Maandamano ya Watanzania nchini Marekani wakati wa ziara ya Rais Samia; Je, suala la Katiba Mpya ni muhimu kwa Taifa letu la Tanzania!?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
MAANDAMANO YA WATANZANIA NCHINI MAREKANI;JE SUALA LA KATIBA MPYA NI MUHIMU KWA TAIFA LETU LA TANZANIA!?

Leo 12:15pm 24/04/2022

Leo tumeamka na video,picha za maandamano ya Watanzania diaspora,katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,wakiwakilisha madai mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya Katiba Mpya na kuachiwa huru wakili @PMadeleka lakini Mimi nimevutiwa na dai la katiba mpya na naomba Watanzania leo tulijadili suala hili,tuache uchawa,tujadili mambo yenye faida kwetu na kwa Taifa letu la Tanzania,kuna haja wakati mwingine haya mambo mazito nasi Watanzania tukayajadili kuliko kusubiri hadi Diaspora uko Marekani waandamane na ndio sisi tujue kuna tatizo tunalo,naamini Diaspora wamekuwa nguzo muhimu kulitetea taifa la la Tanzania kwa siku za hivi karibuni,sasa je wanavyovitetea vina uhalisia kwa Wananchi wa Tanzania!?..

Waluguru wanasema "No research No right to speak) tutajuaje suala la katiba mpya ni takwa la Jamii ya Watanzania au takwa la Wanasiasa!? ni lazima kufanya kura ya maoni kwa watu wote wakiwa huru ili kujua kama kweli wanataka mabadiliko ya katiba au la?? Je sisi tunaoandika mitandaoni ni % ngapi,Diaspora wa Marekani asilimia ngapi!? Watanzania wenyewe ni asilimia ngapi!? ya wale wanaohitaji katiba?? Kwa utafiti huo walao tungejua kuwa Watanzania wangapi wamehojiwa na makundi yapi ambayo wamesema wanataka au hawaitaki.tusiende na mihemko tuuuu twendeni kihaya(kisomi) kwa faida ya Taifa letu la Tanzania.

Tujiulize maswali machache,

1) Hitaji la katiba mpya ni lakisiasa, au la kijamii?

2) Kwa nini katiba mpya idaiwe sasa na kwa nguvu zaidi kama tulivyoona uko Marekani kwenye ziara ya Mama? Kwa nini haikuwa miaka mitano iliyopita? Nini kimepelekea kudai katiba mpya sasa?

3) Eleza hoja yenye mashiko katiba mpya itasaidiaje kuleta maendeleo ya Tanzania na watanzania? Eleza japo kwa mifano hai ni nchi zipi kwa kuwa na katiba(nzuri) zina maendeleo kwa sababu ya katiba?

4) Unakubali au kukanusha juu ya ukweli kuwa katiba iliyopo inapangufu katika tume ya uchaguzi na si katiba yote? Ukanushaji au ukubali uwe na majibu yaliyo na vielelezo hai.

5) Tuambie kwa faida au kwa hasara,nini kitatokea kama tusipokuwa na katiba nyingine kwa miaka 10 ijayo? Mwananchi aliyeko kule Matombo, Morogoro,kasulu,Kigoma, Nyakahoze au Mugumu Serengeti au kule songwe kijijini ataathirika vipi?

-Majibu yanaweza kuwa yafuatayo;-

1.Katiba mpya ni takwa la kijamii ya Watanzania, na linapata msukumo mkubwa na wanasiasa kwani katiba ni mchakato wa kisiasa.

