Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Kufuatia Ziara ya rais Samia huko Marekani, wananchi waishio huko wameandamana kudai katiba mpya.
Watanzania hao walibeba mabango yenye ujumbe wa Kudai katiba mpya na Wengine kubeba mabango yanayotaka serikali imwachie huru Mwanasheria Peter Madeleka ambaye inasemekana amekamatwa na Polisi lakini hajulikani alipo(Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi)
Pia walivaa T-Shirt zinazotaka haki itendeke kwa Ben Saanane, Azory, Gwanda etc
Hapo juu nimeweka video ya maandamano hayo huko Marekani
Pia soma;
Rais Samia: Kisiasa tupo vizuri, leo wanangu wamejipanga na Mabango yao nikawaambia nimewaona, nikawapungia Mkono
Rais samia akiwa Washington D.C amesema Tanzania kisiasa tupo Vizuri. Hali ya Kisiasa Tupo Stable,Hali ya Kisiasa iko Nzuri, tunachukua Hatua za kufanya Vyama vyote vya Siasa vikae Pamoja Kujadili namna ya Kuendesha Siasa zetu Nchini. "Nimeunda timu ndani ya vyama vya siasa, tumeweka Jeshi la...
www.jamiiforums.com
WATANZANIA WAANDAMANA MAREKANI
Baadhi ya Watanzania wamejitokeza nje ya Ubalozi wa Tanzania Nchini #Marekani na kufanya maandamano wakiwasilisha madai mbalimbali
Baadhi ya madai yao waliyoandika kwenye mabango yao ni Mabadiliko ya Katiba na kuachiwa huru kwa Wakili Peter Madeleka pamoja na kufukuzwa Bungeni Wabunge 19 wanaodaiwa kuwa Bungeni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)