mkojo wa bhange
JF-Expert Member
- Aug 2, 2017
- 560
- 638
Haujihisi kuwashwawashwa hivi?Natumia nafasi hii kama ilivyoelezwa kwenye katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kifungu cha 18, kipengele cha kwanza ambayo inasomeka hivi nanukuu:
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Mwisho wa kunukuu.
Natumia haki yangu ya kikatiba kama inavyoeleza hapo juu kumshauri rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ni ndugu John Magufuli, kuendelea kudumisha, kuimarisha na kujenga umoja wa kitaifa katika taifa ambalo watanzania sote tulizoea kuishi kwa upendo kama ndugu kwa kuvumiliana na kusikilizana hivyo kushiriki katika umoja wetu huo ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika ujenzi wa taifa letu pendwa vizuri.
Siku zinavyozidi kwenda mbele inedhihirika wazi ule umoja wa kitaifa unasambaratika kwa spidi kali sana na kupotea.
Natoa mfano kwa visa nilivyoshuhudia nikiwa hapa Tanzania, mie ni mkazi wa kijijini sasa kuna sehemu ambako wazee kwa vijana, walikuwa wanakutana kupata supu hapa kijijini kabla wewe rais hujaingia madarakani lakini ulipochukua tu madaraka pametokea mgawanyiko mkubwa sana uliosababishwa na chuki zinazohubiriwa na watawala wa awamu hii na wewe ukiwemo.
Sasa kile kibanda cha supu kimechomwa moto na watu wasojulikana na watu hawachangamani tena kwa pamoja ila wanakaa kusikojulikana kutegemea na mlengo wao wa kisiasa yani mwanachama wa chama A, atakaa na wa chama A wenzake na yule wa chama B atakaa na wa chama B wenzake. Mambo hayakuwahi kufikia hatua hii hapo awali kabla yako madarakani hakika kama taifa tunaelekea kusikojulikana ndugu rais.
Siyo hivyo tu nachosikitika zaidi ni huku kijijini tulikuwa na utamaduni wa kusaidiana kwa hali na mali bila kujali itikadi zetu za aina yoyote ile, lakini ulipoingia madarakani hali imekuwa tofauti sasa watu wanasaidiana kwa itikadi zao za kisiasa tu.
Nimeshuhudia babu yangu akikataa kumuazimisha kitu jirani yake tena kwa kumkaripia kwa maneno makali kuwa jirani yake ni mwanachama wa chama cha kisiasa tofauti na chake hawezi kumsaidia na asimsumbue tena siku nyingine aende kwa wenzake wa chama chake. Hii ni hatari sana watanzania tumefika pabaya.
Nakushauri rais nusuru hii hali kwa kunusuru umoja wetu wa kitaifa, unda kamati ya maridhiano ikijumuisha wakuu wa vyama vya siasa nchini, viongozi wa kidini yani wachungaji, mashehe na maaskofu, watu kutoka asasi za kiraia nk ili kujadili kwa pamoja ili turudishe umoja wetu wa kitaifa tuliozoea kuwa nao hapo awali.
Tanzania ni nchi yetu sote na machafuko yakitokea tutakaoumia ni sisi watanzania siyo watu wa Rwanda au Burundi.
Tutaumia sisi watanzania.
Mungu ibariki Tanzania ,
Mungu ibariki Afrika.
NB:
Natumaini ushauri wangu utakufikia na utachukua hatua.
Lakini naomba univumilie kama nitakuwa nimekukwaza ndugu rais.
anyway...
haudhani pia kuwa ile kauli ya TUSIPANGIANE bado ipo na inakuhusu?
umesema unamshauri kwa mujibu wa katiba?...unadhani vyama vya siasa vimezuiwa kufanya siasa kwa katiba ipi...ni hiyohiyo unayotumia wewe au kuna nyingine inayotumika wewe huna?
...kuwa makini we are not usingvthat katiba ...not to that extent.