Waziri Maulid Mwita aomba radhi na kutengua kauli ya katibu mtendaji wa baraza la sanaa juu ya kulipa 1,000,000 kupata kibali cha mwanaume kusuka

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
HABARI Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, ameomba radhi na kutengua kauli iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam ya kwamba mwanaume yeyote anayetaka kusuka visiwani humo itambidi alipie kiasi cha shilingi milioni 1 ili kupata kibali cha kusuka.

Waziri Tabia amesema Katibu Mtendaji huyo aliteleza, na kwamba Zanzibar inasimamia sheria inayotaka kulinda mila na utamaduni wa Mzanzibar na ipo kanuni inayoeleza katika mipaka ya Zanzibar wanaume wa Kizanzibar kusuka ni kinyume na mila, utamaduni na desturi na yeyeote atakayekiuka hayo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ama kifungo cha miezi 6.

Aidha Waziri amesema kwamba Wizara yake itaendelea kuheshimu tamaduni za watu wengine ikiwemo pia kuzingatia haki za binadamu na kwamba sheria za Zanzibar ziko palepale kwamba mila silka na tamaduni kuendelea kulindwa.

1689668926062.png

Pia soma: Baraza la Sanaa Zanzibar: Wanaume Wanaosukwa kama Wanawake kukamatwa, faini ni Tsh. Milioni 1 au kifungo cha Miezi 6

Marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
 
#HABARI Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, ameomba radhi na kutengua kauli iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam ya kwamba pale kwamba mila silka na tamaduni kuendelea kulindwa.
Nilisituka kuisikia hiyo habari jana na nikakumbuka labda sasa twarejeshwa enzi zile tulipokuwa tukipimwa upana wa suruali wa chini kwa chupa.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, ameomba radhi na kutengua kauli iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam ya kwamba mwanaume yeyote anayetaka kusuka visiwani humo itambidi alipie kiasi cha shilingi milioni 1 ili kupata kibali cha kusuka.

Waziri Tabia amesema Katibu Mtendaji huyo aliteleza, na kwamba Zanzibar inasimamia sheria inayotaka kulinda mila na utamaduni wa Mzanzibar na ipo kanuni inayoeleza katika mipaka ya Zanzibar wanaume wa Kizanzibar kusuka ni kinyume na mila, utamaduni na desturi na yeyote atakayekiuka hayo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ama kifungo cha miezi 6.

Aidha Waziri amesema kwamba Wizara yake itaendelea kuheshimu tamaduni za watu wengine ikiwemo pia kuzingatia haki za binadamu na kwamba sheria za Zanzibar ziko palepale kwamba mila, silka na tamaduni kuendelea kulindwa.
 
KWA taifa linalotegemea baishara ya utalii Ile ilikua kauli ya kukurupushwa mno

Tukisema baadhi ya viongozi ni wehu hua mnakataa, unafahamu unapokea watu kutoka dunia nzima, na wana tamaduni zao wengine wanasuka, wengine wanavaa hereni na wengine huchora tattoo, yaani unataka bana boy anyoe ndio aje kufanya video z’bar? Unataka wanaotoka italy nao wanyoe ndio waje mambo ya ajabu kweli kweli
 
Kumbe Wakurya tumevuka bahari HADI Zenji....! Tuliacha mbegu!?

Nimefurahi kuona damu yetu ya kikurya iko na mamlaka Zenji...

Damu ya kikurya....maamuzi ya ki-yakheee!
 
Upuuzi, kauli ya kwanza ilikuwa sahihi,haina tofauti na hii, kuna watu huwa wanasema wazanzibari wengi hawana Elimu na hao wachache waliosoma wana tatizo (nimesema kuna watu)
atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ama kifungo cha miezi 6.
Kwa kifupi, hii kauli ya pili haijatengua chochote, na msemaji wa kwanza hakuteleza ulimi, hiyo ni sheria yao wazanzibari ,kwanini wanaionea aibu ?
 
Ni sawa na mwanamke aseme ana mimba alafu akwambie, "ila haina maana kwamba nilifanya ngono "
 
Kwa Utaratibu mpya wa kulipia 1m Kwa anaesuka nywele hapa Zanzibar ndugu zetu Maasai toka Tanganyika watamudu?
 
Ni mbaguzi, Period.
Anaenda kuokota mila na desturi za wakuja halafu anatumia nguvu ya Wananchi wanaomlipia mshahara, kuwakandamiza na kuwabagua kwa mila na desturi zao. Yani, ukilitizama suala na shauri hili kwa undani jambo, ni sawa na kusema 'hatutaki nywele zisizofana na mwarabu au mzungu kisiwani hapa'

Alipaswa kujiuzulu.
 
Back
Top Bottom