Lucy Joseph

Member
Sep 20, 2020
38
95
Kwanza nianze kwa pongezi nyingi kwa Rais wangu, mambo uliyoyafnya ndani ya miaka mitano kwetu sisi wa TANZANIA tunasema ni Maajabu, umetuheshimisha wa Tanzania leo hii tunatajwa duniani kutokana na msimamo wako mzuri kipindi cha ugonjwa wa Corona, mataifa makubwa mpaka leo wanahangaika lakini sisi tukasimama na mungu na isingekuwa wewe haya yote yasingetokea.

Lakini pia katika uongozi wako umejitahidi kupita kila sehemu, kila sekta Tanzania nzima ili kuhakikisha mambo yanakaa sawa ,hongera sana lakini pia tunakushukuru mnooo...Zawadi yetu sisi wa Tanzania ni kwenda kukupigia kura tena za kishindo siku ya Tarehe 28/10/2020.

Mwisho, nimalizie kwa kusema kuongoza nchi sio kazi nyepesi, na mafanikio hayaji kwa kubahatisha lazima pawepo na mipango.
Lakini pia changamoto hazikosekani ,nini kifanyike kwetu sisi?
>Tumpe ushirikiano wa kutosha kwa Rais wetu pamoja na viongozi wake wote.
>Na tumpigie kura za kutosha ili akamalizie yale mambo ambayo ameyaanzisha
IMG_20201009_121222_150.jpg
 
Lucy Joseph

Member
Sep 20, 2020
38
95
Kama unahoja ziwasilishe lakini usiingiziee na uongo kuharibu akili za watu, wapi huko watu wanachapwa bakora, Tanzania hii au
 
Plant

New Member
Sep 11, 2020
4
45
Utitili wa Flyover uliotajwa na mheshiwa pale kwa mkapa....hivi 2025 dar itaonekanaje...Hebu uchaguzi uishe Rais Aapishe ili ulaya ihamie dar
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,157
2,000
Ungemuomba atumie nguvu yake kusimamia haki

Mbagala wameporwa mbunge wao..

Kuna uchaguzi wa mameya wa majiji...asimamie haki walioshinda ndo wapewe

yasije rudia ya manispaa ya Arusha mjini kuhusu uchaguzi wa meya hasa hapa Dar
Well said!
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,157
2,000
Mheshimiwa kasema hataki vitu vya kupangiwa. Mimi ni nani nimshauri mheshimiwa anayejua kila kitu.
 
SHUJAA MKUU

Member
May 22, 2014
32
95
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.
Mimi ushauri wangu mheshimiwa Rais nchi yetu sasa hivi upo mgawanyiko mkubwa Sana. Ameanza na kuunda kamati za amani ili amani iwepo. Tunaomba aunde kamati zitakazo toa elimu ya uzalendo ilk watu wapende nchi yao. Kizazi kilichopo sasa hakijui tilipotoka wanapotokea matapeli wa kuhujumu uchumi wanabebwa tu.
 
Abraham2020

Member
Oct 8, 2020
16
45
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.
Maoni haya umeyachukua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom