BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,124
1689135807959.png
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku tabia ya wanaume kusuka nywele na anayekamatwa faini yake ni Sh1 milioni au kifungu cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Julai 11, 2023, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Elimu na Utamaduni Zanzibar, Dk Omar Adam amesema hatua hiyo inalenga kulinda silika na tamaduni za Kizanzibari.

Amesema katazo hilo ni kwa mujibu wa sheria namba saba ya mwaka 2015 inayolenga kulinda utamaduni, mila na desturi za Mzanzibari bila kuathiri mambo mengine.

“Zanzibar hairuhusu mwanaume kusuka nywele faini ya kusuka nywele kwa Zanzibar ni Sh1 milioni au miezi sita jela au vyote kwa pamoja,” amesema.

Amesema hakuna kibali wala kulipia ili uruhusiwe kusuka nywele kwa mwanamme kama ambavyo awali ilisambaa kwennye mitandao ya kijamii.

“Sheria ilikuwa haijaanza kutekelezwa kwa kutoa faini lakini imeshatokea kama mara tatu mtu anakamatwa na kupewa onyo na wengine wapo wamejirekebisha na wengine wanaendelea kujirekebisha,” amesema

Hata hivyo, amesema katazo hilo haliwahusu Wamaasai kwasababu wanatambua kwamba huo ndio utamaduni wao kwamba mwanaume anasuka na mwanamke ananyoa au naye anasuka.

Kuhusu suala la kuathiri utalii wa Zanzibar, Katibu huyo amesema haliwezi kuathiri kwa sababu utafiti alioufanya kwanza watalii wengi hawasuki huo ni utamaduni ambao umetokea huku.

Kuhusu wasanii, amesema iwapo kuna msanii anataka kufanya shughuli zake wanaweza kukutana naye wakazungumza akavaa kofia mpaka anapokwenda kwenye maonyesho yake.

“Tunachosema suala la ushirikiano wa Muungano kisiwei kichaka cha kuharibu tamaduni silka na atamaduni za Kizanzibar ni akam ilivyo bangi hatuwezi kuruhusu kwamba ziendeel huku asili tuliochiwa na wazee wetu inapotea na katika sula hili tumejipanga tutakuwa wakali sana” alisema

Amesema watapitia hata kwenye shule kutoa elimu hiyo kwa walimu na wanafunzi ili kuwadhibiti wnafunzi wenye tabia hizo.

Sio mara ya kwanza kwa Zanzibar kutoa makatazo kama hayo, mwaka 2021 aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Musa alipiga marufuku kuvaa nguo fupi (nusu uchi) kwa watalii ili kulinda utamaduni wa Zanzibar

Agizo hilo lilitolewa, huku ikielezwa iwapo wakibainika wameevaa nguo zisizo na stara atakamatwa anayewatembeza na kutozwa faini, hata hivyo jambo hilo utekelzaji wake haukuzingatiwa.

Pia, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashidi Msaraka aliwahi kupiga marufuku vijana wanaonyoa viduku ambapo aliwahi kuwakamata na kuchukua mkasi kuwanyoa, hata hivyo nalo halikuwa na mwendelezo wake.

MWANANCHI
Sasisho
Waziri Maulid Mwita aomba radhi na kutengua kauli ya katibu mtendaji wa baraza la sanaa juu ya kulipa 1,000,000 kupata kibali cha mwanaume kusuka

Waziri Tabia amesema Katibu Mtendaji huyo aliteleza, na kwamba Zanzibar inasimamia sheria inayotaka kulinda mila na utamaduni wa Mzanzibar na ipo kanuni inayoeleza katika mipaka ya Zanzibar wanaume wa Kizanzibar kusuka ni kinyume na mila, utamaduni na desturi na yeyeote atakayekiuka hayo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ama kifungo cha miezi 6.

Zaidi soma: Waziri Maulid Mwita aomba radhi na kutengua kauli ya katibu mtendaji wa baraza la sanaa juu ya kulipa 1,000,000 kupata kibali cha mwanaume kusuka

Mada zinazohusiana
Vitu vingine vilivyowahi kupigwa marufuku Zanzibar
 
Safi sana, hii ingeletwa na huku bara pia.

Ukiona picha ya Rayvanny kwa nyuma unaweza hata kupiga nyeto jinsi alivyojipura na kusuka juu utasema ni mtoto wa kike. Imefikia kiasi wasanii wa kike wanashindwa na wanaume kwenye kujiremba, heshima iko wapi hapo.

Ukimuweka mwana hiphop Chemical na Rayvanny unaweza hisi Chemical ndio mwanaume.
 
Safi sana, hii ingeletwa na huku bara pia.

Ukiona picha ya Rayvanny kwa nyuma unaweza hata kupiga nyeto jinsi alivyojipura na kusuka juu utasema ni mtoto wa kike. Imefikia kiasi wasanii wa kike wanashindwa na wanaume kwenye kujiremba, heshima iko wapi hapo.

Ukimuweka mwana hiphop Chemical na Rayvanny unaweza hisi Chemical ndio mwanaume.
 
Sasa hapo Kuna uzuri gani?

"Kibari kusuka milioni, lengo kulinda utamaduni"

Ina maana Nikilipa milioni Kisha nikasuka huo utamaduni utakuwa umelindwa? Hapo walichofanya ni kwamba Zanzibar kusuka ni ruksa ila Kuna gharama kubwa.

Bla bla za kuprotect vijana wasijiingize kwenye mambo ya hovyo wangepiga marufuku Kama hivi "Zanzibar mtoto wa kiume kusuka hairuhusiwi" FULL STOP.
 
Tabia ya wanaume kusuka na kutoga masikio na pua inakera na kushalilisha uanaume.

Suala la kushindana na dada na binti zetu katika urembo liwekewe sheria ambapo mwanaume atalipia angalau milioni 5 kupata kibali cha kusuka ama kutoga masikio.

Nimefurahishwa na Zanzibar kuwa na sheria kama hii lakini wao ni kwa wanaume wanaotaka kusuka nywele

Angalieni hicho ni chanzo cha mapato
 
Back
Top Bottom