Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kufunga ramadhani

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kumuamkia babangu leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuvuka barabara ya Manzese leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kupiga pasi nguo zangu za kuvaa leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuandika maneno haya

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuiona tena ramadhani na kufunga

Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuamka kula Daku leo

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuelewana na mke wangu

Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuwa hai mpaka leo

Hapo vipi niendelee kumshukuru
Au ni ishie hapo
namshukuru sana na kumpongeza kwa kikokotoo kitakachotuuumiza uzeeni nguvu zetu zitakapoisha.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika maeneo yote nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Mwenyekiti Chatanda amesema kuwa kupitia Ziara ya iliyofanywa na viongozi wa UWT Taifa katika mikoa 17 imejionea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika Kongamano la Kumshukuru Rais Samia lililofanyika Machi 26, 2024 katika ukumbi wa Mkuki jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Chatanda amesema

“Utendaji bora wa kazi wa Rais Samia ambae pia ni Mwenyekiti wetu wa CCM unadhihirisha uwezo wa Mwanamke kuongoza,kwani miradi mbalimbali ya maendeleo imeendelea kutekelezwa na hakuna miradi ya kimkakati aliyoikuata iliyosimama” Alisema Mwenyekiti Chatanda na kuongeza

"tumeweza kufanya ziara katika Mikoa 17, Wilaya 84, Kata 854 na kuweza kufanya mikutano ya hadhara 854, Mikutano ya ndani 35, Mikutano ya kwenye miradi 320 na kufanya jumla ya mikutano 1,209, niwaombe viongozi wa CCM na Serikali kwenda kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yenu ili wananchi wapewe huduma kwa wakati sahihi."

#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee
 

Attachments

  • VID-20240329-WA0053.mp4
    37.4 MB
Acha mikwara wewe, mama Samia ndiye amiri jeshi mkuu sasa hivi, na ataongoza nchi kadri kwa style yake sio lazima amuige Magufuli, Magufuli ameshakufa.

Magufuli ali reverse vitu vingi vya Kikwete tu alivyoona havipo sawa, Mwinyi pia ali reverse vingi vya Nyerere ambavyo aliamini havipo sawa, Mkapa hivyo hivyo, Kikwete n.k
Uliyempongeza umeona alikoifikisha nchi?
Haya endelea tena kumpongeza
 
Mimi ni msomi wa ulaya wa International Development . Namkubali Sana Mama
Ushauri wangu kwa Her Excellency Dr Samia ni Kama ifuatavyo:

1. Kujenga vyanzo vingi vya umeme, umeme mwingi wa uhakika utaamsha private sector hasa viwanda na wajasiriamali wadogo na kupunguza unemployment. Pia foreign investors watakuja wenyewe kwa wingi na kuongeza revenue ambayo itatumika kuongeza vyanzo vya maji na kilimo cha umwagiliaji.

2. Kujenga reli ya SGR Dar to Mwanza - Musoma hadi Kagera na Kigoma.
Reli ya umeme itaongeza mizigo ya nchi jirani na kuongeza mapato ya reli na bandari na kampuni za clearing and forwarding. Pia mapato makubwa yanaweza kupunguza kodi kwa raia masikini

3. Kuongeza ununuzi wa ndege za abiria na mizigo, wageni wataongezeka na kukuza utalii na uwekezaji wa mizigo na mitaji toka nje na kuongeza upatikanaji wa pesa za kigeni zitakuja kwa wingi

4. Kubadili teaching language kutoka kiswahili hadi English kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Huu ni mwiba mchungu ila maendeleo ya nchi hutegemea jinsi inashirikiana na nchi zingine, kwasasa Tanzania ni kisiwa, watanzania wengi hawapati fursa za mitaji toka nje au kwenda nje kufanya kazi na kuongeza remittance sababu hawajui kuongea kiingereza fasaha. Ni vizuri tuige mambo mazuri kama Kenya wanatuacha kiuchumi sababu wageni hupenda zaidi kuwekeza Kenya kwenye ukame kisa ni mawasiliano tu na wakenya kwa lugha ya kiingereza. Kiswahili ni lugha yetu haitopotea maana tunaongea nyumbani huko shule iwe English na miaka kumi tu matokeo tutayaona. Mfano uko wazi watoto wa English Academy wanaotumia Cambridge curriculum wana akili kuliko St Kayumba!

Ukiangalia kwa makini Royal Tour movie utaona kitabia Mama Samia ni mzungu kabisa, na wazungu wako dynamic, hawakai na mila za kizamani zinazokwamisha maendeleo ya nchi, ukweli kuendelea kufundisha kiswahili shuleni kwa nchi masikini ni kuendelea kuididimiza nchi, English speaking society will open up new avenues for international transfer of capital and technology and ultimately bring rapid economic growth and happiness to the entire population. Hili nina uhakika nalo. Wazee wabaki na kiswahili chao nyumbani watoto wapige English shuleni na kazini wapate maendeleo. Hii inaitwa Paradigm shift, imetokea nchi nyingi kama Japan, UAE na Singapore, huwa ni maamuzi ya mtu mmoja tu nchi nzima inahama na kuachana na umaskini mazima

5. Kuondoa bureaucracy na udanganyifu kwenye mikopo ya halmashauri ambako kuna uhuni mwingi toka kwa watendaji wanaosimamia mchakato wa vikundi vya wajasiriamali vianzishwe na kupeleka maombi na hakuna mikopo inayotolewa. Hili ni Jipu , tume iundwe kuchunguza halmashauri zote mikopo inapoenda maana vikundi havipewi na pesa inatoka

Yakifanyika haya hakuna haja ya kupiga kampeni!!!

All the best Mama Samia
 
Bahati nzuri tuna demokrasia na kila mtu anauwezo wa kutukana au kutoa maoni bila kuhofia mtu yeyote tofauti ni enzi zile za Giza ambapo hata ukila kw amama ntilie unaogopa kuongea.

Mama amebkish swala moja tu la umeme nchi iwe paradiso. Pesa zipo za kumwaga ukiamua kufanya kazi yoyote inalipa
 
Bahati nzuri tuna demokrasia na kila mtu anauwezo wa kutukana au kutoa maoni bila kuhofia mtu yeyote tofauti ni enzi zile za Giza ambapo hata ukila kw amama ntilie unaogopa kuongea.

Mama amebkish swala moja tu la umeme nchi iwe paradiso. Pesa zipo za kumwaga ukiamua kufanya kazi yoyote inalipa
Pesa ni ya kumwaga kazi yoyote inalipa? Sijui research yako umefanya wapi, pls rudi kitaa upya uyaone maisha
 
Japo yanapanda ila yanapatika kama Samia leo hii hata humu msingefika kazini tunamshukuru Rais kwa kutuheshimisha

Asante rais Samia mafuta yapo kwenye bei stahiki na elekezi nani kama mama?Mama hoyeeeee mitano tena

Katiba ibadilishwe rais samia atawale hadi 2080 anaupiga mwingi sana uchumi umekua mama kafungua nchi kila mtanzania anafurahia hakika kama sio mama watz tusingekua hai mama hoyeeee
 
Back
Top Bottom