Zuchu afungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa Zanzibar

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1709628191466.png

Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Pia Soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Kuna watu mnaroho ngumu hivi nyimbo zile za kihuni sijua sukari mara namnyonyesha mnazisikizaga nyumbani na watoto wapo kweli. Mle hamna msanii matusi tu yamejaa bora nisikilize msondo ngoma au wanasikinde ngoma ya ukae sio upuuzi wa weka mate itereze.
 
Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita...
ZA NINI HIZI Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa
 
Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita...
CCM inaharibu vijana kwa kuhendekeza wasanii wa hovyo.
 
Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.
 
Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.
Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Ila hii faini kwa mtu baki asiyekuwa wao si ni sawa na kumla kichwa Beyonce binti beberu huko aliko?
 
Hukumu ya wapi hii.
Mtu aliyepewa adhabu halazimiki kuomba radhi.
Kuomba radhi lengo lake ni kusamehewa.
Sasa kama hawajamsamehe, kwa nini aombe radhi?
Mnapoandika hukumu muwe mnajitahidi kushirikish wanasheria.
Sio mtu kasomea uhasibu eti naye unamkuta anatoa hukumu. No way.
 
Back
Top Bottom