Status
Not open for further replies.
Kwanza nianze kwa pongezi nyingi kwa Rais wangu, mambo uliyoyafnya ndani ya miaka mitano kwetu sisi wa TANZANIA tunasema ni Maajabu, umetuheshimisha wa Tanzania leo hii tunatajwa duniani kutokana na msimamo wako mzuri kipindi cha ugonjwa wa Corona, mataifa makubwa mpaka leo wanahangaika lakini sisi tukasimama na mungu na isingekuwa wewe haya yote yasingetokea.

Lakini pia katika uongozi wako umejitahidi kupita kila sehemu, kila sekta Tanzania nzima ili kuhakikisha mambo yanakaa sawa ,hongera sana lakini pia tunakushukuru mnooo...Zawadi yetu sisi wa Tanzania ni kwenda kukupigia kura tena za kishindo siku ya Tarehe 28/10/2020.

Mwisho, nimalizie kwa kusema kuongoza nchi sio kazi nyepesi, na mafanikio hayaji kwa kubahatisha lazima pawepo na mipango.
Lakini pia changamoto hazikosekani ,nini kifanyike kwetu sisi?
>Tumpe ushirikiano wa kutosha kwa Rais wetu pamoja na viongozi wake wote.
>Na tumpigie kura za kutosha ili akamalizie yale mambo ambayo ameyaanzisha
IMG_20201009_121222_150.jpg
 
Kama unahoja ziwasilishe lakini usiingiziee na uongo kuharibu akili za watu, wapi huko watu wanachapwa bakora, Tanzania hii au
 
Utitili wa Flyover uliotajwa na mheshiwa pale kwa mkapa....hivi 2025 dar itaonekanaje...Hebu uchaguzi uishe Rais Aapishe ili ulaya ihamie dar
 
Ungemuomba atumie nguvu yake kusimamia haki

Mbagala wameporwa mbunge wao..

Kuna uchaguzi wa mameya wa majiji...asimamie haki walioshinda ndo wapewe

yasije rudia ya manispaa ya Arusha mjini kuhusu uchaguzi wa meya hasa hapa Dar
Well said!
 
Mheshimiwa kasema hataki vitu vya kupangiwa. Mimi ni nani nimshauri mheshimiwa anayejua kila kitu.
 
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli..
Mimi ushauri wangu mheshimiwa Rais nchi yetu sasa hivi upo mgawanyiko mkubwa Sana. Ameanza na kuunda kamati za amani ili amani iwepo.

Tunaomba aunde kamati zitakazo toa elimu ya uzalendo ilk watu wapende nchi yao. Kizazi kilichopo sasa hakijui tilipotoka wanapotokea matapeli wa kuhujumu uchumi wanabebwa tu.
 
Kila la kheri Mh Rais Dk.John Pombe Magufuli sasa wakati wakuwatumikia watanzania umefika, kwanza katiba ya Jaji Warioba ni muhimu sana kwa watanzania hasa kipindi hiki cha mabadiliko ya kiuchumi,kidemokrasia na kisayasi.

Dunia huru inahitaji Mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kielimu ambayo yataleta mwanga mpya na matumaini kwa watanzania. Fumua mifumo ya kiutendaji ndani ya Serikali, ondoa uteuzi husio na tija hata manufaa kwa taifa,wakati wakupiga marufuku ya magari ya kifahari kwa viongozi na watendaji wa serikali,maboresho makubwa ya vitendea kazi na vifaa tiba kwa hospitali zetu nchini,ongeza nguvu za kifedha kwa Taasisi za ukaguzi wa hesabu za serikali na ile Taasisi ya mapambano dhidi ya rushwaTunaposema elimu,elimu,elimu tunamaana mfumo wa elimu ni wa kwanza kiuchumi,wapili kiuchumi na watatu kiuchumi uchumi wowote duniani hauwezi kukuwa kama watu wake hawana elimu shindanishi katika soko huru na huria katika kujiajiri nakujitafutia mitaji.

Maboresho ya sheria zetu ni muhimu sana. Tunajua watakufuata kuomba msaada wa kuwakumbuka watoto wao kwenye nafasi za uteuzi lasha wengini ni mizigo kwa ukuaji wa uchumi wetu na wengine wamefanya siasa ni ajira tena ili lipo vyama vyote lakini chako kinazidi wakatae maana watanzania 45M ni masikini sana.

Kuna watumishi waliojisahau washugulikiwe hasa nafasi za juu,kodi kumbwa kwa watumishi wadogo hii tofauti inakatisha tamaa na kuvunja moyo sana,ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma bado ni changamoto.

Kwakuwa tunaheshimu haki na demokrasia ya kweli basi ni vyema Zanzibar ikaachwa huru kuamua mambo yake, busara na hekima itumike tukiweka maslahi ya vyama vyetu nyuma. kwanini tumwage damu za watu wasiokuwa na hatia na kamwe hukumu hii sio duniani tuu hata kwa muumba wetu, Zanzibar ni nchi tajiri sana lakini inaitaji hekima na mkono wa Mungu katika kutatua tatizo lake inaumiza haki kuporwa inatesa sana sana,watanzania wengi wanakosa haki zao mbele za mamlaka zilizowekwa kisheria hii inaleta chuki ambayo si vyema kuziendeleza wakati zinaweza kutatulika.

Kila la kheri Amri jeshi wa tano wa Jamuhuri ya watu wa Tanzania

Ujumbe huu nimeukuta mahali uko kwenye social media ulitumwa miaka mitano iliyopita.
 
Ladies and gents Sisi kama watanzania tunakila sababu ya kuipenda nchi yetu, kuonesha uzalendo

Tuna haki ya kujivunia Tanzania yetu.

Ila haki siku zote huambatana na wajibu,tunawajibu wa kuishauri serikali yetu ili viongozi wasiposikiliza ushauri huo tuwe na haki ya kulaumu kinachofanyika, JF ni jukwaa kubwa viongozi watayapata mawazo yetu kupitia humu. Imagine wewe ndo ungekuwa ndo rais ungefanya nini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili? Au ungepata nafasi ya kumshauri rais ungeshauri nini

Naomba tuweke pembeni masuala ya ushabiki wa vyama vya siasa maana MAENDELEO HAYANA CHAMA naomba tuishauri Serikali yetu juu ya mambo mbalimbali

kiuchumi
Kiutamaduni
Kisiasa

Kama taifa bado tunachangamoto nyingi sana mfano Suala la ajira kwa vijana,mifumo ya elimu,umasikini ,miundombinu ,hali za kisiasa nchini,Usalama wa raia na mengine mengi tu.
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom