Mh.Rais amewaasa MARAS na WAKUU WA MIKOA wakawasikilize vyema WADAU wa chama hususani wanapotaka ILANI YA CHAMA CHAO ITEKELEZWE IPASAVYO.....

Mh.Rais SSH amewakumbusha wote wakiwemo na wale ambao walikuwa/wametoka UPINZANI,ya kwamba WAMEAPA kuisimamia ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI na kuwa si HIYARI ila ni lazima....

Je umeshawahi kuyasikia maneno ya kiongozi mteuliwa wa RAIS ambaye huwa ameshawahi kusema kuwa yeye ni mtumishi na mtendaji tu wa SERIKALI na chama cha CCM hakimhusu kihivyo?!!🤣

TUTUPIE USHUHUDA WAKO HAPA.....

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#SiempreCCM
Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa katiba mpya
 
Huyu mzee nae anatakiwa apumzike, tokea enzi za Nyerere yupo, enzi za Mwinyi yupo, enzi za Mkapa yupo, enzi za Kikwete yupo, enzi za Magufuli yupo, enzi za Samia yupo( kwa sauti ya Mheshimiwa sana Makongoro Nyerere ). Hana tofauti na akina Wassira!
Hana Tofauti na M/kiti Wa Cdm, Mkapa Kaondoka Yeye Yupo, JK Kaondoka Yeye Yupo, JPM(Mungu amlaze mahala pema peponi) Mjuba Mwenyekiti Yupo, Hata Samia ataondoka Mjuba atabaki Kama M/kiti... Hakuna utofauti Sana
 
Eti wanawake wakigombana watamuaibisha mama 🤣

Kwa nini wasigombane kugombea wanaume walio wachache?

