issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205



Mama Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) amesema kuwa anawaomba wafanye kampeni kwa amani wakipita wawasikilize wala wasigombane nao.

Amesema kuwa wapo wagombea watakwenda kuwaambia kuwa walivunjwa miguu na mwingine alimsikia akisema kuwa alipigwa risasi 16.

''Watakuja kuwaambieni wamevunjwa miguu lakini waulizeni ilikuwaje wakavunjwa miguu, wengine jana nilisikia mmoja anasema amemimiwa risasi 16 nataka niwaambie huyo sio askari wetu wa serikali ya chama cha Mapinduzi, askari wetu akipiga mtu tatu akamkosa atawajibika sikwambii askari aliefundishwa akapiga 16 huyo mtu atoke mzima".
 
Hapo kasema ukweli mtupu Maana yeye ndo miongoni mwa maboss wa Askari wao wa CCM hivyo anawajua vizuri weredi wao. Kwahiyo Mimi naamini alichokisema na ndo uhalisia.

Zitto aliutaka uenyekit wa chadema akafukuzwa Chama.
Ben sanane aliutaka uenyekit wa Chama akapotea mpaka leo.
Tundu lissu aliutaka uenyekiti wa Chama akapigwa na vitu vinavyosadikika ni risasi.
F. SUMAYE aliutaka uenyekiti wa Chama akaambiwa kuwa Sumu haionjwi kwa usalama wa maisha yake akaamua kujiweka pembeni na kuchomoka kwenye himaya za mtia Sumu.

Swali; kwanini Kila anaeutaka uenyekiti wa Chama CDM anapatwa na matatizo Ni ipi Siri iliyopo Hapo nyuma?

Je nikweli Mbowe Ni kibaraka wa serikali kwamba hawezi kutoka kwenye kile kiti kwa masilahi ya Taifa?
 

Tumwambie tu huyu mke wa Coplo wa zimamoto kuwa wauaji waliowatuma kumuua Lissu hawakumkosa, walimpata, walimimina zaidi ya 30, na zote zililenga pale pale anapokaa Lissu kwa upande wa ndani. Hongera huyo askari kaiva kwenye shabaha.
Mliwatuma wakatekeleza maelekezo.
Ila hata siku moja shetani hajawahi kumzidi Mungu!
Nilikuwa nakuona ww mama mstaarab umekaa kimya haufungamani na hao wenzako, kumbe ulikuwa umeficha makucha, Lissu mliyomtwanga marisasi ya kutosha Mungu akasema no, huyu mtu ni mpango wangu, ni lazima aishi! Mna roho mbaya sana ninyi watu, sijui mwanamke gan ww, hukuzaa??
 
Back
Top Bottom