Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,224
- 12,729
Kutoka kitabu Safari za Waswahili.
Khabari za nywele zao waanaume na wanawake.
"Wanawaume wengine wanasuka na wengine wananyoa, na kusuka kwao kwanza huosha nywele na majani ya mkunungu na maji yaliyo moto kidogo. Na majani yake yanateleza sana maji yake. Akesha osha kichwa, huleta udongo mwekundu, khalafu huzisuka zile nywele, na kupaka udongo juu yake. akesha suka hutia mafuta ya nyonyo kichwani. Huo ndio msuko wa waanaume.
Wa kadhalika wanawake wanafanya kama hivyo. Mwanamke hanyoi nywele zake, ila anayetoka katika uzazi, baada ya kwisha kuzaa kwa siku arbaini, hunyoa nywele zake, ama kama hukazaa hazinyoi. Walakini wanawake namna wanayosuka nyingine na wanaume namna nyingine, bali wote wanatia udongo mwekundu kichwani na mafuta ya nyonyo.
Wanawake wanasukwa na wanawake wenzao, na wanaume kadhalika, walakini khabari ya kusuka wanaume yalikuwa zamani, sasa mno wananyoa. Na wanawake misuko ya kizamani wameiwacha, wanasuka namna ya sasa. Kadhalika udongo mwekundu hawaatamii sana."
Pia soma:
Baraza la Sanaa Zanzibar: Wanaume Wanaosukwa kama Wanawake kukamatwa, faini ni Tsh. Milioni 1 au kifungo cha Miezi 6
Kwa marufuku nyingine Zanzibar soma: