Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Naomba kuwapa pole Watanzania wenzangu kufuatia msiba huu mkubwa wa Taifa letu. Kifo cha Rais John J. P. Magufuli kumeacha ombwe na pia mafunzo kwa maisha yetu sote. Nimepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu. Vyovyote vile ilivyo, kama nilivyowahi kusema huko nyuma hakuna ombwe la uongozi Tanzania.
Tumewahi kuondokewa na Waziri Mkuu akiwa madarakani, Makamu wa Rais, mawaziri n.k Huu ni wakati wa mapitio yetu. Taifa litaendelea kuwa salama na kwa pamoja katika maombolezo yetu tuondoe utata wowote ule; mama Samia Suluhu Hassan ameandaliwa na ndio sababu amekuwa makamu wa Rais mara hizi mbili chini ya Magufuli.
Taifa liko salama mikononi mwake na tumwombee hekima, ujasiri, na kuthubutu anapoliongoza kupitia maombolezo ya kitaifa na hatimaye kushika usukani wa taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki mama Samia Suluhu Hassan
Amina.
WatanzaniaTukoPamoja.