Shaka: 2025 Mgombea Urais wa CCM ni mmoja tu Rais Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania na Rais Mwinyi kwa Upande wa Zanzibar "Case Closed "

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,530
2,141
IMG-20221120-WA0105.jpg

Wale wanachama wote ndani ya CCM wanaounyatia Urais wa Samia 2025 watafute kazi ya kufanya kwani kwa kauli hii ya Msemaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka naona "Case Close " Wanaobwabwaja na kukejeli kazi nzuri za Rais Samia Suluhu Hassan ujumbe huu uwafikie wote kwani fomu ya Urais ni moja tu kwa Bara nayo ni kwa Rais Samia na moja nyingine nayo ni kwa Rais Mwinyi kwa Zanzibar,

========

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza katika uchaguzi kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, ni salamu za kukubalika kwa Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, amesema umati huo wa wanachama ni salamu za historia mpya katika kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2024 na 2025 kwa kuwa viongozi watakaopatikana mwaka huu ndio wanaokwenda kukiongoza Chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Magharibi katika ukumbi wa Banquet mjini Unguja.

“Viongozi hao wa Chama wa mikoa ndio watakaotoa mwelekeo wa ushindi wa CCM 2024 katika uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara na 2025 uchaguzi mkuu kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Shaka alisema kuwa CCM bado chaguo la umma kwa kuwa ni madhubuti, chenye muundo bora, mtandao mpana, viongozi imara, sera nzuri na kubeba matumaini na matarajio ya wananchi.

Alisisitiza kwamba mwitikio wa wanachama wa CCM kujitokeza kuomba uongozi umekuwa mkubwa kuliko wakati wowote katika historia ya Chama.

Kwa mujibu wa Shaka, mwitikio huo ni kielelezo cha kukubalika, demokrasia pana na utendaji haki ndani ya Chama pamoja na imani kubwa waliyonayo wanachama kwa uongozi wa Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, alisisitiza kuelekea 2025 Chama kwa mujibu wa utaratibu na utamaduni wake hakina mpango wa kupata wagombea urais wengine kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala yake kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuendeleza umoja, mshikamano na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ili itekelezwe kwa viwango kama ilivyoahidiwa kwa wananchi.

“Tabia na utamaduni huu wa kuahidi na kutekeleza umeendelea kuifanya CCM kutokuwa na mpinzani katika siasa za ushindani. Wanachama wa CCM fanyeni uchaguzi wa viongozi kwa sifa na uwezo wa kuongoza kwa maslahi ya Chama na nchi yetu,” alisema.
 
Halafu mbona ghafla sana!!
Mama Samia ndie Rais na ataamua mwenyewe aache au aendelee

Hawa chawa wanapokuwa wengi ndio yanaharibu utaratibu
 
Tusikubali Mama ayumbishwe Paskali, Tusimame kwa pamoja kwamba 2025 ni mama tena liwake inyeshe
 
Hahahahah..hamuwezi kuulazimishia umma wa wenye nchi yao zaidi ya raia milioni 60 rais mnayemtaka nyinyi. Urais mtu hapewi tu kwa hisani kama zawadi, eti afe mwenzako wewe ndio uuchukue urais kwa kuurithi na uung'ang'anie. Anataka awe rais 2025 on what merit? Kafanya kipi cha ku-warrant kupewa uongozi wa juu wa taifa 2025? Mtu ana uwezo mdogo hivi kila mtu anaona halafu apewe miaka 5 mingine ya kuharibu? Nani atakubali?
 
Wale wanachama wote ndani ya CCM wanaounyatia Urais wa Samia 2025 watafute kazi ya kufanya kwani kwa kauli hii ya Msemaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka naona "Case Close " Wanaobwabwaja na kukejeli kazi nzuri za Rais Samia Suluhu Hassan ujumbe huu uwafikie wote kwani fomu ya Urais ni moja tu kwa Bara nayo ni kwa Rais Samia na moja nyingine nayo ni kwa Rais Mwinyi kwa Zanzibar,

====
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza katika uchaguzi kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, ni salamu za kukubalika kwa Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, amesema umati huo wa wanachama ni salamu za historia mpya katika kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2024 na 2025 kwa kuwa viongozi watakaopatikana mwaka huu ndio wanaokwenda kukiongoza Chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Magharibi katika ukumbi wa Banquet mjini Unguja.

“Viongozi hao wa Chama wa mikoa ndio watakaotoa mwelekeo wa ushindi wa CCM 2024 katika uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara na 2025 uchaguzi mkuu kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Shaka alisema kuwa CCM bado chaguo la umma kwa kuwa ni madhubuti, chenye muundo bora, mtandao mpana, viongozi imara, sera nzuri na kubeba matumaini na matarajio ya wananchi.

Alisisitiza kwamba mwitikio wa wanachama wa CCM kujitokeza kuomba uongozi umekuwa mkubwa kuliko wakati wowote katika historia ya Chama.

Kwa mujibu wa Shaka, mwitikio huo ni kielelezo cha kukubalika, demokrasia pana na utendaji haki ndani ya Chama pamoja na imani kubwa waliyonayo wanachama kwa uongozi wa Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, alisisitiza kuelekea 2025 Chama kwa mujibu wa utaratibu na utamaduni wake hakina mpango wa kupata wagombea urais wengine kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala yake kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuendeleza umoja, mshikamano na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ili itekelezwe kwa viwango kama ilivyoahidiwa kwa wananchi.

“Tabia na utamaduni huu wa kuahidi na kutekeleza umeendelea kuifanya CCM kutokuwa na mpinzani katika siasa za ushindani. Wanachama wa CCM fanyeni uchaguzi wa viongozi kwa sifa na uwezo wa kuongoza kwa maslahi ya Chama na nchi yetu,” alisema.
Hajathubutu kusema hivyo. Mwenyewe anajua samia ni rais wa katiba tu. Uenyekiti ccm kapewa kwa desturi ya ccm kumpa nafasi hiyo kama rais anatoka ccm.
Demokrasia ndani ya ccm inadai mgombea urais ajaye wa ccm lazima apatikane kwa kuwepo uhuru kabisa kufuatana na katiba ya ccm. Lazima mama apitie mchakato kama hataki ushauri wa kutogombea. Wanamapinduzi ndani ya chama wanataka mwanamapinfuzi mjamaa aongoze chama na kua mgombea urais.
 
Hapa mtasubiri,Hii ni desturi hivyo lazima iwe otherwise Rais akatae mwenyewe
 
Hilo hua hawalifanyi ovyo ovyo tu ingekua ivo 2015 wangempitsha lowasa hua wanaangalia maslahi ya chama
 
Back
Top Bottom