Dkt Samia, Rais pendwa wa dunia; muasisi wa haki na uhuru wa pili Tanzania

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
132
541
DKT SAMIA, RAIS PENDWA WA DUNIA; MUASISI WA HAKI NA UHURU WA PILI TANZANIA.

Mimi ni mwanasiasa, ninaifanya Siasa kwa vitendo na sio kuisoma mtandaoni wala kuhadithiwa. Chama changu cha kwanza kujiunga nacho kilikuwa ACT wazalendo mwaka 2015 ambapo niliaminiwa nikawa msaidizi wa Mgombea Urais Marehemu Mama Anna Mghwira, ambapo nilikuwa namsaidia kuandaa hotuba zake na kusimamia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Baada ya uchaguzi Mkuu nikateuliwa na Chama hicho kuwa Afisa Habari wa Taifa na mwaka 2020 nikagombea Ubunge Jimbo la Singida Magharibi. Naishukuru sana ACT wazalendo na viongozi wake kwa kunilea.

Lakini 2020 Desemba 31, nikakoshwa zaidi na Sera na mienendo ya Chama cha Chama cha Mapinduzi. Narudia kwa msisikitizo Desemba 31, 2020 NIKAKOSHWA ZAIDI NA CHAMA CHA Mapinduzi, na sio mtu fulani kama "individual" wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kwa utashi wangu, na kwa kuzingatia haki zangu kama raia wa Tanzania zilizopo kwenye Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na marekebisho yake, NIKAHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM hadi sasa niandikapo Makala hii. Nakipenda sana Chama changu, na nafurahia mno Siasa zake. Nina amani tele.

Baada ya utangulizi huu ambao kimaantiki unanipa uhalali kuichambua Siasa kinagaubaga, naomba niwakaribishe katika Makala (ndefu kiasi) ila muhimu sana kwa kila Mtanzania mwenzangu kuisoma na kuielewa juu ya miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Kama wewe "Mhafidhina" mchukia Siasa Mpya za Rais Dkt Samia, na hupandwa "kiroho dunda" ukiona wafuasi wake (Chawa) tukimpongeza usitafune "malimao" vumilia, tusameheane maana ndio tafsiri sahihi ya kila Mtanzania kujimwaya na UHURU WA KUJIELEZA uliondikwa katika Ibara ya 18 ya Katiba yetu ya nchi ya mwaka 1977.

Machi 19, 2021 kwangu mimi ilikuwa siku ambapo Nchi yetu ya Tanzania ilipata Uhuru wa Pili ukiachana na ule wa mwaka 1961 kutoka kwa wakoloni. Ilikuwa siku ambayo si tu Tanzania kama Nchi ilibofya "reverse gear" kurejea upya "kiutekelezaji" wa kulinda tunu za Taifa, bali pia Chama Tawala cha Mapinduzi CCM kilibadili "gia angani" na kuikumbatia Katiba yake na miongozo ya waasisi ya kuanzishwa kwake. Niliona Tanzania yetu ikifanana kabisa na mtu aliyelala jana kipofu, na kuamka mwenye Macho ng'aafu yenye kuliona jua barabara.

Baada ya Machi 19, 2021, Kwenye vijiwe vya mitandao ya kijamii na hata ndani ya mitaa mbalimbali nchini, palisikika sauti kadhaa zikidai "huyu mama hataweza iongoza Nchi", sababu kuu ikidaiwa kwamba ni "Mwanamke" na namna "alivyo mpole" kwamba ni Sifa ambazo ni mbingu na ardhi na Sifa za Mtangulizi wake ambaye alijitanabaisha kuwa Mkuu wa Nchi aliyejipamba muda wote na "ukali kwenye sura hadi kwenye kauli zake" mithili ya nyoka "koboko" akiwasulubu watesi wake porini.

