Aiseeee....wamejitahidi kubana bajeti, kuna mwaka SEIJII alisema wametumia 1.2trilion
 
Mi nashauri wangeuzindulia pale mlima Kilimanjaro ili watalii waongezeke. Wangeweka kwenye ratiba kile kipindi ambapo watalii wanakuja jwa wingi huku ndo wauwashe hivyo mtalii akianza kuoanda mlima anajua kileleni anakuta kuna mwenge mubashara
 
Habari wadau!

Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.

Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.

Nini faida yake?

Kimsingi, Mwenge unatumia gharama kubwa mno, kiasi kwamba fedha hizo zingetumika kufanya shughuli za maendeleo, baadhi ya kero kwa wananchi ama zingekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.

Inashangaza kuona kuwa Mwenge ule ulikabidhiwa katika eneo la shule ambayo haikuwa na madawati.

Njia nzima katika Wilaya ya Manyoni, Singida, tangu tumepokea Mwenge, shule zote njiani wanafunzi walikuwa wamejipanga barabarani, hawakusoma siku hiyo. Lakini hata Mwenge haukusimama njiani.

Wananchi wa Lusilile na vijiji jirani waliniambia kuwa kulikuwa na msako maalumu kwa wananchi watakaokiuka kuhudhuria mbio za Mwenge, hivyo walilazimika kujipanga barabarani tangu asubuhi na baadaye kupigwa na jua kali, njaa na kiu zao hadi Mwenge ulipopita.

Wapo waliolazimishwa kucheza ngoma ili ionekane wanaufurahia Mwenge. Kifupi, wapo wananchi ambao hawakufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuheshimu amri ya kuhudhuria mbio za Mwenge

Hata hivyo, katika mbio za Mwenge, Mwenyekiti wa CCM na katibu wake, pamoja na viongozi wa Umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) ni watu wa kuheshimiwa kuliko hata askari wa cheo cha juu.

Kuna bajeti ya kuweka mafuta gari ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa CCM, wa UWT, na UVCCM, japo wanahadaa kuwa Mwenge ni wa kitaifa. Ni uongo, kuthibitisha hili, huwezi kuona popote risiti ya mafuta kwa magari ya wenyeviti wa mikoa wa TLP, NCCR, CUF, CHADEMA, NLD.

Kichefuchefu kingine ni kwamba kuna fungu la kununua nguo za mapokezi ya Mwenge, zipo tofauti kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya katibu tawala wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya Ofisi ya TAKUKURU, ofisi ya Usalama wa Taifa na viongozi wengine.

Pia unakuta kuna sare za mapokezi ya Mwenge zingine za kimbizia Mwenge. Fungu la suti hizo zilitosha kununua madawati kwa ajili ya darasa moja la shule waliyoenda kukabidhiana Mwenge ambayo haikuwa na madawati.

Mwenge unatembezwa na kaulimbiu za “kumulika wezi na wala rushwa,” nilishtuka zaidi tulipokuwa Manyoni Mjini, ukarabati wa mnara wa Mwenge, mnara ambao umejengwa miaka mingi huko nyuma, mnara ulipigwa rangi na kuandikwa kaulimbiu ya “Tumethubutu, tumeweza, na Tunasonga mbele” kwa gharama ya Sh. 2.5 milioni. Haiingii akilini. Watanzania tuache kuhalalisha wizi wa kimachomacho kama huu.

Mwenge ni nini? Kwanini unatumika kama alama katika mavazi na kadi za UVCCM? Mwenge una msafara mrefu kuliko hata msafara wa rais?

Katika msafara wa Mwenge, kuna kundi kubwa la askari polisi, sijui wote hao wanalinda nini? Hivi katika Tanzania nani anaweza kuwa na wazo la kuiba Mwenge? Na akiuiba ataufanyia nini?. Polisi wanaolinda Mwenge wapo makini zaidi kuliko hata wale wanaolinda benki.

Tunaambiwa wanaangalia usalama wa Mwenge, je Mwenge huwa unaugua? Mwenge unaweza kuwekewa sumu? Mwenge na TAKUKURU au uhamiaji zina uhusiano gani? Mwenge na mkuu wa Magereza, vina uhusiano gani? Mkuu wa gereza anahusika na wafungwa, je kwenye Mwenge kuna wafungwa? Mwenge na Uhamiaji lini na wapi? Mwenge na Jeshi la Wananchi ambalo jukumu lake ni kulinda mipaka, lini na wapi na kwa nini? Wote hawa wanalipwa pesa kuhalalisha mbio hizi.

Hivi hatuwezi kufungua shule mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kupanda miti mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kuzindua majengo mpaka Mwenge upite. Miaka zaidi 50 ya Uhuru tumegandamizwa kiakili na Mwenge, kwanini?

Hakika Mwenge sasa unaunguza wazalendo, unanyonya wanyonge, unanyanyasa walipakodi. Unamaliza fedha lukuki bila kuwa na tija. Rais anayebana matumizi ya hovyo amebariki ukimbizwe. Ajabu.

Ni vyema Mwenge nao ukafutwa na kuzikwa kabisa, kwani nalo ni jibu, tena limekomaa, tayari kwa kutumbuliwa
Ni upuuzi wa hali ya kuwa ña hilo dudé afadhali hizo pasa zingeenda kuokoa maisha ya watu huku
Vijijini kuna njaa kali
 
Ukimbizaji Mwenge usitishwe mara moja!
 
Hivi hata china hua wanaukimbiza ule wakwao ee!!! Nimeuliza tu maana hua wanasema dunia nzima ni nchi mbili pekee zinazojivunia kwa kua na mwenge wa uhuru.
 
Mimi nimeshiriki sana maandalizi ya mbio za mwenge, mtoa mada na baadhi ya wachangiaji hawana uelewa wa upatikanaji na matumizi ya pesa zinazotangazwa kwenye mbio za Mwenge.
Mwenge hautii hasara serikali, na wala hazikatwi pesa za kazi zingine eti zipelekwe kwenye Mwenge, hapana. Hata hizo sare, tunajinunulia kama vile tunavyonunua sare za sherehe zingine. Mwenge huchangamsha shughuli za maendeleo na kuwapa watu burudani pale unapopita.
Nafikiri wizara husika ianze kutoa somo juu ya mbio hizi kwani kizazi hiki hakina elimu juu ya hii kitu.
Binafsi naona Mwenge uendelee kukimbizwa, ila uwekwe kitaifa zaidi sio kichama wala kijeshi.
Mwenge Oyeee!!
 
Kwa gharama hizi zilivyo kubwa na tulivyo na umaskini huu, sina shaka hata wenzetu wanatucheka sana. Hili la Mwenge liloshapitwa na wakati kitambo sana, ni kama suala la kuhamia Dodoma.
 
B 400 inatosha kujenga daraja mto Magara,kutengeneza barabara kiwango cha lami Mbulu hadi Mbuyu wa mjerumani, Karatu-Mbulu hadi Singida na zahanati 10
 
hata ukizuiliwa bado watu mtalalama tu.
oooh kulikua kuna watu wamejiajiri kupitia mbio za mwenge. na mambo mengine kedekede

Waswahili sisi tuna jema.
Mwenge hauajiri ila wanateuliwa watu 7 tu,wote makada,tutakukagua rinda wewe
 
Back
Top Bottom