Kila la kheri Mh Rais Dk.John Pombe Magufuli sasa wakati wakuwatumikia watanzania umefika, kwanza katiba ya Jaji Warioba ni muhimu sana kwa watanzania hasa kipindi hiki cha mabadiliko ya kiuchumi,kidemokrasia na kisayasi.
Dunia huru inahitaji Mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kielimu ambayo yataleta mwanga mpya na matumaini kwa watanzania. Fumua mifumo ya kiutendaji ndani ya Serikali, ondoa uteuzi husio na tija hata manufaa kwa taifa,wakati wakupiga marufuku ya magari ya kifahari kwa viongozi na watendaji wa serikali,maboresho makubwa ya vitendea kazi na vifaa tiba kwa hospitali zetu nchini,ongeza nguvu za kifedha kwa Taasisi za ukaguzi wa hesabu za serikali na ile Taasisi ya mapambano dhidi ya rushwaTunaposema elimu,elimu,elimu tunamaana mfumo wa elimu ni wa kwanza kiuchumi,wapili kiuchumi na watatu kiuchumi uchumi wowote duniani hauwezi kukuwa kama watu wake hawana elimu shindanishi katika soko huru na huria katika kujiajiri nakujitafutia mitaji.
Maboresho ya sheria zetu ni muhimu sana. Tunajua watakufuata kuomba msaada wa kuwakumbuka watoto wao kwenye nafasi za uteuzi lasha wengini ni mizigo kwa ukuaji wa uchumi wetu na wengine wamefanya siasa ni ajira tena ili lipo vyama vyote lakini chako kinazidi wakatae maana watanzania 45M ni masikini sana.
Kuna watumishi waliojisahau washugulikiwe hasa nafasi za juu,kodi kumbwa kwa watumishi wadogo hii tofauti inakatisha tamaa na kuvunja moyo sana,ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma bado ni changamoto.
Kwakuwa tunaheshimu haki na demokrasia ya kweli basi ni vyema Zanzibar ikaachwa huru kuamua mambo yake, busara na hekima itumike tukiweka maslahi ya vyama vyetu nyuma. kwanini tumwage damu za watu wasiokuwa na hatia na kamwe hukumu hii sio duniani tuu hata kwa muumba wetu, Zanzibar ni nchi tajiri sana lakini inaitaji hekima na mkono wa Mungu katika kutatua tatizo lake inaumiza haki kuporwa inatesa sana sana,watanzania wengi wanakosa haki zao mbele za mamlaka zilizowekwa kisheria hii inaleta chuki ambayo si vyema kuziendeleza wakati zinaweza kutatulika.
Kila la kheri Amri jeshi wa tano wa Jamuhuri ya watu wa Tanzania
Ujumbe huu nimeukuta mahali uko kwenye social media ulitumwa miaka mitano iliyopita.