BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120

Serikali imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na mawe kutoka mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara, ambapo imesema hadi kufikiasaa 6:00 mchana leo December 08,2023 idadi ya vifo imefikia 80 (Watu wazima ni 48 wakiwemo Wanaume 19 na Wanawake 29) na Watoto ni 32 (wakiwemo wa kiume 15 na wa kike 17).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali akiongea leo Katesh, Hanang, Manyara amesema “Mwili mmoja wa Mtoto wa kiume ambao ulikuwa haujatambuliwa hadi jana sasa umetambuliwa lakini kuna mwili wa Mwananke mmoja Mtu mzima uliopatikana leo ambao bado haujatambuliwa, hivyo jumla ya maiti zilizokwishatambuliwa hadi sasa ni 79.

”Kwa jumla hadi kufikia saa 6:00 mchana leo, idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali zetu Mkoani Manyara ilifikia 133 (Watu wazima 71 na Watoto 62, kwa mujibu wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waathirika wote wanatibiwa bure na pia serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote”.


===========
MANYARA: Idadi ya Watu waliopoteza maisha kutokana na Mafuriko yaliyosababishwa na Mvua zilizonyesha kuanzia Desemba 2 huko Hananga imefikia 47 na Majeruhi 85

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Mvua hizo zimeathiri Miundombinu ikiwemo kuvunja baadhi ya Nyumba, kukata Mawasiliano ya Barabara na Umeme.

============

===========

Watu watano wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa wilayani Hanang mkoani Manyara baada ya mvua iliyonyesha usiku wa Desemba 2, 2023 kusababisha mafuriko.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Desemba 3, 2023 amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na madhara katika mali za watu.

Fuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi na tovuti kwa taarifa zaidi

--

UPDATE: WALIOFARIKI DUNIA WAFIKIA 17

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema Watu 17 wamefariki dunia katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kufuatia mafuriko yaliyoambatana na mawe makubwa na miti kuingia katika makazi ya Watu ambapo imepelekea nyumba kadhaa kuanguka.

“Leo asubuhi tumepata changamoto hapa Hanang toka jana usiku zilikuwa zikinyesha mvua za kawaida lakini maji yakawa yameporomoka kutoka Mlima Hanang yakiwa na mawe na miti kuja katika Mji wa Kateshi yakiwa na nguvu, ambapo mpaka sasa tumepata vifo vya Watu 17 pamoja na majeruhi ambapo maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Tumaini lakini pia uharibifu wa miundombinu ya barabara kati ya Sindiga na Babati yamesimama kwa muda ila TANROADs na TARURA wapo hapa kuhakikisha mawasiliano yanarejea”

“Pia niwaombe Wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati jitihada za uokoaji zikiendelea”

====

HANANG, Manyara: At least 20 people have been confirmed dead and several others missing following heavy rains that triggered flash floods in northeastern town of Hanang in Manyara region on Sunday.

Manyara Regional Commissioner, Queen Sendiga, confirmed the incident, saying 70 people have suffered minor and serious injuries. The leader described the incident as “fatality and a tragedy” in the region.

Sendiga said the rescue teams were swiftly deployed to the affected areas to provide support and aid in the search for the missing.

==============
Snapinsta.app_407756995_896597195156626_357921907578162516_n_1080.jpg
WALIOFARIKI WAFIKIA 49
MAAFA HANANG | Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, wilayani Hanang imeongezeka na kufikia watu 49 baada ya kupatikana miili miwili wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga aliyotoa asubuhi ya leo Disemba 4, 2023 inasema idadi ya majeruhi bado ni 85.

Ameongeza kuwa shule za msingi Katesh, Hanang na Dumanang zitatumika katika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo, na kuwataka wananchi kuhama mara moja maeneo ya hatari ili kujikinga na madhara mengine yanayoweza kutokea.

MANYARA: IDADI YA WALIOFARIKI KWA MAFURIKO YAFIKA 63, MAJERUHI 116

Idadi ya Watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, Wilayani Hanang imeongezeka na kufikia 63 baada ya kupatikana miili zaidi wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea

Waziri Mkuu Kassim Majalia amesema maporomoko ya udongo yamechangia athari kuwa kubwa.

Pia soma; Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang
Snapinsta.app_407756995_896597195156626_357921907578162516_n_1080.jpg
 
Mlima hanang unashusha mafuriko ya matope, katesh inafunikwa.

Inahisiwa kwamba crater ya juu ya mlima imezidiwa na maji na kupasuka.

Video hapa chini ni karibu na stendi ya katesh.
 
Back
Top Bottom