2.Katiba imeanza kudaiwa toka 1992 mfumo wa vyama vingi uliporejea hapa nchini. Huenda wakati huo vijana wengi wa sasa walikuwa hawajazaliwa,ni kama ilivyo wale ambao hawamjui Jenerali Imrani Kombe na Augustino Lyatonga Mrema,Sasa basi 2010-2015 kulifanyika msukumo mkubwa wa kupata katiba mpya, hatimaye ilitungwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya, na tume ya Jaji Warioba ilizunguka nchi nzima, kukusanya maoni ya wananchi. Hatimaye kukawa na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa inasubiri kupigiwa kura japo rasimu ya Warioba ilichezewa. Miaka mitano iliyopita nchi hii ilipata kiongozi Mzalendo na kiwango cha Uzalendo wake kilizidi asilimia mia moja,Watanzania waliamini walipata Kiongozi waliyemtaka kuiongoza nchi mahali sahihi na kulinda rasilimali za nchi yao.

3.Katiba mpya italeta maendeleo maana itatoa viongozi wenye uhalali wa umma, na wataweza kuwajibishwa iwapo watakosea. nchi za Kenya, Afrika kusini na Ghana ni mifano halisi wa nchi zenye katiba bora, na zinaaminika hata na wawekezaji, kwani zinajali utawala wa sheria, na sio utashi wa rais aliye madarakani.

4.Tume ya uchaguzi ni sehemu tu ya mapungufu ya hiyo katiba, lakini kuna madaraka makubwa ya urais ambayo yanatumika vibaya, na kwa maslahi binafsi ya rais na genge lake. Udhaifu huo umedhibitika wazi wakati wa awamu ya Richmond na Escrow, na katika awamu zote za Serikali ya CCM.

5.Bila utawala wa sheria ni ngumu muwekazaji makini kuwekeza,katiba itatoa msimamo wa faida kwa nchi na kwa mwekezaji.Tutajua kinachopatikana kwenye uchimbaji Madini kutoka kwa kila mwekezaji,tutajua tunachopata kutoka katika Bandari zetu,tutajua kodi zetu zinatumikaje,katiba itasimamia maendeleo ya Tanzania nzima,ndipo kila mwananchi atakuwa Mzalendo kwa maana atakuwa ameonda faida ya rasilimali katika nchi yake,faida ya kodi yake ikimletea maendeleo katika nchi yake ya Tanzania.

-Tuchekeche akili zetu kwa kufanya tafakuri jadidi.

Maendeleo siyo lazima yawe ya vitu kama nyumba, magari, n.k Kumbuka kuna maendeleo ya kiuchumi, Kijamii, na kisiasa,kuwa na katiba ambayo inatoa kinga dhidi ya viongozi wenye choyo, wenye kutumia mali za umma vibaya, wenye kutumia madaraka vibaya hayo nayo ni maendeleo makubwa sana. Mfano mzuri ni Nchini Kenya ambapo kupitia katiba yao. Rais haongozi kwa matamko. Anachokifanya Rais kinapingwa mahakamani. Kitu ambacho ni tofauti hapa Tanzania.Mfano kipindi cha ESCROW viongozi wote waliojihusisha na ubadhilifu ule wangeshitakiwa ila kwa sababu kuna kinga za hapa na pale hawakufanywa lolote.

Kadhalika, investors hawawezi kuwekeza katika Nchi ambayo inaongozwa kwa matamko badala ya kuongoza kwa kuheshimu Katiba na sheria zingine za Nchi. Je kati ya Kenya na Tanzania ni nchi gani ina wawekezaji wengi?Tanzania tupo nyuma sana kimaendeleo katika nyanja ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ukilinganisha na Nchi ya Kenya,huduma za Kijamii nchini Kenya wameendelea sana mfano mzuri ni msanii Ommy dimpozi ambaye alishindwa kugundulika anaumwa ni,ni hapa nchini ila alipoenda Kenya aliambiwa tatizo lake.

-Mambo gani yanafanya suala la katiba mpya liwe muhimu sana!?

Hivi sasa tunaona Mambo mengi ya Muungano hayaendi sawa,mfano Mtanzania bara akienda Zanzibar haruhusiwi kununua ardhi Ila Mzanzibari akija Tanzania bara anaruhusiwa kununua ardhi,hili jambo tungeomba tupate ufahamu kama tumeelewa vibaya na mambo mengi tumeona yakifanyika upande wa Zanzibar,Sasa basi Katiba Mpya italeta muafaka kwa Mambo kadhaa hasa haya yafuatayo, kwa sababu lipo kundi linaloona kama maoni yake yamewekwa kando.