Hakika msemo wa wahenga "Mdharau Mwiba mguu huota tende" hadi sasa umewadhibu wote waliyomdogosha Mama huyu ambaye ndiye Mwanamke wa Kwanza Kuwa Rais Tanzania tangu tupate uhuru 1961 ambaye kupitia Falsafa yake ya 4R amefanikiwa kuibeba Nchi kwa wepesi kama karatasi bila shuruti kuifikisha "kaanani" ndani ya muda mfupi wa miaka miwili tofauti kabisa na wengi ikiwemo Kiongozi wa ACT wazalendo Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyewahi kudai patahitajika miaka 10 kuirejesha Nchi kwenye utulivu wa Kisiasa na Kiuchumi kama ilivyokuwa awamu ya 4 ya Rais Dkt Jakaya Kikwete.

Utekelezaji wa Falsafa ya 4R (Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya) umekuwa tiba dhidi ya vidonda, upendo dhidi ya chuki, furaha dhidi ya karaha, haki dhidi ya dhuluma na kubwa zaidi "uhuru" dhidi ya "utumwa wa kifira na kimamlaka" baina ya Mtawala mweusi na raia wake weusi ndani ya Tanzania ya Afrika huru.

Falsafa hii inanitafakarisha huenda kwamba Muasisi wake, Rais Dkt Samia Suluhu alipata maono kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia vitabu vyake vitakatifu ikiwemo cha Bibilia Wakorintho 13:4-7 ambayo kwa "acknowledgement" nilitumiwa kwenye group la WhatsApp na Classmates wangu tuliosoma nao Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Fine And Performing Arts "FPA" ambapo mistari hiyo inasema;

4) Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.

5) Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya.

6) Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli.

7) Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

Na katika kuienenda kwa vitendo imani hii, akiwa anafahamu Siasa ndio usukani uendeshayo kila tumaini na tamanio la maisha ya mwanadamu, Rais Dkt Samia alifanya na ameendelea kufanya mageuzi lulu ya kisiasa kama sehemu ya kuifungua na kuiponya Nchi.

Kwenye maisha naamini kila ujio wa tatizo ama changamoto una kheri ndani yake iliyojificha, mathalani; mimi baada ya kumaliza darasa la saba Shule ya Msingi Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, nilianza kufanya biashara ya kuku na mbuzi. Siku moja likanijia wazo la kutoroka nyumbani kwenda Arusha "kutafuta maisha" kwenye sekta ya Utalii, siku moja kabla ya kuondoka, mwanakijiji mmoja akanijia akilia shida ya dharura akinibembeleza aniuzie mbuzi wawili kwa bei rahisi.

Nikaona hili hilo ni "zali ya mentali" nikawanunua, kumbe walikuwa mbuzi wa wizi, kesho yake nikakamatwa na "migambo" hadi ofisi ya Kijiji, katika utetezi, kwakuwa Serikali ya Kijiji iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Mzee Kiwesi Daghau ilikuwa inanifahamu mimi na Familia yangu hatuna hata chembe ya historia ya wizi wala kumdhulumu mtu, basi iliamuru nielewane na Familia miliki ya hao mbuzi, ambapo niliwarudishia mbuzi wao na fidia.

Na ndoto yangu ya kutorokea Arusha (ambayo kwa wakati huo ilikuwa fasheni) ikafia hapo kwani mtaji wangu na hela za ziada ulitafunwa wote, but here comes a glorious news:- wiki mbili mbele, matokeo ya Darasa la Saba yakatoka nimefaulu. Naam ingawa nilijua nitafaulu kwakuwa darasa la kwanza hadi darasa la 7 kwenye mitihani ya Shule nilikuwa nashika namba moja na nikiteleza kidogo namba mbili, namba 3 nimeshika mara moja tu. Hivyo nikapangiwa na nikaendelea na Masomo ya Sekondari, Shule ya Puma, Ikungi Singida.

Mfano huu wa KUTAPELIWA ili NIENDE SHULE naufananisha na ujio wa Mtangulizi wa Rais Samia, Hayati Magufuli kwamba licha ya wengi nchini na hata Mataifa mengine duniani kumzodoa vikali Enzi zake ikiwemo mimi kupitia mitandao ya kijamii, na kuutafsiri uongozi wake kama Uongozi wenye nasaba na "udikteta" na usiooana na "maendeleo ya watu bali maendeleo ya vitu", lakini tutamkumbuka kama Mkuu wa Nchi aliyetukumbusha BILA KUPENDA, kupitia Utendaji wake wa kiimla umuhimu wa Tanzania na nchi yeyote duniani kuwa na mifumo ya imara ya HAKI, UHURU na MAENDELEO SHIRIKISHI yanayomtanguliza mbele mwananchi ambaye ndiye Mwenye Nchi badala ya kutanguliza "maendeleo ya vitu" na kuwaacha watu taabani kimaisha.

Fundisho hili adhimu lenye kubeba Elimu ya HAKI, UHURU na KUJITAMBUA "Self Esteem" si tu limeishia kwa Nchi, bali pia hata kwenye vyama vyote vya Siasa nchini hususani Chama cha Mapinduzi CCM limeingia mioyoni haswaa. Asante Hayati Magufuli.

Kuna VIGWEGWE WA KISIASA kutoka Vyama vya Upinzani ambao tukimpa kongele Rais Dkt Samia kwa kutuletea mageuzi pendwa, wanazodoa wakihoji kwamba "kwani aliipokea Nchi akiwa chini ya Chama Cha Upinzani"?, na kuna "vigwegwe wa Kisiasa" ndani ya CCM yetu ambao pia tukisema "Mama ana upiga mwingi" wanazodoa hivo hivyo kwamba tunamchonganisha na Hayati Magufuli, kana kwamba ni uhaini kujadili madhaifu ya awamu ya 5 yaliyorekebisha na awamu ya Sita...!!

Who said so!!? Tujadili.

Look!!

Chama cha Mapinduzi CCM ni Chama bora kuliko cha Siasa Afrika na hata duniani ndio maana hata sasa Kipo hai na hakuna wa kukiondoa, angalia Katiba yake, Sera, Ilani Historia na Miongozo yake, vyote vinazungumzia HAKI, UHURU na Maendeleo ya watu, hivyo ieleweke madhaifu ya mwanachama wake aliyepewa ridhaa ya kuongoza katika nafasi yeyote ile, ni madhaifu yake, na kila mwanachama wa CCM ana haki na wajibu kumsahihisha, na kuhakikisha madhaifu hayo hayajirudii kwa manufaa ya Chama na Taifa, na ndio maana ahadi au imani ya Chama ukiangalia hata kwenye kadi ya uanachama pameandikwa nanukuu:

Chama kinaamini kwamba:-

a) Binadamu wote ni sawa
b) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthamini utu wake

Sasa tujiulize Kiongozi Kinara wa kueneza chuki, uadui, utengano, utumwa baina ya watu wake huyo ni mwanachama wa shujaa wa Chama cha Mapinduzi CCM? Anastahili kuenziwa? Rais Dkt Samia anatii na kuitekeleza Imani ya Chama cha Mapinduzi bila kumumunya maneno wala kupindisha vitendo, tukimpongeza nongwa? Hebu kaeni kwa utulivu wahafidhina.

SIASA SAFI.

Rais Samia ameikuta Nchi imetamalaki Siasa zilizojaa uadui na chuki zilizopitiliza. Nani ambaye hakumbuki ulishajengwa utamaduni Mpya kila mwenye Chama tofauti na wewe ni adui wako? Kila apandae jukwaani ni kueneza HATE SPEECH inayoambatana na vitisho vya kuuana dhidi ya wanaopingana na misimamo ya Chama chake? Na viongozi wa Chama na Serikali wanabariki kauli hizo ovu zinazokizana na Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa?

Nahoji nani asiyekumbuka Ulinzi na Usalama wa mwanasiasa na Mwanaharakati uliondoka kutoka kwenye mikono ya dola salama na kumilikiwa na kundi ovu mithili ya Alshabab lilioitwa "watu wasiojulikana"?

Nani asiyekumbuka Wanasiasa wenye heshima kubwa katika nchi kama akina Mzee Kikwete, Mzee Makamba, Membe, Ridhiwani Kikwete, Nape Nnauye, Tundu Lissu, Zitto, Mbowe, Maalim Seif na wengine wengi walifanyiwa "Defamation" wazi wazi bila Soni wala haya na kutweza utu wao na akina Musiba na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa na si tu na Chama Tawala wala Serikali?

Hamkumbuki hata mimi Suphian niliandikwa nafanya mapenzi ya Jinsia moja (Shoga), kwamba eti nafanya ushenzi huo na Wanasiasa Zitto na Hayati Maalim Seif? Kisa tu napingana na Utawala uliokuwa unasigina Katiba ya nchi, Demokrasia na Haki za Binadamu!!? Mnadhani Mwanamke wangu, Wazazi wangu, rafiki na jamaa zangu walijisikiaje?

Nani ambaye hakumbuki ilikuwa dhambi kubwa ya hata kufutwa uanachama ikibainika mwanasiasa wa Upinzani na na mwanachama wa Chama Tawala kuonekana hadharani wakishiriki jambo la kijamii au hata tu kutakiana kheri ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii au hata kukutwa wanakunywa kahawa pamoja kijiweni?

Nauliza nani amesahau habari za kila uchwao za wanasiasa, Wanaharakati na Waandishi kutekwa, kubambikizia kesi, na hata kuuawa na hakuna taarifa ya watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya Sheria? Kichaka kinabaki tu "uchunguzi unaendelea"..!!?

Nahoji nani hakumbuki vyama vya Siasa vilipigwa "stop" kufanya mikutano ya hadhara kinyume na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na marekebisho yake na Katiba ya nchi iliyopo? Nani hakumbuki huko majimboni wabunge walikuwa wanatumia hadi vyombo vya Ulinzi na Usalama kutishia, kupigana ngumi hadharani na kuwakamata wagombea au wanasiasa kutoka vyama tofauti na vyao? Mimi mwenyewe nilishawahi kufuatwa na Polisi zaidi ya mara nne kwetu Kijijini Minyughe kwa agizo la OCD aliyepewa agizo na Mbunge kisa tu nafanya Shughuli zangu halali za kisiasa... Imagine!!

Nahoji mazingaombwe yote haya ya Kutekana, kubambikiziana kesi, kumchafuana, kutwezana utu yanapatikana katika ibara gani ya Katiba yetu? Katiba gani ya Chama cha Siasa? Sheria gani ya nchi? Ilani, Sera na Miongozo gani? Kama sio roho binafsi ya Kiongozi na genge lake aliyekengeuka kufuata Katiba ya Nchi na Katiba ya Chama chake...!!? Tumsifie? Chama kimtetee? Rais Samia amtetee? Aisee HAPANA abebe tu "zigo lake la Mavi" daima.

Rais Dkt Samia amekuja. Akaenenda katika Katiba, Sheria na Ustaarabu wa Kitanzania, Miaka miwili yake Ikulu hatujasikia mwanasiasa, mwanaharakati wala Mwanahabari ametekwa, amebambikiziwa kesi, amepigwa risasi, amehojiwa uraia wala kuuawa badala yake sote tunakunywa kahawa, tunahoji, tunakosoa Serikali hatufungwi, tunafanya mikutano ya hadhara na wala hatuonani maadui kisa tuna vyama Tofauti. Sote tunalindwa sawia na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Sio hivyo tu, Mhe. Rais Samia amekubali Sheria zote kandamizi za kisiasa kwenda kurekebishwa kama sio kufutwa kabisa, pamoja na kukubali Mchakato wa kuunda Katiba Mpya kuanzishwa ili kuruhusu mazingira ya Uhuru, Haki na aminifu ya ushindani wa kisiasa baina ya vyama vya Siasa kama ambavyo Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 inavyoelekeza.

DIPLOMASIA NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA.

Miaka miwili ya Uongozi wa Rais Dkt Samia amefanya ziara zaidi ya 10 sasa nje ya nchi na kufanikiwa kuikutanisha Nchi na dunia na kuifungua Nchi kimahusiano ulimwenguni na kukaribisha fursa lukuki za kiuwekezaji na kibiashara, Kitendo ambacho ni kinyume na hali aliyoikuta ya miaka 7 nyuma ambapo Rais wa Nchi hakuthubutu kuvuka mpaka wa Afrika, na badala yake alisifika kutunushiana misuli na Mataifa makubwa duniani suala ambalo liliikosesha Nchi yetu mapato na fursa nyingi duniani.

Ilikuwa na suala la ajabu kuamka asubuhi kutoona habari hasi ya Tanzania kusemwa vibaya na vyombo vya habari na Taasisi za Kimataifa kwamba Rais anainajisi Demokrasia, Uhuru wa Kujieleza na Haki za Binadamu. Leo hii hali ni shwari, tunasemwa vizuri kila uchwao, Wawekezaji Wanamiminika kutoka nje kuja kuwekeza Tanzania. What a good news!!? Hakuna kama Mama!!

Kwa mfano katika uwezekaji na biashara, Wiki tatu baada ya ziara ya Mhe. Rais Samia nchini Misri, wafanyabiashara 111 kutoka nchini humo wamekuja Tanzania kuangalia fursa za kibiashara na uwezekaji.

Aidha Mahusiano haya adimu yamechagiza ukuaji wa Kila Sekta nchini, kwa mfano Sekta ya Utalii imekuwa kwa kiwango kisichomithika kwani wageni wengi wameshawisha kuja kwa wingi kutokana na Sera rafiki ya Utalii, Mazingira mazuri ya kisiasa na mchango wa Filamu ya ROYAL TOUR ambayo Rais Samia aliamua kujishusha kuwa TOUR GUIDE bila kujali cheo chake nyeti katika nchi cha Urais. Leo hii ukienda Ngorongoro, Serengeti hakuna tofauti kati ya LOW SEASON na HIGH SEASON , zote ni HIGH SEASON kwa maana kuna mafuriko ya watalii.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idadi ya watalii kutoka nje ya nchi waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika kipindi cha Januari hadi Mei 2022 wameendelea kuongezeka hadi 458,048 ikilinganishwa na watalii 317,270 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni sawa na asilimia 44.4. Wondrous!!

Aidha kwenye Sekta hii kama ilivyo kwenye sekta zingine, Serikali imekuwa Sikivu kupokea maoni boreshi, mathalani mimi Suphian kama raia mwaka jana 2022 nilikuwa na mradi wangu wa Utalii kusapoti ROYAL TOUR ya Rais Samia na katika kutembelea vivutio mbalimbali alivyotembelea nikabaini watalii wengi wanalalimikia changamoto ya huduma ya mawasiliano ya Internet na hivyo kuandika barua kwa Mawaziri husika kutatua jambo hili kuwapa haki ya taarifa watalii.

Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri wa Habari Mhe. Nape Nnauye alizindua mtambo wa Internet Mlima Kilimanjaro, na kutangaza kwamba Serikali ina endelea kusimika na kuboresha huduma hii katika vivutio vyote nchini.

AJIRA.

Miaka miwili ya Rais Dkt Samia, Serikali imeajiri mara tatu kuliko utaratibu wa kawaida wa Serikali wa kuajiri mara moja kila mwaka, hii ni nje ya ajira zisizo rasmi ambapo vijana wengi wameajiriwa kwenye Miradi mikubwa ya kimkakati. Imagine Mama ametenga zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya Ajira mpya 32,604. Hii ni kinyume kabisa na hali aliyoikuta ya Serikali kukataa kuajiri tangu mwaka 2016 na kusababisha maelfu ya wahitimu kuwa ombaomba majumbani na wengine kujiingiza kwenye vitendo ovu.

