Hongera sana mama kizuri Huwa kinajiuza.

Tanzania sasa ni namba moja duniani kwa furaha ya watu wake

Demokrasia nchini imepanuka hata kila mtu anatukana lakini hakuna anayemkamata

Sekta Binafsi imekua na pesa mtaani zimejaa.

Ajira kila Kona zimejaa
Ziko wapi dolla?
 
Rais huyu kiboko kila Kona anaongelewa yeye tu as if Marais wengine hawajawahi kufanya chochote na ni kama nchi imepata uhuru juzi tu.

Hivi Samia amefanya nini kuteka nyoyo za Watanzania?
 
Futa, ondoa🤣🤣🤣😂😂uliwaza nini mpendwa kwamba hakukuwa na lolote lililokufurahisha alofanya? Ungeshauri hata vingine vya kuendeleza alivyoviacha mpendwa
 
Kuna kanuni inasema katika maisha tunatofautiana kwa mambo mengi lakini ni muhimu kukubali kuto kukubaliana.

Kwenye eneo hilo awamu hii imefauru kwa asilimia kubwa nadhani zaidi ya asilimia 90.

Tatizo ninaloliona ni ngazi za makao makuu ndiyo kikwazo hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.

Leo kuna idara zinasubiri maamuzi ya makao makuu na ukimya huo unakwamisha kazi zote.

Kuna Idara hata kudhibitisha malipo ya haki ya wafanyakazi yanakwamishwa na Makao makuu kwa utashi binafsi.

Leo imefikia hatua ya kuwaongezea wastaafu mikataba isiyo na tija kwasababu binafsi wala siyo kwa ajili ya kuboresha utumishi wa umma. Pesa hizo zingetumika kuajiri watumishi wapya na wenye nguvu.
 
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kufunga ramadhani

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kumuamkia babangu leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuvuka barabara ya Manzese leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kupiga pasi nguo zangu za kuvaa leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuandika maneno haya

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuiona tena ramadhani na kufunga

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuamka kula Daku leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuelewana na mke wangu

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuwa hai mpaka leo

Hapo vipi niendelee kumshukuru
Au ni ishie hapo
 
Namshukuru mueshimiwa sana Raisi nimeweza kujiunga bando la buku jero airtel.
Namshukuru tena nimeweza kunywa supu ya buku na mihogo ya mia nne na pilipili ya kupikwa.
 
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kufunga ramadhani

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kumuamkia babangu leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuvuka barabara ya Manzese leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kupiga pasi nguo zangu za kuvaa leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuandika maneno haya

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuiona tena ramadhani na kufunga

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuamka kula Daku leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuelewana na mke wangu

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuwa hai mpaka leo

Hapo vipi niendelee kumshukuru
Au ni ishie hapo
Aiseeee hii kali sana 🤣
 
Back
Top Bottom