Masuala hayo baadhi ni;

-Masuala ya Muungano

-Tume huru ya uchaguzi

-Mamlaka yanayotajwa kuwa makubwa ya Rais

-Madaraka ya umma

-Haki za binadamu na Utawala bora

-Uwepo wa Mgombea binafsi

-Na Mgawanyo wa madaraka ya mihimili mitatu (Serikali, bunge na Mahakama) na uhuru wa Bunge na Mahakama.

Nimalizie kwa kusema,Katiba ya sasa ya Tanzania ina umri wa karibu miaka 41 sasa, ilitungwa mwaka mwaka 1977. Kwa sababu Katiba hii na katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961, ikaja ya 1962,ya 1964, 1965 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977, pamoja na marekebisho yake yote 14 kumekuwa na malalamiko kwamba wananchi hawakushirikishwa kikamilifu kuzitunga katiba hizo wakati zinahusu maisha yao. Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora ambao umeishia njiani.

Kuna masuala muhimu yanayopaswa kuwepo katika katiba Mpya ama kurekebishwa, na katika hilo Wananchi,Watanzania hawahitaji hisani kutoka kwa mtu yoyote wakiwemo viongozi.Uchumi na Katiba bora ni kama ndugu wanaoendana, ukitaka kuwa na uchumi bora inakupaswa uwe na Katiba bora itakayoleta utulivu, itakayovutia wawekezaji na itakayosimamia mamlaka na rasimili mali za nchi, kubwa zaidi la Wananchi ni usimamizi wa rasilimali za nchi yao.

Naama,naamini mapungufu yaliyopo kwenye katiba ya sasa yanaweza yasiwe takwa la kijamii kati ya Watanzania ila la kisiasa,lakini ni muhimu tukatambua kuwa jamii yote ya kitanzania ina inaustarabu wake,wakati wanasiasa wanakwenda kushoto,jamii ya kitanzania inaweza kwenda kulia kama ndio njia bora ya kulinda amani,kwa hiyo katiba mpya haiwezi ikawa ni hitaji la kisiasa pekee ilihali Watanzania uwa wanavumiliaga tu upepo mbaya unapopita,funika kombe mwanaharamu apite.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Wewe elimu yako inakusaidia kuandika maneno mingi tu bila kufikiri.

Mchakato wa katiba mpya ulishaitishwa baada ya mahitaji kuonekana. Ndiyo maana tume ya Jaji Warioba ikaundwa, ikazunguka na kukusanya maoni yanayoomyesha wananchi wanahitaji katiba mpya, katiba pendekezwa ikaandikwa, bunge la katiba likaundwa...then wewe msomi njaa unakuja kuongea nini hapa?

Unatafuta kujipendekeza upatiwe kazi?
 
Halikwepeki, watu wanataka serikali inayowajibika wa wananchi, bora enzi za mwendazake vitu vilikuwa havipandi bei ovyo.
 
Wee jama naona umeamua kuja na ID nyingine baada ya magufuli kufa
IMG_4296.jpg
 
Wengi walioandamana ni wauza madawa ya kulevya huko marekani, na wanalala kwenye nyumba za maboksi
Wewe unaongea tu kama limbukeni, utaongeleaje mambo ya nchi ambayo hata huna ndoto ya kwendapo na sidhani kama hata umewahi kutoka nje ya mipaka ya nchi hii.

Unafikiri kuuza madawa ya kulevya Marekani ni sawa na kuuza gongo hapo Chanika. Bure kabisa.
 
Hiyo namba3 imeonesha namna Gani unamiliki Kichwa kama Sanduku la kubebea meno tu
 
Wewe unaongea tu kama limbukeni, utaongeleaje mambo ya nchi ambayo hata huna ndoto ya kwendapo na sidhani kama hata umewahi kutoka nje ya mipaka ya nchi hii.

