa wanauelewa mkubwa sana rejea matokeo ya hivi karibuni.

Hakuna haja ya kuajiri walimu kabisa tena ikiwezekana wapunguzwe maana ni wengi sana. Kutakua na ajira za muda za kusimamia mitahani kama ifanyikavyo tume ya uchaguzi.
 
Uchaguzi umeisha serikali imeanza kuundwa na hivi karibuni Baraza litaundwa’Kwa Maori yako ni mambo gani ungeshauri serikali ya Dr magufuli ifanye KIUCHUMI kisiasa na kijamii
Aliishakataa kupangiwa, na ukipanga ndio unaharibu kabisaaa
 
Alegeze sana uingizaji wa mitaji kutoka kokote kule, hasa mitaji inayolenga kuwekezwa kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidha aina yeyote ile.
 
"Mimi ukinishauri ndio umeharibu kabisa maana sitofanya unachonishauri".

JOHN POMBE MAGUFULI.

"Hakuna aliyenishauri kuchukua fomu nilikwenda mimi mwenyewe kwahiyo sitaki ushauri".
JONH POMBE MAGUFULI.

"Mimi HUWA SIPANGIWI"

JOHN POMBE MAGUFULI HATAKI NA HAPENDI USHAURI WENU.
Utawala wa kishetani.
Maguful.jpg
 
Apitie ilani za vyama vingine na yaliyoainishwa mazuri ayachukuwe na kuyatekeleza,

Kwenye Serikali yake aendelee kushirikisha baadhi ya viongozi wa upinzani ili kuongeza maridhiano,

Mahusiano ya kimataifa yaangaliwe upya
 
Katiba mpya ya tume ya warioba ni muhimu kuliko mambo yote kwa kizazi chetu cha vijana maana tunataka maisha tofauti na katiba ya 1964 na 1977
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom