Sijajua hao CEO talented unatumia vigezo gani kuwapata..na vipaji unazungumzia ni zile inayotokana na A's za madarasani au kuna kingine?
Yaani tusiporekebisha Katiba yetu ili kuweka mambo chini kama inchi tutazidi kuruka na kukanyagana kama unavyonikanyaga na mada yako hii.. hivi CEO yupi atakua na nguvu mbele ya Waziri kama jambo husika halimpendezi Waziri?
Je utafanya kazi chini ya mkuu wa mkoa anaesema katika ofisi yake anayo wafanyakazi 4 tu? kisa katiba imeshikiliwa na MTU mmoja. Katiba Katiba Katiba jamani tubadilike sana tunataka kua na nchi nzuri
Ni kweli kwamba hatakiwi kupangiwa cha kufanya. Rais yupo sahihi sana. Wewe ungependa kuna anapangiwa cha kufanya?? Kwanini apangiwe?? Nani ampangie??Mbona husikii wewe, mwenyew ashasema hatak kupangiwa cha kufanya mwache eeeh!!!
Naomba niwambie jambo moja ambalo pengine miongoni mwenu wapo wanaofahamu na wengine labda hawajui. Mimi nafanya kazi kama Afisa tarafa huku kasulu,na kambi ya wakimbizi ya nyarugusu ipo ndani ya tarafa yangu.Kwa mazingira haya na nafasi hii napata kukutana na wazungu wengi wa mashirika yanayohudumia wakimbizi kwenye vikao mbalimbali. Jambo kubwa nililogundua ni kwamba wazungu ni wanafiki sana. Wanajifanya very sympathetic kwa waafrika( wakimbizi) kumbe sio kweli. Nasema tena sio kweli kwamba wanatupenda na wanatuonea huruma kwa shida zinazotukabiri hasa wakimbizi. Nao ni wapiga dili tu. Suala la vyombo vya habari vya wazungu kuisakama serikali ya JPM ni dhahiri kuwa wameona kwa trend hii kuna uwezekano tukasimama kwa miguu yetu,jambo ambalo hawataki kulisikia,ninyi nyote ni mashahidi. Kazi kubwa iliyobaki ni sisi wananchi kumuunga mkono rais wetu hasa kwa kuchapa kazi sana ili tuondokane na utumwa huu wa fikra na uchumi ambao kwao ni mtaji. Rais tumemchagua sisi na ni rais wetu na sio wa BBC wala nini. Wanannchi tuna nafasi kubwa ya kumfanya rais wetu afanye kazi kwa kujiamini ili siku moja tuondokane na minyororo hii ambayo kwa sasa tunafungwa vichwani badala ya miguuni. Rais wetu kazi na kasi yako kwangu imetukuka na najiona mwenye bahati kufanya kazi katika kipindi cha utawala wako kwani sikubahatisha kufanya kipindi cha mwalimu nyerere.
Rais wetu amesema vema sana kwamba haya magari yanayotumiwa na mashirika yanayohudumia wakimbizi yakimaliza shughuli zao yasiuzwe Bali zipewe Halmashauri husika,rais akapiga pin magari yaliyotarajiwa kuuzwa mwishoni mwa mwaka jana. Sasa wamekuja na mbinu ya kukodi magari ya watu binafsi ili kumchenga rais. Nikipata nafasi namweleza rais wangu. Haya nayo ni majipu.Kweli kabisa mfano Waingereza wenyewe wanarithishana uongozi afu wanaingilia demokrasia za nchi za Afrika. Hawa watu hawatupendi ila wanapenda mazingira yetu sababu yanawarahisishia kupiga dili zao kilaini.
Inabidi wazungu watulipe kwanza fidia ya utumwa kwa kuwatesa mababu zetu na kuwageuza bidhaa kama condoms kwa zaidi ya miaka 400.
Hujui unataka nini!! Wansema kama hujui uendako,njia yoyote ile inakufikisha.Kwani wanaomsema vibaya Magufuli wazungu tu?
Mbona hata mimi Mtanzania mweusi naona anavyoharibu nchi?