Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Jana Rais Samia Suluhu aliwasili mjini Dodoma na leo atawaapisha makatibu tawala aliowateua Mei 29, 2021. Pia Rais Samia aliwateua William Erio kuwa Afisa mtendaji mkuu wa FCC na Dkt. John Mduma kuwa mkurugenzi mkuu wa WCF. Kuwa nami.
==========
Tulia Ackson: Wanawake hamkuteuliwa kwakuwa ni Wanawake, bali kwakuwa mna uwezo wa kuongoza
Tunakupongeza sana Rais kwa kuendelea kutoa fursa kwa wanawake. Makatibu tawala wamefikia asilimia 40. Upande wa mahakama wa rufani, wanawake wamekuwa wengi. Bungeni tuko karibu asilimia 36 na Rais amechukua asilimia 21 amewapa uwaziri- Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge
Ninaamini wanawake mmeteuliwa si kwa sababu ni wanawake lakini mna uwezo wa kuongoza hivyo nendeni mkatumike kwa uadilidu na bidii- Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge
Rais Samia Suluhu amekamilisha zoezi la kuwaapisha makatibu tawala na sasa ni kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa Umma kinachoongozwa na Jaji.
"Kwenye ukusanyaji wa mapato fanyeni ‘Enforcement of Law’ Sheria zipo zinazoelekeza ukusanyajji wa mapato kwenye maeneo yenu, zifateni sheria msiende kufuata vifua vyenu na mioyo yenu.”
“Lakini pia kuna uzembe mkubwa, ukipitia mafaili ya utumishi watu wanajifanyia wanavyotaka, akipewa adhabu na utumishi anakata rufaa, sasa nitakapopokea tena rufaa za namna hiyo mimi na ninyi,”
Ma-RAS na Ma-RC Wanawake Mushirikiane
Rais Samia amesema ameteua wanawake asilimia 46% katika nafasi za Katibu Tawala wa Mikoa kwa sababu anaamini wanawake wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi kuliko wanaume. Amewataka walioteuliwa kuwatumikia na kuwaheshimu wananchi kuthibitisha imani hiyo.
“Nimewaweka Wanawake 46% ktk uteuzi nafasi za Makatibu Tawala wa Mikoa ili mkafanye kazi na tuone mabadiliko sasa walipokuwa Ma-RAS wengi Wanaume na sasa hivi mko Karibu sawasawa, msipofanya vizuri huko mbele tutaona cha kufanya”
"Ile mikoa ambayo kuna wanawake kwa wanawake, ile bibi usinibabaishe nisije nikaisikia, pale nyinyi sio wanawake ni RC na RAS mkifanya hivyo mnanitia aibu mimi,maana yatakayosemwa tulijua tu, mbona mnaolewa wawili mnakaa pamoja"
"Why [kwanini] msikae pamoja, mbona mnaolewa wawili mnakaa pamoja?"
"Muende mkachape kazi wanawake kwa wanawake, hiyo mikoa naitegemea sana nione impact ya kuweka wanawake pamoja, kazi ziende, spidi iende, nataka kuona hayo matokeo"
''Ningependa kuongelea 46% ya wanawake tumefanya 'Affirmative action', nimefanya hivi nikijua wanawake mna uwezo mkubwa wa kufanya kazi hii hamna sababu ya kwenda kuwa wanyonge”
Viongozi Wanawake na Wanaume mshirikiane
Rais Samia pia amewaagiza wakuu wa mikoa waliopelekewa makatibu tawala wanawake wakafanye nao kazi sawa kwani wana uwezo na sifa zinazostahili.
“Naomba sana mkashirikiane, kule ambako kuna RAS na RC ambao ni Wanawake na Wanaume mkashirikiane mpendane na naposema mpendane sikusudii yale nakusudia mkapendane kwenye kazi mkienda mkifanya yenu Vyombo vinakutazameni Mimi yangu ni maamuzi”
Kuna tuliowabadilisha vituo, si kwamba mlitenda mabaya
“Nimewasimamisha wakuu wa mikoa na Ma-RAS ili nione, kama umesoma Sociology utagundua huko kutakuwa na nini, ndio maana nilipomsimamisha RC Mwanza na RAS nikaona hiki ni kiberiti na petroli, Ngusa ni mkimya yule kule ni mlipukaji, sijui itakuwaje ila sisi tutaangalia.
“Kuna tuliowabadilisha vituo, si kwamba mlitenda mabaya mlikotoka, kubadilika ndio kukuza uzoefu na kujifunza zaidi, ukizoea palepale hutafanya vizuri, ukienda sehemu mpya nenda na mazuri acha mabaya kule, kafanye kazi.
“Wengine hawakuwa kwenye uongozi, tumewaibua, kaonyesheni kwamba mnaweza kufanya kazi. Nimepata malalamiko mbona huyu alikuwa balozi ameshushwa, hapana, RAS ni dhamana kubwa, tunaamini mtakuwa washauri na wasimamizi wazuri.
Sina uwezo wa kuhesabu matofali, nie mnisaidie huko
“Nendeni mkasimamie matumizi mazuri ya serikali, Hayati Dkt. Magufuli, alikuwa na huo ujuzi wa kwenda na kuhesabu mabati na matofali, lakini mimi sina huo ujuzi mimi ujuzi wangu ni grafu za uchumi si ujuzi wa construction engineering, nyie mtanisaidia huko.
“Nimelaumiwa sana nilipomteua Batlida kwamba huyu alikuwa Balozi kwanini kamshusha, hukushushwa u-RAS ni dhamana kubwa nenda kafanye kazi kuna matarajio mengi wananchi wanatusubiri.
“Kamanda Wambura umefanya kazi nzuri sana, utumishi wako katika Jeshi la polisi ni wa kutukuka, hivi karibuni tulikuwa na changamoto Dar es Salaam umefanya kazi nzuri sana na ndicho kilichonivutia nikuweke hapo sasa kuwa DCI,” amesema Rais Samia.
Kila aliyeteuliwa anaangaliwa kwa karibu
"Kila niliyemteua ana mtu nyuma anamfuata, na humjui ni nani. Nendeni kafanye kazi mjue nina jicho linakuangalia huku, na sitanii kwenye hilo."

Msiwakwamishe wapinzani ninaowateua
“Kwa RC Queen Iringa tuna experience ya Kilimanjaro tulipomuweka Anna walimpa shida Ma-DC akina Agness ambaye sasa nimekupandisha kuwa RC, tunawavuta hawa toka Upinzani sababu nao ni Watanzania na tunayehisi ana mchango tutamuingiza”Kuna tuliowabadilisha vituo, si kwamba mlitenda mabaya