Aidha Rais Dkt Samia katika kuwajali watumishi wa Umma, mapema tu alipoingia madarakani, ameongezea mishahara watumishi kwa 23%, akawapandisha madaraja na kulipa malimbizo yao, huku akiboresha mazingira ya kazi ikiwemo kujenga ofisi zao na kununua vifaa vya kazi, mambo ambayo kwa hakika hayakufanywa na Mtangulizi wake kwa miaka takribani 7.

Kwa upande mwingine Rais Dkt Samia akitambua Serikali inawajibu wa kutengeneza mazingira shirikishi na rafiki kwa vijana wanaoanza biashara, pamoja na mambo mengine ametoa kibali wanaoanzisha biashara kutodaiwa kodi hadi biashara zao zifikishe umri wa miezi Sita hadi mwaka mmoja ambapo angalau zitakuwa zimezaa faida. Huu uamuzi haukwepo kwa miaka yote nyuma kabla ya awamu yake.

Kwa upande mwingine pia Rais Dkt Samia hajawapa kisongo vijana wasomi, kwani pamoja na kuboresha mazingira ya kusomea shuleni na vyuoni, kutoa kibali cha Elimu bure kutoka Shule ya Msingi hadi Kidato Cha Sita, Mama ameongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu (Boom) kutoka Tsh. 8,000 kwa siku kabla ya kuingia madarakani hadi Tsh 10,000 kwa siku na kutoa jumla ya Shilingi Bilioni 84 kwa wanafunzi 42,000 waliokuwa na changamoto ya mkopo wa Elimu ya Juu. Nani kama Mama??

UCHUMI.

Katika Uchumi sote tunafahamu kwamba Rais Dkt Samia ameipokea Nchi ikiwa na Uchumi ukiwa na nyufa nyingi kwasababu ya "Approach" zisizo rafiki za kukuza Uchumi kama vile kutumia "Cash" kuendesha miradi mikubwa ya kimkakati na kusababisha mzunguko finyu wa fedha mtaani na ndio maana wananchi tulikuja na kauli ya "vyuma kukaza", lakini pia sakata la korona na vita vya Russia na Ukraine..!!

Pamoja na gunia hili la msumari katika Uchumi, Rais Dkt Samia hakulikimbia mithili ya Mama yake Elizabeth 2 wa Uingereza aliyekataa kuhama Uingereza vita vya Pili vya dunia kama ambavyo familia za aina yake "ROYAL FAMILY" wangejihami, alipambana, na kutia moyo askari na viongozi wenzake hadi wakamshinda Hitler, vivo hivyo Rais Samia hakutaka kukimbia matatizo ya kiuchumi, ameyadhibiti kwa kutumia "akili" kwa kushirikiana wataalam ikiwemo kutotumia Fedha taslimu kuendesha miradi mikubwa ya kimkakati badala yake amekopa tena mikopo ya riba nafuu sana, ameweka nguvu kwenye Miradi ya kuzalisha ajira, ameweka sera rafiki za uwezekaji na kuwatoa hofu wanyabiashara tofauti kabisa na enzi za kabla yake ambapo Wawekezaji na Wafanyakazi wa ndani na nje walikuwa hawana uhakika na mikataba yao maana Mkuu wa Nchi alikuwa anaweza wa kukuita leo, kesho akavunja mkataba.

Aidha katika hali ya kustaajabisha, ukiachana na maongezeko ya bajeti ya kilimo ya miaka miwili iliyopita, katika mwaka huu wa fedha Rais Samia ameiongeza bajeti ya kilimo inayotegemewa na zaidi 80% ya Watanzania kutoka Bilioni 294 mpaka Bilioni 900 bajeti ambayo haijawahi kutokea tangu tupate uhuru, huku akifuta ruzuku katika mbolea na mbegu, na kuhamasisha wananchi kulima kilimo cha kisasa na huku akiwahakikishia masoko bora ndani na nje ya nchi.