Unafikiri kuuza madawa ya kulevya Marekani ni sawa na kuuza gongo hapo Chanika. Bure kabisa.
Tumia kichwa kufikiri, sio Kubebea nywele
 
Hongereni wadau wa TZ USA,hakika Katiba Bora ndio takwa la Msingi la Watanzania imegeuka hisani ya Mwenyekiti wa CCM !!!
 
Shida ya wabongo ni wavuvi wa kufanya kaz wagumu kuamin maendeleo yao yatakuja baaada ya kuumiza miili yao au akili au pesa zao wanaamin maendeleo yao au shida zao zimelewa au yataletwa ma mtu wanapendwa kuaidiwa kama kwa mchungaji au mganga wanaaamin katika kupewa sio kupsmbana wanaamin umaskin wao au ugumu wa maisha chanzo ni katiba mpya ndio maana baadh yao wanakimbilia huko kwa mfano chadema wanashindwa kupata ushind wa kishindo simple tu sio sababu ya katiba kama wanavyodhan shida haeana personel ya kuwawezesha kufanya hivyo na hawana time wanadunda tu huku wakitoa shutuma kila siku mastermind lowasa alipokua pale alikuja na vision kaliii sana ambayo ingeifanya chadema kua chama kikubwa zaid ya ccm lowasa alikua na mpango wa kujenga ofis ya chadem kila kata tanzania na kua na mwakilish kila mtaaa maana yake nini kila uchaguz chadema ingekua na mtu wa kujal maslai yao hata kama wangenunuliwa kusingekuepo na pesa ya kuwanunua wote
 
MAANDAMANO YA WATANZANIA NCHINI MAREKANI;JE SUALA LA KATIBA MPYA NI MUHIMU KWA TAIFA LETU LA TANZANIA!?

Leo 12:15pm 24/04/2022

Leo tumeamka na video,picha za maandamano ya Watanzania diaspora,katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,wakiwakilisha madai mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya Katiba Mpya na kuachiwa huru wakili @PMadeleka lakini Mimi nimevutiwa na dai la katiba mpya na naomba Watanzania leo tulijadili suala hili,tuache uchawa,tujadili mambo yenye faida kwetu na kwa Taifa letu la Tanzania,kuna haja wakati mwingine haya mambo mazito nasi Watanzania tukayajadili kuliko kusubiri hadi Diaspora uko Marekani waandamane na ndio sisi tujue kuna tatizo tunalo,naamini Diaspora wamekuwa nguzo muhimu kulitetea taifa la la Tanzania kwa siku za hivi karibuni,sasa je wanavyovitetea vina uhalisia kwa Wananchi wa Tanzania!?..

Waluguru wanasema "No research No right to speak) tutajuaje suala la katiba mpya ni takwa la Jamii ya Watanzania au takwa la Wanasiasa!? ni lazima kufanya kura ya maoni kwa watu wote wakiwa huru ili kujua kama kweli wanataka mabadiliko ya katiba au la?? Je sisi tunaoandika mitandaoni ni % ngapi,Diaspora wa Marekani asilimia ngapi!? Watanzania wenyewe ni asilimia ngapi!? ya wale wanaohitaji katiba?? Kwa utafiti huo walao tungejua kuwa Watanzania wangapi wamehojiwa na makundi yapi ambayo wamesema wanataka au hawaitaki.tusiende na mihemko tuuuu twendeni kihaya(kisomi) kwa faida ya Taifa letu la Tanzania.

Tujiulize maswali machache,

1) Hitaji la katiba mpya ni lakisiasa, au la kijamii?

2) Kwa nini katiba mpya idaiwe sasa na kwa nguvu zaidi kama tulivyoona uko Marekani kwenye ziara ya Mama? Kwa nini haikuwa miaka mitano iliyopita? Nini kimepelekea kudai katiba mpya sasa?

3) Eleza hoja yenye mashiko katiba mpya itasaidiaje kuleta maendeleo ya Tanzania na watanzania? Eleza japo kwa mifano hai ni nchi zipi kwa kuwa na katiba(nzuri) zina maendeleo kwa sababu ya katiba?

4) Unakubali au kukanusha juu ya ukweli kuwa katiba iliyopo inapangufu katika tume ya uchaguzi na si katiba yote? Ukanushaji au ukubali uwe na majibu yaliyo na vielelezo hai.

5) Tuambie kwa faida au kwa hasara,nini kitatokea kama tusipokuwa na katiba nyingine kwa miaka 10 ijayo? Mwananchi aliyeko kule Matombo, Morogoro,kasulu,Kigoma, Nyakahoze au Mugumu Serengeti au kule songwe kijijini ataathirika vipi?

-Majibu yanaweza kuwa yafuatayo;-

1.Katiba mpya ni takwa la kijamii ya Watanzania, na linapata msukumo mkubwa na wanasiasa kwani katiba ni mchakato wa kisiasa.

2.Katiba imeanza kudaiwa toka 1992 mfumo wa vyama vingi uliporejea hapa nchini. Huenda wakati huo vijana wengi wa sasa walikuwa hawajazaliwa,ni kama ilivyo wale ambao hawamjui Jenerali Imrani Kombe na Augustino Lyatonga Mrema,Sasa basi 2010-2015 kulifanyika msukumo mkubwa wa kupata katiba mpya, hatimaye ilitungwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya, na tume ya Jaji Warioba ilizunguka nchi nzima, kukusanya maoni ya wananchi. Hatimaye kukawa na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa inasubiri kupigiwa kura japo rasimu ya Warioba ilichezewa. Miaka mitano iliyopita nchi hii ilipata kiongozi Mzalendo na kiwango cha Uzalendo wake kilizidi asilimia mia moja,Watanzania waliamini walipata Kiongozi waliyemtaka kuiongoza nchi mahali sahihi na kulinda rasilimali za nchi yao.

3.Katiba mpya italeta maendeleo maana itatoa viongozi wenye uhalali wa umma, na wataweza kuwajibishwa iwapo watakosea. nchi za Kenya, Afrika kusini na Ghana ni mifano halisi wa nchi zenye katiba bora, na zinaaminika hata na wawekezaji, kwani zinajali utawala wa sheria, na sio utashi wa rais aliye madarakani.

4.Tume ya uchaguzi ni sehemu tu ya mapungufu ya hiyo katiba, lakini kuna madaraka makubwa ya urais ambayo yanatumika vibaya, na kwa maslahi binafsi ya rais na genge lake. Udhaifu huo umedhibitika wazi wakati wa awamu ya Richmond na Escrow, na katika awamu zote za Serikali ya CCM.

5.Bila utawala wa sheria ni ngumu muwekazaji makini kuwekeza,katiba itatoa msimamo wa faida kwa nchi na kwa mwekezaji.Tutajua kinachopatikana kwenye uchimbaji Madini kutoka kwa kila mwekezaji,tutajua tunachopata kutoka katika Bandari zetu,tutajua kodi zetu zinatumikaje,katiba itasimamia maendeleo ya Tanzania nzima,ndipo kila mwananchi atakuwa Mzalendo kwa maana atakuwa ameonda faida ya rasilimali katika nchi yake,faida ya kodi yake ikimletea maendeleo katika nchi yake ya Tanzania.

-Tuchekeche akili zetu kwa kufanya tafakuri jadidi.

Maendeleo siyo lazima yawe ya vitu kama nyumba, magari, n.k Kumbuka kuna maendeleo ya kiuchumi, Kijamii, na kisiasa,kuwa na katiba ambayo inatoa kinga dhidi ya viongozi wenye choyo, wenye kutumia mali za umma vibaya, wenye kutumia madaraka vibaya hayo nayo ni maendeleo makubwa sana. Mfano mzuri ni Nchini Kenya ambapo kupitia katiba yao. Rais haongozi kwa matamko. Anachokifanya Rais kinapingwa mahakamani. Kitu ambacho ni tofauti hapa Tanzania.Mfano kipindi cha ESCROW viongozi wote waliojihusisha na ubadhilifu ule wangeshitakiwa ila kwa sababu kuna kinga za hapa na pale hawakufanywa lolote.

Kadhalika, investors hawawezi kuwekeza katika Nchi ambayo inaongozwa kwa matamko badala ya kuongoza kwa kuheshimu Katiba na sheria zingine za Nchi. Je kati ya Kenya na Tanzania ni nchi gani ina wawekezaji wengi?Tanzania tupo nyuma sana kimaendeleo katika nyanja ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ukilinganisha na Nchi ya Kenya,huduma za Kijamii nchini Kenya wameendelea sana mfano mzuri ni msanii Ommy dimpozi ambaye alishindwa kugundulika anaumwa ni,ni hapa nchini ila alipoenda Kenya aliambiwa tatizo lake.

-Mambo gani yanafanya suala la katiba mpya liwe muhimu sana!?

Hivi sasa tunaona Mambo mengi ya Muungano hayaendi sawa,mfano Mtanzania bara akienda Zanzibar haruhusiwi kununua ardhi Ila Mzanzibari akija Tanzania bara anaruhusiwa kununua ardhi,hili jambo tungeomba tupate ufahamu kama tumeelewa vibaya na mambo mengi tumeona yakifanyika upande wa Zanzibar,Sasa basi Katiba Mpya italeta muafaka kwa Mambo kadhaa hasa haya yafuatayo, kwa sababu lipo kundi linaloona kama maoni yake yamewekwa kando.

Masuala hayo baadhi ni;

-Masuala ya Muungano

-Tume huru ya uchaguzi

-Mamlaka yanayotajwa kuwa makubwa ya Rais

-Madaraka ya umma

-Haki za binadamu na Utawala bora

-Uwepo wa Mgombea binafsi

-Na Mgawanyo wa madaraka ya mihimili mitatu (Serikali, bunge na Mahakama) na uhuru wa Bunge na Mahakama.

Nimalizie kwa kusema,Katiba ya sasa ya Tanzania ina umri wa karibu miaka 41 sasa, ilitungwa mwaka mwaka 1977. Kwa sababu Katiba hii na katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961, ikaja ya 1962,ya 1964, 1965 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977, pamoja na marekebisho yake yote 14 kumekuwa na malalamiko kwamba wananchi hawakushirikishwa kikamilifu kuzitunga katiba hizo wakati zinahusu maisha yao. Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora ambao umeishia njiani.

Kuna masuala muhimu yanayopaswa kuwepo katika katiba Mpya ama kurekebishwa, na katika hilo Wananchi,Watanzania hawahitaji hisani kutoka kwa mtu yoyote wakiwemo viongozi.Uchumi na Katiba bora ni kama ndugu wanaoendana, ukitaka kuwa na uchumi bora inakupaswa uwe na Katiba bora itakayoleta utulivu, itakayovutia wawekezaji na itakayosimamia mamlaka na rasimili mali za nchi, kubwa zaidi la Wananchi ni usimamizi wa rasilimali za nchi yao.

Naama,naamini mapungufu yaliyopo kwenye katiba ya sasa yanaweza yasiwe takwa la kijamii kati ya Watanzania ila la kisiasa,lakini ni muhimu tukatambua kuwa jamii yote ya kitanzania ina inaustarabu wake,wakati wanasiasa wanakwenda kushoto,jamii ya kitanzania inaweza kwenda kulia kama ndio njia bora ya kulinda amani,kwa hiyo katiba mpya haiwezi ikawa ni hitaji la kisiasa pekee ilihali Watanzania uwa wanavumiliaga tu upepo mbaya unapopita,funika kombe mwanaharamu apite.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Uko Vizuri Kongole Kwako.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom