Wewe ni chawa wa nani?

Unamdanganya sana 'Maza Mizinguo' kwa hayo unayomshauri ayafanye.

Kwa bahati nzuri anazo akili za kumtosha kutofuata upumbavu unaojaribu kumhimiza aufanye.
Kutofuata ushauri huu will be a grave mistake,......hatofanya chochote cha maana; atadharaulika kwa wapinzani, wananchi mpaka chamani kwake! Akiwalea hawa, nakuapia, kufikia 2024 ataona muda wake unachelewa kuisha!!
 
Baadhi ya Watanzania wamejitokeza nje ya Ubalozi wa Tanzania Nchini #Marekani na kufanya maandamano wakiwasilisha madai mbalimbali.

Baadhi ya madai yao waliyoandika kwenye mabango yao ni Mabadiliko ya Katiba, kuachiwa huru kwa Wakili Peter Madeleka pamoja na kufukuzwa Bungeni Wabunge 19 wanaodaiwa kuwa Bungeni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Watanzania wameamua Wanapiga Nje n Ndani🔥🔥🔥🔥
 
Kutofuata ushauri huu will be a grave mistake,......hatofanya chochote cha maana; atadharaulika kwa wapinzani, wananchi mpaka chamani kwake! Akiwalea hawa, nakuapia, kufikia 2024 ataona muda wake unachelewa kuisha!!
Ushauri wa kipumbavu kabisa huo.
Wakati wa mageuzi kwa Tanzania ni sasa, hata ufanye nini huwezi kuyazuia tena.
 
Hao ni vijana wenzetu waliokulia katika maisha bora viunga vya Ursino ,Ada Estate ,Regency...wazazi wao wakawapeleka US....wengine ni wabwia unga tu......
nilivyosikia waandamanaji nikajua mitaa flani imefungwa huko US,kumbe wabwia unga kadhaa tu.
 
Ushauri wa kipumbavu kabisa huo.
Wakati wa mageuzi kwa Tanzania ni sasa, hata ufanye nini huwezi kuyazuia tena.
Hat Mh Rais Samia kashasema.

Hivi wanadhani hizo pesa kwa marekani zinatoka hivi hivi.

Marekani anapiga msumari huku watanzanua nao wakiendelea kudai mabadiliko muhimu kikaba.

Mh Samia anajua Nchi kwanza Chama baadae.
 
Baadhi ya walioko katika maandamano wanafahamika....

Ni vijana wa wenye nazo,maisha bora na wenye pesa waliolelewa Masaki ,Kichanga Chui ,Mikocheni maeneo ya Regency na mitaa ya Ursino,Ada Estate ,Upanga....

Hivi kweli hawa ndio WANAWASEMEA watanzania wote hata wa kule Nyanguge ,Kwimba ,Sakura ,Kibinda ,Mkwaja ,Bweni ,Mwera ,Kipumbwi ,Pembeabwe,Ipinda ,Matema ,Tanganyika Masagati ,Mlimba na Mkoka Nachingwea?!!!!

Yaani watanzania hao nao wanahitaji katiba mpya ?!!!😳🤣🤣

#Siempre JMT🙏
#Katiba Iliyopo Inatosha 👍
Kwa hiyo vijana wenye nazo ndio hutaki wapiganie katiba mpya?

Acha wivu.

Wenye akili ni wenye nazo.

Jumbe Brown hamna pakukimbilia this time.

Wanyonge wamewakataa na matajiri pia.
 
Baadhi ya Watanzania wamejitokeza nje ya Ubalozi wa Tanzania Nchini #Marekani na kufanya maandamano wakiwasilisha madai mbalimbali.

Baadhi ya madai yao waliyoandika kwenye mabango yao ni Mabadiliko ya Katiba, kuachiwa huru kwa Wakili Peter Madeleka pamoja na kufukuzwa Bungeni Wabunge 19 wanaodaiwa kuwa Bungeni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wamefanya jambo jema sana. Wabarikiwe amina.
 
Badala ya katiba mabango yangebeba ujumbe kumshurtisha Rais arudi nyumbani kushughulika na mambo muhimu zaidi tunayokabiliana nayo kama kudorora kwa uchumi kutokana na mambo mbali mbali.

Yaani kwa hali ya uchumi namna ilivyo mbaya ni anasa tu zinazofanyika huo uzinduzi wa filamu.
 
Kila la kheri kamanda, twasubiri mabadiliko tuone. Sorry, hv ni kupitia cdm au umoja party?!!!!
Unaendelea kuonyesha ujuha wako hapa.
Hivi Tanzania wewe unaiona katika picha hiyo pekee ya hayo mavyama unayojitangaza nayo?
 
Back
Top Bottom