Watumishi TFS Manyara walitakiwa wawe nyuma ya nondo. Waligundua hatari wakakaa kimya hadi maafa yametokea

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,811
Ukimsikiliza huyu Jamaa unaona kabisa anakera na kutia hasira na Yuko comfortable kabisa kusimulia ujinga.

Yaani watu waligundua kabisa tena baada ya kupewa taarifa na wenyeji kwamba kuna hatari ya Maporomoko ya udongo Toka mwaka Jana ila wakakausha Hadi Maafa yametokea halafu ndio anasimulia.

View: https://www.instagram.com/reel/C0gAxG-IplY/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==

Hii Nchi tutaendelea kupata hasara ya maisha, Mali nk kama tutaendelea kuchekeana Kwa uzembe wa namna hii.

Aisee washukuru Mimi sio Rais, saa hii mngekuwa nyuma ya nondo Kwa Mashtaka ya mauaji.

Pia soma> Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63

@Mods,Kwa nini mumeondoa video niliyoambatanisha kutoka kwenye interview ya Mwandishi wa Clouds aliyeko site?

Na Mbaya zaidi mumewasiliana na watu wa clouds wamefuta hiyo video.

The moments naiweka hapa ilishakiwa na wachangiaji 180 wakilaumu Mamlaka(TFS) kwamba kumbe walijua ila Wakakausha.

Kwa staili hii,Je jf inaaminiwa kweli?

View: https://www.instagram.com/p/C0eSITSoaE2/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==
 
Hasira za bure tu.

Hata kama wangeambiwa kwamba kuna hatari bado wangebakia hapo hapo kwa kigezo kwamba wao ni wenyeji wa siku nyingi hapo na hukujawahi kutokea shida.

Kisarawe pale Msitu wa Kazimzumbwi tope lilimeguka na kufunga barabara ya Kisarawe-Dar Es Salaam

Cha msingi wananchi wawe macho na miinuko.

Hii ni Elinino haiitanii, ni vurugu mechi
 
Acha kutetea ujinga,watu dizaini Yako ningewaahikisha adabu Ili wengine wajifunze.

Nyie ndio mumesababisha hasara ya pale Jangwani
 
Acha kutetea ujinga,watu dizaini Yako ningewaahikisha adabu Ili wengine wajifunze.

Nyie ndio mumesababisha hasara ya pale Jangwani
Uzuri au ubaya anayeathirika ni mwananchi ambaye ameshapewa tahadhari.

Ipo miinuko sehemu nyingi sana. Hivyo inawapasa watu wachukue hatua kwa uzoefu wa huko Hanang' ili kuepuka madhara zaidi.

Bado mvua ina miezi minne ya kunyesha, yaani inakoma Aprili-Mei huko.
 
Back
Top Bottom