Kwa werevu huu wa kiuchumi, Rais Dkt Samia amepambana hadi kufanikiwa kuukuza Uchumi wa Tanzania ulidorora kwa kuongeza Ukuaji wa Pato la Taifa katika robo ya pili ya mwaka 2021 kwa 4.3% ukilinganisha na 4% mwaka 2020.

Mambo ni mengi ameboresha Mheshimiwa Rais, hapa nimetaja machache sana na ameonesha nia ya kuendelea kuboresha na kuanzisha vipya vya neema, hivyo nawaombeni Watanzania wenzangu tumuunge mkono, tuamini katika yeye, tupendane licha ya tofauti zetu za kiitikadi, tufanye Siasa Safi, tutangulize maslahi mapana ya nchi.. Mengi mazuri yaja chini ya Rais Dkt Samia.

Hakika Rais Dkt Samia ndiye ROLE MODEL wangu wangu na ROLE MODEL wa wengi katika Siasa duniani. Mpenda DEMOKRASIA na MWANADIPLOMASIA wa kweli. Hii ndiyo aina ya Siasa niipendayo, na bila shaka wengi tuipendayo, Siasa ya Ushawishi na siyo Siasa ya unyang'anyi. Rais Dkt Samia hakika ndiye Mzalendo halisi wa Nchi Mwenye kuoanisha kauli zake njema na matendo yake mema. Kheri imtawale atuvushe salama hadi 2030.

Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu ibariki Tanzania

Suphian Juma Nkuwi,
Kada wa CCM,
Singida,
Machi 17, 2023
Simu: +255717027973

FB_IMG_1679119486277.jpg
IMG-20230318-WA0000.jpg
 
Umeandika story ndefu isiyo na tija yoyote. Nikujuze tu mtoa uzi, wewe wala siyo mwanasiasa bali ni mganga njaa mzuri, hata huko CCM kilichokupeleka si ubovu wa sera za huko utokako bali ni uroho wa madaraka na hizi nyuzi ni kujitangaza ili wakuone!! Pole Sana lakini ukipunguza uchawa jina lako litaandikwa kwenye miongoni mwa...
 
Huyu jamaa nilipishana naye hapa Dodoma mida ya usiku akiwa na mjibaba mmoja katika pozi ambalo si la kawaida, kuuliza nikaambiwa huyu jamaa ni shoga maarufu tu, sasa na hapa nimeangalia jinsi alivyokaa kuanzia macho yake, pua mpaka akili zake, Nakiri kuwa nimethibitisha kwamba huyu jamaa anafanya biashara chafu ya kuuza kinyeo hasa kwa viongozi.
 
Huyu jamaa nilipishana naye happ Dodoma mida ya usiku akiwa na mjibaba mmoja, kuuliza nikaambiwa huyu jamaa no shoga maarufu tu, sasa na hapa nimeangalia jinsi alivyokaa kuanzia macho yake, pua mpaka akili zake, Nakiri kuwa nimethibitisha kwamba huyi jamaa anafanya biashara chafu ya kuuza kinyeo hasa kwa viongozi.
Liko wazi
 
Rais msikibu na muungwana haijawahi kutokea.

Anaupiga mwingi!

Jiwe ziii!!!!
Legacy hoi!
Kumbukizi ya jiwe chali!!!
 
Huu ndiyo ukweli wenyewe ukifanya mazuri utasemwa kwa mazuri, hakika sioni anayetosha 2025,zaidi Dr. SAMIAH.
 
Wewe Juma huna cha kuwambia watu wanaokujua. Ni njaa tu zinakutuma.

Ni mwasisi wa haki na uhuru. Mbona ulikuwa unawashabikia hao waliotowesha haki na uhuru ukawaita ni wazalendo?

Uteuzi hupati maana kila mtu anakujua unafanya hivyo kwa unafiki tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom