Rais Samia jukumu la kuwafanya Watanzania wakukumbuke kwa wema lipo mikononi mwako

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,248
Awali ya yote Rais Samia Suluhu Hassan nikupongeze kwa kibarua kizito ulicho nacho cha kuhakikisha Tanzania na Watanzania tunapata maisha bora.

Wapo wanao kubedha, wapo wanao kukejeli, lakini tupo tunao kupenda kwa dhati ambao ukizungumza sauti yako inapenya hadi ndani uvunguni mwa mioyo yetu.
images (19).jpeg
Mh Rais tokea, tuondokewe na kipenzi cha Watanzania Marehemu aliekuwa Rais wa Tanzania mh JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, ni kama uongozi wako umeingiwa na ubaridi, ni kama vile una uogopa Urais, ni kama vile uamini kuwa wewe ndio kiongozi MUANDAMIZI wa Tanzania na vyote vilivyopo, watu, madini, wanyama.
Tanzania yote ipo mikononi mwako,

Hali iliyo kupata huwapata watu wote waliofiwa na watu wao wa karibu, kuna kipindi unaweza ukakaa ndani ukahisi kama una muona ndugu yako alie kutoka.

kuna muda unaweza ukapita sehemu mlizokuwa mnapenda kwenda pamoja ukahisi kama upo nae.

ni Mapenzi ya dhati ndio hutufanya tuhisi kama ndugu zetu walio tutangulia mbele za haki kama bado tunao na pengine wanatuona.

KIFO ni FUMBO ambalo hakuna anae weza kulifumbua na sisi binaadam huwa na kasumba ya kuto kuridhika hivyo hata kama mtu atakufa normal death bado kuna mtu atahisiwa uchawi...!

Kwa kifupi sisi wote ni Marehemu watarajiwa, kitacho tutofautisha ni muda wa kuondoka na aina ya vifo tu.
images (20).jpeg
Nikukumbushe tu Mh Rais hakuna KIFO kinauma sana kama cha familia kumpoteza BABA, lakini haiwezi kufanya maisha mengine yasiendelee. wapo wakina mama ambao walifiwa na waume zao wakaziogopa nyumba zao mwisho wa siku waliizoea hali.

Maisha yakaendelea wakawalea watoto wao bila BABA. bado maisha yaka wanyookea lakini zipo familia ambazo zilipoteza uelekeo baada ya BABA kufariki ina hudhunisha sana. sitaki kuamini kuwa baada ya sisi kuondokewa na JEMEDARI wa vita Mh Dk, Joseph John Pombe Magufuli. basi kila kitu kiyumbe.

Binafsi naamini nchi yetu ina mifumo rasmi ya kiuongozi ambayo kiongozi yeyote lazima akabidhiwe aifuate. kwa cheo chako sio lazima ufuate mfumo huo unayo nafasi ya kufanya mageuzi makubwa ukauthibitishia Ulimwengu kuwa wanawake mnaweza.

Mh Rais, nchi zetu za Afrika ile kasumba ya mfumo dume huwa inadhoofisha sana utawala wa wanawake, kwa ufupi ukiacha kuwa wanawake hampendani wenyewe kwa wenyewe natural lakini wanaume awapendi kuongozwa na Wanawake.

Ndio maana hakuna historia ya mwanamke kugombea Urais kwenye nchi zetu za afrika akapata ukiacha mh SALHA WORK ZEWDE Ambae alichaguliwa na bunge la nchi yake ya Ethiopia.

Wanaume wote waliokuzunguka awajapendezwa na wewe kuwa kiongozi MUANDAMIZI kuwazidi wao, hivyo usipo fanya uamuzi kama Rais lazima wata kudhoofisha ili uonekane hufai.

Mwenyezi Mungu akupe matumaini, akupe nguvu na ujasiri. watanzania tunahitaji matokeo bado unao muda wakufanya mageuzi ukabaki kuwa kipenzi cha Watanzania lakini hilo litawezekana ikiwa utaamua kuziba masikio na kufumbua macho.

Masikio hayana uwezo wa kuzuia kila kelele ila macho yanaweza kuzuiwa kuona baadhi ya vitu. hivyo ziba masikio maana kuna watu wamekuzunguka wana kupigia kelele ambazo zitakutisha mwisho wa siku utakiogopa kiti chako cha Thamani.

Fumbua macho uone nini Watanzania tunataka tufanyie kwa haki na upendo sisi Watanganyika tutakupenda na kukulinda daima.

Tunataka

1. KATIBA mpya na tueleweshwe kifungu kwa kifungu.

2. Tunataka elimu bora na sio bora ELIMU.

3. Tunataka Ajira zisizo na upendeleo hili Jakaya Mrisho Kikwete alilimudu ila JEMEDARI Mh Rais John Joseph Pombe Magufuli alifeli😭😭😭

4. Tunahitaji utufutie wimbo wa ELIMU, BARABARA, UMEME & MAJI kwenye kampeni zenu wimbo huo tumechoka kuusiliza tukea tuna pata uhuru wimbo ni ule ule...!

5. Watanzania tunataka tuwe na maamuzi asilimia 100 kwenye Rasilimari zetu.

6. Nchi hii ni ya Watanzania wote na sio ya viongozi wachache tunahitaji maamuzi ya kila kitu yatoke kwa Wananchi na sio kwa viongozi.

yapo mengi ila kwa leo naomba niishie hapa...nakupenda sana Mh Rais, nakuombea dua njema. na nina kushukuru sana kwa uongozi wako uliotukuka.


soma zaidi hapa.....

Naongea na Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Viashiria vyote vinaonyesha pasi na shaka kuwa hicho kiatu kwake ni oversize! Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
sidhani ujue kiongozi kwa nchi zenye katiba nzuri...Urais hata wewe una uweza kwasababu Rais anaishi kwa kufuata taratibu za nchi...

kuna ugumu gani kufuata script...?​
 
Back
Top Bottom