SSH jiandae madam kuaibishwa na hao watoto wa kike uliowateua
 
Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Samia Suluhu Hassan leo jumatano Juni 02, 2021 amewaapisha makatibu tawala wa mikoa (RAC) pamoja na wakuu wa taaisisi katika hafla iliyofanyika katika ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Zifuatazo ni dondoo na nukuu kutoka katika hotuba ya Rais katika hafla hiyo.​
  • Majukumu ya makatibu tawala (RAS)
Makatibu tawala wa mikoa wana majukumu mbalimbali yakiwemo; RAS ni mtendaji mkuu wa mkoa, mkuu wa utumishi katika mkoa, katibu wa kamati ya ulinzi na usalama, na msimamizi wa masurufu.
Rais amesema:
"Makatibu Tawala wa mikoa ni watendaji wakuu wa Serikali katika mkoa, nyinyi ni wasimamizi wa shughuli zote za kiutendaji katika mikoa, maafisa masuhuri wa mikoa na wakuu wa utumishi wa umma kwenye mikoa yenu. Kwa hiyo mna kazi kubwa ya kwenda kuifanya huko muendako." Pia akaongeza "Nyinyi (RAS) ndiyo viungo wa Serikali za mitaa na Serikali kuu, taarifa zote kutoka huko zinatoka kwenu. Ni wajibu wenu kuleta taarifa zilizo sahihi.Kila niliyemteua kuna mtu nyuma anamfuata na hajui ni nani, kafanye kazi ukijua nina jicho linakuangalia na sitanii katika hilo." Akafunga kwa kusema " Watumishi wote wa Serikali kwenye mikoa wako chini yenu (RAS). Kazi ya kuchunga watumishi wa umma ni shughuli kubwa kwa sababu tunajua yanayotendeka huko mikoani, watumishi wa Serikali wakifanya vizuri ni nyinyi na wakifanya vibaya ni nyinyi; mna kazi huko ya kwenda kufanya."
  • Ubunifu na kufanya kazi.​
Rais amewasisitiza wateule wote kuwa wanatakiwa kufanya kazi, wawe wabunifu na wakusanye mapato.
"Tunatarajia ubunifu wenu wa kiwango cha juu katika kujenga uchumi wa nchi hii. Nendeni kasimamieni uchumi wa mikoa yenu. Uchumi ni mapato na matumizi; kwenye ukusanyaji wa mapato tekelezeni sheria (enforcement of law) na sio utekelezaji mwingine (task force). Sheria zipo zinazoelekeza ukusanyaji wa mapato, msiende kufuata vifua vyenu na mioyo yenu."
"Kama mlivyoapa hapa na kumuomba Mungu awasaidie; Mkachape kazi vizuri na mkawajibike kama matarajio ya wananchi wengi yalivyo."
"Majukumu yaliyo mbeleni yenu ni makubwa mno na wote tunawatazama nyinyi. Ninyi ni kiungo muhimu kati ya Serikali za mitaa na Serikali Kuu."
  • Kuwateua wanawake wengi.
Rais ameeleza kwamba amewateua wanawake wengi katika nafasi hizo kwa sababu wanawake wana uwezo mkubwa na wanafanya kazi vizuri. Rais amesema
"Kuhusu 46% ya wanawake (RAS); tumezingatia usawa wa kijinsia (Affirmative action) lakini sio hilo tu; nimefanya hivi nikijua wanawake mna uwezo mkubwa wa kufanya kazi hii, hamna sababu ya kwenda kuwa wanyonge. Huko mnakokwenda kunatakiwa uadilifu, utendaji uliosimama vizuri, uaminifu lakini na unyenyekevu kwa watu (wananchi wa kawaida), kazi hii wanawake mnaifanya vizuri."
  • Viongozi wanawake kugombana
Rais amewaonya viongozi wanawake waache tabia ya kutunishia misuli bali wafanye kazi.
Rais amesema, "Mikoa ambayo kuna wanawake kwa wanawake, ile bibi usinibabaishe nisije nikaisikia. Pale nyinyi sio wanawake ni Mkuu wa Mkoa na RAS, hamna sababu ya kuparuana, mkifanya hivyo mnanitia aibu mimi."
  • Migogoro ya ardhi
Rais amewataadharisha wateule wote kuwa waachane mara moja na tabia ya kujiingiza katika migogoro. Rais amesema:
"Sitavumilia kusikia RAS, Mkuu wa Mkoa naye ameenda kuingia kwenye migogoro ya ardhi. Umepelekwa kwa kazi maalum, usieende kushiriki kwenye migogoro ya ardhi.Nendeni (RAS) mkasimamieni matumizi mazuri ya serikali, kama kuna miradi basi iendane na thamani ya fedha inayotumika." na pia akaongeza "Tunatarajia mtakwenda kuwa washauri wazuri pia mtakwenda kuwahudumia watu vizuri. Mnakokwenda kuna migogoro mingi ya mirathi na migogoro ya ardhi, nendeni kasimamieni."
  • Uwekezaji
Rais amewaagiza wateule wote walioapa waende wakaweke mazingira mazuri ya uwekezaji. Rais amesema, "Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, kasimamieni uchumi wa viwanda kwa kutenga maeneo wawekezaji waje. Yawepo maji, umeme, njia zipitike ili mwekezaji akae, afanye uzalishaji na uchumi wetu ukue. Nendeni kaendelezeni maeneo yenu ya viwanda."
  • Kufanya kampeni za ubunge
Rais amewaonya wale wote waliokosa ubunge ila wameteuliwa kwenye nafasi za uongozi waache kufanya shughuli za kutafuta ubunge bali wawatumikie wananchi.
Rais amesema, "Uzoefu unatuonyesha wale waliogombea ubunge na hawakufanikiwa kwa sababu hizi na zile na tukawapa nafasi (RC na RAC), kawaida mawazo yenu yanakuwa tena kule mlikotoka kwenye jimbo. Kafanyeni kazi achaneni na hayo mambo ya ubunge."

IMG-20210602-WA0068.jpg
IMG-20210602-WA0069.jpg
IMG-20210602-WA0070.jpg
IMG-20210602-WA0071.jpg
IMG-20210602-WA0072.jpg
IMG-20210602-WA0081.jpg
IMG-20210602-WA0082.jpg
IMG-20210602-WA0083.jpg
IMG-20210602-WA0084.jpg
IMG-20210602-WA0085.jpg
IMG-20210602-WA0088.jpg
IMG-20210602-WA0091.jpg
 
Back
Top Bottom